Hiki ndicho kinachomfamya Prof. Lipumba kuing'ang'ania CUF na sababu ya kuukana UKAWA

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Haya ni maneno ambayo nimeyapata na kuyahifadhi kutoka kwa wanasiasa wakongwe na wazoefu kabisa wakati wakijadili suala ung'ang'anizi wa Prof. Lipumba ndani ya chama cha CUF na mgogoro unaoendelea hivi sasa.

Inasemwa kua huu mkakati haujaanza leo, alianza kusukwa tangu mwaka 2015 kabla ya uchaguzi mkuu. Tatizo la Zanzibar ndilo ambalo nalo limekuja kukomaza tifu hili la mgogoro ndani ya CUF. Mwanzo kabisa tatizo kubwa lilikua ni ujio wa LOWASSA ndani ya vyama vya UKAWA na kugombea URAIS kupitia CHADEMA.

Ilikuaje? Fuatilia andiko hii kwa makini;

Baada ya Lowassa kutua ndani ya vyama vya UKAWA lilikua ni tukio na tishio kubwa sana na la ghafla lililowatesa sana upande wa pili na kuwafanya kukosa usingizi kwa kukesha wakijadiliana na kupanga mikakati na namna ya kuikabili nguvu yake kwa namna yeyote ile ili kuhakikisha kua anskosa pa kutokea wakati wa uchaguzi mkuu, kuna watu waliishiwa nguvu kiasi kilichowafanya hata kuifikiria kesho yao chini ya Tanzania ya Lowassa na CHADEMA na kukosa majibu.

Mkakati wa kwanza ilikua ni kuwatafuta watu tena viongozi walioamwami na wenye ushawishi mkubwa ndani ya vyama vya UKAWA, mkakati huo ulianza kutekelezwa mara moja kwa Kumnasa aliyekua kigogo mkubwa kabisa wa CHADEMA na aliyekua katibu mkuu wa Chama hicho kwa kumshauri kua aachane na chama hicho kwani hata wao upande wa CCM walidai kua Walimwami sana Dr. Slaa kwa ukali wake wa kukemea ufisadi kwa mana ya kwamba ni bora hata yeye angeshinda Urais wangekua tayari kumpa ushirikiano, haya maneno inasemwa kua yalimkata nguvu kabisa Dr. Slaa bila kujua kua alikua anapakwa mafuta kwa mgongo wa Chupa, yeye aliamini kua wanachokisema CCM ni kweli ndipo akaingia ndani ya msitari na akapigilia msumari wa kua hayuko tayari kumpokea fisadi kama alivyoamini miaka yote.

Wajuzi wa mambo wanasema kua Dr. aliungana na mke wake Mama Mshumbushi kushikilia msimamo huo na hatimaye akabwaga manyanga kwa nafasi yake ya Ukatibu mkuu CHADEMA. Suala la kushawishiwa kukubali kufanya hivyo kwa nguvu ya pesa wujuzi wa mambo anasema lilikua ni siri kubwa ambayo ilifanyika nje ya mpaka ya nchi yetu lakini lilikomazwa zaidi sana na imani ya kupakwa mafuta kwa mgongo wa Chupa kua ni bora yeye angeongoza nchi kuliko fisadi.

Baada ya Dr. Slaa kuondoka, ilitakiwa wafuasi wake washawishiwe kumfuata atakapohamia au kuachana na CHADEMA ikiwa yeye ataamua kufanya hivyo. Kilichowashtusha na kuwaumiza wanaccm ni kwamba wafuasi wengi wa Chadema hawakua na shida na kujiuzulu kwa Dr. Slaa,hii ilileta maana ya kushindwa kufanikiwa kiasi kwa mikakati.

Ikapangwa watoke vijana watakaovishwa mavazi ya CHADEMA kujifanya wanampenda sana Dr. na ionekane kwamba amefanya uamuzi sahihi kujiuzulu kwa ajili ya kutomtaka Lowassa, kufanya hivyo pia kungewaaminisha wananchi wengi kua ni kweli Lowassa hafai wasimpe kura zao lakini kumbe Uongozi wa CHADEMA ulijiandaa imara kulikabili hilo mapema.

ILIKUAJE KWA LIPUMBA?

Namna ya kumnasa huyu bwana haikua tofaoti sana na ya kumnasa Dr, mbinu zilikua zile zile kwa kumwambia "ni bora wewe ungegombea URAIS na ukashinda sisi tungekua tayari kukupa ushirikiano lakini sio fisadi huyu" na kifuta jasho ambacho wajuzi wengi hua hawasemi kwa madai kua hayo mambo yalifanyika kwa siri kubwa sana na hakuna anayejua kiwango halisi alichopokea huyo mheshimiwa na aliyempatia.

Lakini nae Prof baada ya kuona kua kurudi na kuzalizimisha kugombea Urais kupitia umoja huo isingewezekana maana kilichokuwa na nafasi wakati huo ni kuzungusha mikono kama ishara ya kumkubali Lowassa kama mwana mabadiliko,hivyo akaona njia sahihi wakati kwa aliokua nao muda ule ni kubwaga manyanga kwa nafasi yake kama mwenyekiti wa CUF na mwenyekiti mweza wa UKAWA.

Kama ilivyokua kwa Dr kumbe Profesa naye alitakiwa kuondoka na wafuasi watakaosaidia kuzigawa kura ili fisadi asishinde, vile vile wangejitokeza vijana watakaovalia mavazi ya CUF ili kujifanya kua wameudhika na kukarahishwa na fisadi kukaribishwa ndani ya UKAWA. Hili pia halikufanikiwa kwa madai kwamba CUF wao walijifunza baada ya kuona wenzao wa CHADEMA wametikiswa kwahiyo nao walikutwa imara na ni wachache tu walioondoka na Profesa tofauti na matarajio ya upande wa pili.

UNAWEZA KUSTAAJABU;

Kumbe hawa jamaa baada ya kkubwaga ndani ya vyama vyao walitakiwa kurudi baadae baada ya uchaguzi kuisha kwa njia ya kutenheneza influences kwa baadhi ya wanachama kwa angle za madhaifu ya katiba za vyama hivyo,na hii ndio maana hawakurudisha kadi zao baada ya kubwaga manyanga. Kufanya hivyo lengo kuu ni kuiua kabisa nguvu ya vyama hivyo ambavyo upande wa pili unaona bado kwa umoja wao wana nguvu kubwa ya kuiyumbisha serikali.

Kwahiyo njia pekee ni kuwagawa tu na kuwasambaratisha kwa migogoro kama tuvyoiona sasa ndani ya CUF. Inawezekana kabisa hata CHADEMA wasipokua makini kwa sasa kwa kutambua kua kuna madhaifu ndani ya katiba yao yanatafutwa kwa udi na uvumba kwa sasa watokee watu watakaoonekana kua bado wana kiu na Dr Slaa erejee kukiendesha chama tena. Kama hili litashindikana basi inaweza kutafutwa mbinu nyingine ya kuwagawa CHADEMA.

NINI MIKAKATI YA SASA JUU YA UKAWA?

Mikatiti inayosukwa kwa sasa juu ya UKAWA ambao wanaonekana bado kua na nguvu kubwa bara na visiwani ni kuhakikisha umoja huo unasambaratishwa haraka sana kwa kupandiliziwa viruzi wa migogoro ndani ya vyama, Inasemwa kua kitendo cha aliyekua mgombea Urais visiwani Zanzibar Maalim Seif Sharifu Hamad ambayee a naamini kua ndiye mshindi wa Uchaguzi wa October 2015 kuendelea kuzishawishi jumuiya za kimataifa kuzielekeza mamlaka za Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kua aliyeshinda kihalali October 2015 akabidhiwe kiti chake.Pia kufuatia ushawishi huo unaofanywa na mkongwe huyo wa siasa kwa jumuiya za kimataifa,kuna uwezekekano kua endapo maelekezo ya jumuiya hizo za kimataifa hayatatekelezwa kuna uwezekano mkubwa wa Tanzania kwa ujumla kukumbwa na vikwazo vya vya kimataifa vya kiuchumi na mengineyo jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa uchumi wa nchi.

Kiingine ni kujaribu kuuvunja UKAWA ili kupunguza nguvu ya aliyekua mgombea wa UKAWA kupitia Chadema ambaye anatajwa kua bado ni tishio kwa chama tawala na pia bado anao ushawishi mkubwa pande zote mbili za Muungano.Haya yote yanafanyika kwa umakini na ufundi mkubwa kabla ya Uchaguzi mkubwa 2020 ili kukipa nafasi kubwa chama tawala kushinda kiti cha Urais viti vingi vya Ubunge na udiwani.
 
huyu jamaa yuko kama anataka kumpola mtu simu.
FB_IMG_1474770074453.jpg

swissme
 
This is LIVE & Direct bila chenga bila ukuda.......
Ni hivi Daima giza halitoweza shinda NURU.......hawajamaaa hata leo wakisema tuweka gozi kati hata familia zao hazitawapa KURA hakika...yaani 2020 wasahahu kabisaa.
La msingi na la mbolea kwasasa UKAWA ni kuondoa hivi vichaka vidogovidogo kama Propesa Pumba n.k na kuhakikisha tunapata TUME HURU YA UCHAGUZI HAKI YA MUNGU HAKUNA ANAYE ITAKA CCM SIYO KAMA MAGOLI YA MKONO NGOMA ILISHAISHA KABLA HATA YA HALF TIME WANAJUA FIKA.Ndiyo maana wanahofu sana na kujaza upepo mara kwa mara....
 
Hii habar yaukawa kunawakati inatia kinyaa kabsa, issue ya professor lipumba ni issue za CUF kwa muda huu hio ukawa ikae pending kwanza
 
wazee hiyo siku hii hapa.
View attachment 409087
swissme

Nimejiuliza maswali haya mara nyingi (kiasi yanafanana);

1) Kama kweli CCM kinaamini na/au kinajua ni chama kinachoongoza Taifa hili kwa usawa, haki na maendeleo je ni kwanini kimekuwa chama cha kijasusi? Kwanini kimekuwa na hofu kuu kuhusu vyama vya upinzani?

2) Je ni kwanini CCM kinatumia mwavuli wa Serikali na vyombo vyake ili kukilinda kibaki madarakani kimabavu? Je ni kwanini kinaogopa wananchi wale wale ambao kinadai ndio waliokipa kura "za kishindo"? Je chanzo cha mamlaka yao ni kipi basi?

3) Kwanini CCM kisijikite kwenye kuwapa wananchi kiu yao ambayo ni uongozi thabiti wenye uwezo, maono na utashi wa kuliunganisha Taifa hili ili lipige hatua mbele za maendeleo badala yake kimejikita kwenye kuua Upinzani (hasa wa hoja)?
 
Nimejiuliza maswali hiya mara nyingi (yana fanana);

1) Kama kweli CCM kinaamini na/au kinajua ni chama kinachoongoza Taifa hili kwa usawa, haki na maendeleo je ni kwanini kimekuwa chama cha kijasusi? Kwanini kimekuwa na hofu kuu kuhusu vyama vya upinzani?

2) Je ni kwanini CCM kinatumia mwavuli wa Serikali (hasa Polisi katika kukandamiza upinzani) ili kukilinda kibaki madarakani kimabavu? Je ni kwanini kinaogopa wananchi wale wale ambao kinadai ndio waliokipa kura "za kishindo"? Je chanzo cha mamlaka yao ni kipi basi?

3) Kwanini CCM kisijikite kuwapa wananchi kiu yao ambayo ni uongozi thabiti wenye uwezo, maono na utashi wa kuliunganisha Taifa hili ili lipige hatua mbele za maendeleo badala yake kimejikita kwenye kuua Upinzani (hasa wa hoja)?
kwasababu wako na ahadi hewa waizi wa mali za umma na ni vibaka wa demokrasia kwa hiyo lazima wanunue dr na prof uchwara wapenda pesa .

swissme
 
Nimejiuliza maswali hiya mara nyingi (yana fanana);

1) Kama kweli CCM kinaamini na/au kinajua ni chama kinachoongoza Taifa hili kwa usawa, haki na maendeleo je ni kwanini kimekuwa chama cha kijasusi? Kwanini kimekuwa na hofu kuu kuhusu vyama vya upinzani?

2) Je ni kwanini CCM kinatumia mwavuli wa Serikali (hasa Polisi katika kukandamiza upinzani) ili kukilinda kibaki madarakani kimabavu? Je ni kwanini kinaogopa wananchi wale wale ambao kinadai ndio waliokipa kura "za kishindo"? Je chanzo cha mamlaka yao ni kipi basi?

3) Kwanini CCM kisijikite kuwapa wananchi kiu yao ambayo ni uongozi thabiti wenye uwezo, maono na utashi wa kuliunganisha Taifa hili ili lipige hatua mbele za maendeleo badala yake kimejikita kwenye kuua Upinzani (hasa wa hoja)?
Wakikijibu niite.
 
Haya ni maneno ambayo nimeyapata na kuyahifadhi kutoka kwa wanasiasa wakongwe na wazoefu kabisa wakati wakijadili suala ung'ang'anizi wa Prof. Lipumba ndani ya chama cha CUF na mgogoro unaoendelea hivi sasa.

Inasemwa kua huu mkakati haujaanza leo, alianza kusukwa tangu mwaka 2015 kabla ya uchaguzi mkuu. Tatizo la Zanzibar ndilo ambalo nalo limekuja kukomaza tifu hili la mgogoro ndani ya CUF. Mwanzo kabisa tatizo kubwa lilikua ni ujio wa LOWASSA ndani ya vyama vya UKAWA na kugombea URAIS kupitia CHADEMA.

Ilikuaje? Fuatilia andiko hii kwa makini;

Baada ya Lowassa kutua ndani ya vyama vya UKAWA lilikua ni tukio na tishio kubwa sana na la ghafla lililowatesa sana upande wa pili na kuwafanya kukosa usingizi kwa kukesha wakijadiliana na kupanga mikakati na namna ya kuikabili nguvu yake kwa namna yeyote ile ili kuhakikisha kua anskosa pa kutokea wakati wa uchaguzi mkuu, kuna watu waliishiwa nguvu kiasi kilichowafanya hata kuifikiria kesho yao chini ya Tanzania ya Lowassa na CHADEMA na kukosa majibu.

Mkakati wa kwanza ilikua ni kuwatafuta watu tena viongozi walioamwami na wenye ushawishi mkubwa ndani ya vyama vya UKAWA, mkakati huo ulianza kutekelezwa mara moja kwa Kumnasa aliyekua kigogo mkubwa kabisa wa CHADEMA na aliyekua katibu mkuu wa Chama hicho kwa kumshauri kua aachane na chama hicho kwani hata wao upande wa CCM walidai kua Walimwami sana Dr. Slaa kwa ukali wake wa kukemea ufisadi kwa mana ya kwamba ni bora hata yeye angeshinda Urais wangekua tayari kumpa ushirikiano, haya maneno inasemwa kua yalimkata nguvu kabisa Dr. Slaa bila kujua kua alikua anapakwa mafuta kwa mgongo wa Chupa, yeye aliamini kua wanachokisema CCM ni kweli ndipo akaingia ndani ya msitari na akapigilia msumari wa kua hayuko tayari kumpokea fisadi kama alivyoamini miaka yote.

Wajuzi wa mambo wanasema kua Dr. aliungana na mke wake Mama Mshumbushi kushikilia msimamo huo na hatimaye akabwaga manyanga kwa nafasi yake ya Ukatibu mkuu CHADEMA. Suala la kushawishiwa kukubali kufanya hivyo kwa nguvu ya pesa wujuzi wa mambo anasema lilikua ni siri kubwa ambayo ilifanyika nje ya mpaka ya nchi yetu lakini lilikomazwa zaidi sana na imani ya kupakwa mafuta kwa mgongo wa Chupa kua ni bora yeye angeongoza nchi kuliko fisadi.

Baada ya Dr. Slaa kuondoka, ilitakiwa wafuasi wake washawishiwe kumfuata atakapohamia au kuachana na CHADEMA ikiwa yeye ataamua kufanya hivyo. Kilichowashtusha na kuwaumiza wanaccm ni kwamba wafuasi wengi wa Chadema hawakua na shida na kujiuzulu kwa Dr. Slaa,hii ilileta maana ya kushindwa kufanikiwa kiasi kwa mikakati.

Ikapangwa watoke vijana watakaovishwa mavazi ya CHADEMA kujifanya wanampenda sana Dr. na ionekane kwamba amefanya uamuzi sahihi kujiuzulu kwa ajili ya kutomtaka Lowassa, kufanya hivyo pia kungewaaminisha wananchi wengi kua ni kweli Lowassa hafai wasimpe kura zao lakini kumbe Uongozi wa CHADEMA ulijiandaa imara kulikabili hilo mapema.

ILIKUAJE KWA LIPUMBA?

Namna ya kumnasa huyu bwana haikua tofaoti sana na ya kumnasa Dr, mbinu zilikua zile zile kwa kumwambia "ni bora wewe ungegombea URAIS na ukashinda sisi tungekua tayari kukupa ushirikiano lakini sio fisadi huyu" na kifuta jasho ambacho wajuzi wengi hua hawasemi kwa madai kua hayo mambo yalifanyika kwa siri kubwa sana na hakuna anayejua kiwango halisi alichopokea huyo mheshimiwa na aliyempatia.

Lakini nae Prof baada ya kuona kua kurudi na kuzalizimisha kugombea Urais kupitia umoja huo isingewezekana maana kilichokuwa na nafasi wakati huo ni kuzungusha mikono kama ishara ya kumkubali Lowassa kama mwana mabadiliko,hivyo akaona njia sahihi wakati kwa aliokua nao muda ule ni kubwaga manyanga kwa nafasi yake kama mwenyekiti wa CUF na mwenyekiti mweza wa UKAWA.

Kama ilivyokua kwa Dr kumbe Profesa naye alitakiwa kuondoka na wafuasi watakaosaidia kuzigawa kura ili fisadi asishinde, vile vile wangejitokeza vijana watakaovalia mavazi ya CUF ili kujifanya kua wameudhika na kukarahishwa na fisadi kukaribishwa ndani ya UKAWA. Hili pia halikufanikiwa kwa madai kwamba CUF wao walijifunza baada ya kuona wenzao wa CHADEMA wametikiswa kwahiyo nao walikutwa imara na ni wachache tu walioondoka na Profesa tofauti na matarajio ya upande wa pili.

UNAWEZA KUSTAAJABU;

Kumbe hawa jamaa baada ya kkubwaga ndani ya vyama vyao walitakiwa kurudi baadae baada ya uchaguzi kuisha kwa njia ya kutenheneza influences kwa baadhi ya wanachama kwa angle za madhaifu ya katiba za vyama hivyo,na hii ndio maana hawakurudisha kadi zao baada ya kubwaga manyanga. Kufanya hivyo lengo kuu ni kuiua kabisa nguvu ya vyama hivyo ambavyo upande wa pili unaona bado kwa umoja wao wana nguvu kubwa ya kuiyumbisha serikali.

Kwahiyo njia pekee ni kuwagawa tu na kuwasambaratisha kwa migogoro kama tuvyoiona sasa ndani ya CUF. Inawezekana kabisa hata CHADEMA wasipokua makini kwa sasa kwa kutambua kua kuna madhaifu ndani ya katiba yao yanatafutwa kwa udi na uvumba kwa sasa watokee watu watakaoonekana kua bado wana kiu na Dr Slaa erejee kukiendesha chama tena. Kama hili litashindikana basi inaweza kutafutwa mbinu nyingine ya kuwagawa CHADEMA.

NINI MIKAKATI YA SASA JUU YA UKAWA?

Mikatiti inayosukwa kwa sasa juu ya UKAWA ambao wanaonekana bado kua na nguvu kubwa bara na visiwani ni kuhakikisha umoja huo unasambaratishwa haraka sana kwa kupandiliziwa viruzi wa migogoro ndani ya vyama, Inasemwa kua kitendo cha aliyekua mgombea Urais visiwani Zanzibar Maalim Seif Sharifu Hamad ambayee a naamini kua ndiye mshindi wa Uchaguzi wa October 2015 kuendelea kuzishawishi jumuiya za kimataifa kuzielekeza mamlaka za Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kua aliyeshinda kihalali October 2015 akabidhiwe kiti chake.Pia kufuatia ushawishi huo unaofanywa na mkongwe huyo wa siasa kwa jumuiya za kimataifa,kuna uwezekekano kua endapo maelekezo ya jumuiya hizo za kimataifa hayatatekelezwa kuna uwezekano mkubwa wa Tanzania kwa ujumla kukumbwa na vikwazo vya vya kimataifa vya kiuchumi na mengineyo jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa uchumi wa nchi.

Kiingine ni kujaribu kuuvunja UKAWA ili kupunguza nguvu ya aliyekua mgombea wa UKAWA kupitia Chadema ambaye anatajwa kua bado ni tishio kwa chama tawala na pia bado anao ushawishi mkubwa pande zote mbili za Muungano.Haya yote yanafanyika kwa umakini na ufundi mkubwa kabla ya Uchaguzi mkubwa 2020 ili kukipa nafasi kubwa chama tawala kushinda kiti cha Urais viti vingi vya Ubunge na udiwani.
Yaani wewe kwa akili yako uliamini kwamba Lowassa atashinda na kuwa Rais? Basi ulikuwa unaishi kwenye matumaini hewa huku ukisubiri yasiyowezekana!! Pole sana!
 
Back
Top Bottom