mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,307
- 6,514
Stephen Wasira ni mwanasiasa mkongwe. Hata hivyo, Uchaguzi Mkuu 2015 ulimwacha hoi. Alikatwa jina kwenye chama chake (CCM) katika mbio za kuwania tiketi ya kuwa mgombea urais kisha akaangushwa kwenye ubunge.
Wasira alishindwa mwanamke kijana mdogo, Ester Bulaya, walipogombea jimbo la Bunda Mjini. Baada ya hapo zikaanza sarakasi za mahakamani ambako Wasira alishtaki na kushindwa, alikata rufaa na kushindwa.
Mambo mawili zingatia kabla hujaanza siasa. Mosi zina tabia ya kujaza upepo, inawezekana ukawa huna uwezo lakini ukawa tishio kwelikweli. Siasa zinaweza kukufanya ujione unakaribiana na Mungu kutokana na sifa utakazojazwa.
Siasa zinaweza kukupa sifa bora ambazo hustahili, inategemea na jinsi ambavyo upepo umeamua. Kama upepo unakupuliza kwa nguvu, unaweza kuwafanya watu wakuone kwamba hajawahi kutokea mwanasiasa mahiri duniani kama wewe.
Chukua mifano ya karibu kwa Augustino Lyatonga Mrema wa leo. Jinsi ambavyo akizungumza watu wanaulizana “hivi alizungumza nini?” Kwa maana umakini wa watu kumsikiliza Mrema leo ni mdogo.
Mfano wa Mrema na Mkapa
Rudi miaka 21 nyuma kwenye Uchaguzi Mkuu 1995, Mrema alikuwa ndiye nyota wa mchezo katika siasa za Tanzania. Mtindo wa Mrema wa kuhutubia alionao sasa ni uleule wa mwaka 1995, kilichopo ni kuwa kipindi hicho siasa zilimjaza upepo, wananchi walishangilia kila neno lake.
Hivi sasa ule upepo wa kisiasa haujai tena ndani ya Mrema, wananchi hawamhusudu kama ilivyokuwa, kwa hiyo ni rahisi kuyaona makosa yake kila wakati.
Hii ni saikolojia; Makosa ya mwenye kupendwa huwa hayaonekani. Anayependwa anaweza kuboronga lakini anayempenda akapokea katika hali chanya. Hoja za Mrema ni zilezile za miaka yote nyakati hizo kinywa chake kilionekana kama mgodi, kila kilichomtoka mdomoni kilidhaniwa ni dhahabu.
Mfikirie Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, jinsi alivyo na akili, achana na kasoro zake, kwani kila binadamu ana upungufu. Kumbuka kuwa kama siyo nguvu ya CCM na juhudi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mkapa hakuwa na nguvu kumshinda Mrema kwenye uchaguzi.
Watanzania walikuwa tayari kuongozwa na Mrema kuliko Mkapa kwa kuzingatia mvuto wa mtu na mtu. Jiulize leo, je, Mrema alikuwa na uwezo wa kuongoza nchi kwa kuyapima matendo yake ya sasa?
Kabla ya Mrema, marehemu Mchungaji Christopher Mtikila alipozungumza, maneno yake yalitoboa ubongo wa vijana ambao walipotoka Viwanja vya Jangwani kumsikiliza, moja kwa moja waliingia mitaani na kusababisha taharuki. Ila Mtikila alifikwa na mauti akiwa mwanasiasa asiye na ushawishi kabisa.
Upepo wa siasa huweza kumfanya mtu awe sawa na malaika. Akikohoa watu wanamsifu “anakohoa vizuri”, akiwa mchafu, hajijali, watu watamfurahia “hana makuu.”
Siasa huisha muda wake
Jambo la pili la kuzingatia unapoingia kwenye siasa ni kutambua kuwa siasa huwa na muda maalum, yaani zina ‘expire date’. Unaweza kuwa mwanasiasa tishio mpaka taifa likawa haliwezi kuzungumza siasa bila kukutaja lakini mwisho ukifika utasahaulika kabisa.
Usiingie kwenye siasa ukiamini kuwa utakuwa mkubwa kuliko wote kisha utadumu mpaka kifo kitakapokuondoa duniani, utajidanganya. Siasa usiziendee kwa miguu yote miwili, jiwekee akiba ya kuishi pembeni nje ya siasa.
Unaweza kuingia kwenye siasa lakini ukiwa umepishana na upepo, hata ufanye matukio gani utaonekana wa kawaida tu. Wenye upepo wakigusa tu hao wanang’ara, wewe unajiuliza mbona unafanya kazi kubwa na haipewi uzito unaostahili?
Hilo ni angalizo, kwa maana siasa ni mchezo wa “ujanja kupata” siyo “kupata ni uwezo”, wengi tu wenye uwezo wao hawakuwahi kuaminika. Marehemu Prof Leonard Shayo alikuwa msomi mkubwa.
Hata hivyo, katika mbio za urais mwaka 2005, Prof Shayo alikuwa kati ya wagombea walioburuza mkia, nyuma ya akina Mrema, Freeman Mbowe (Chadema), Prof Ibrahim Lipumba (Cuf), marehemu Dk Sengondo Mvungi (NCCR-Mageuzi) na kadhalika. Usimtaje Dk Jakaya Kikwete ambaye ndiye alishinda.
Bila shaka Shayo kupitia chama cha Demokrasia Makini, aliamini kwa uwezo wake angeweza kukubalika kwa urahisi. Hakujua kuwa siasa ni upepo, na upepo ulimjaza kweli Dk Kikwete kiasi kwamba alipata kura zaidi ya asilimia 80. Uchaguzi Mkuu 2010, upepo wa JK ulipungua akapata kura asilimia 61.
Turudi kwenye kipengele chetu, siasa huwa zina muda maalum, ukishaisha unaweza kushangaa. Muda wa Mrema uliisha ndiyo maana leo hachukuliwi kama mwanasiasa wa kupigiwa makofi. Ni zamu ya wengine.
Ukivuma sana jiandae kufifia
Katika siasa, ukishafanikiwa kuuteka umma na kukuelekea, anza kujipanga kukabidhi kijiti na ujiweke pembeni. Wanasiasa ambao walijiweka pembeni na kubaki kuwa washauri wakati bado wana uwezo, wamebaki na heshima.
Muone Edwin Mtei anavyoheshimika Chadema. Wafikirie akina Dk Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Warioba, Dk John Samuel Malecela, Pius Msekwa na wengine CCM. Wanaendelea kuheshimika kwa sababu walikubali kukaa pembeni kipindi ambacho walikuwa na uwezo wa kuendelea kupambana.
Mtazame Lipumba alivyokuwa akichukuliwa kama alama kuu ya Cuf, na leo anavyochukuliwa. Katika siasa za Tanzania kabla Nape Nnauye katika nafasi ya ukuu wa idara ya Itikadi na Uenezi CCM, alishakuwepo Omar Mapuri, jiulize amekwenda wapi? Nape naye kampisha Humphrey Polepole.
Kutotambua kuwa ukuu wa kisiasa una ‘expire date’ ni janga ambalo huwatesa wengi. Siasa hulazimisha wanasiasa kupumzika. Na upepo wa kisiasa huwa unazunguka. Ni kama ambavyo itafika wakati Tundu Lissu atazungumza na wenye kumuona kamanda leo, hawatayashika anayoyasema kwa umakini kama ilivyo sasa. Upepo utakuwa umekwenda kwa wengine.
Siasa usiitolee machozi
Jambo la tatu ni kuwa siasa usiitolee machozi. Ukiadhiriwa kwenye ulingo wa kisiasa fahamu kuwa ndiyo tabia yake. Wenye shahada zao za uzamivu (PhD) wengi tu wameshawekwa benchi na wenye elimu ya msingi tu.
Usiumie sana kutochaguliwa, ukahisi kuwa labda hukujenga hoja zenye kueleweka au ulipungukiwa uwezo wa ushawishi. Elewa kuwa wanaosikiliza hoja ni watu na huchagua cha kusikiliza au wanaweza kusikiliza lakini akachagua cha kutunza kichwani. Kuelewa ni utashi.
Na kwa sababu wanaosikiliza kwa utashi wao huamua nani wayapokee maneno yake, ni hapo mtu mwenye kuzungumza pumba anaweza kupigiwa makofi na kuchaguliwa, wewe na pointi zako zote ukakataliwa. Hilo lisikuumize, wanaochagua wana utashi wao.
Ndiyo maana nimesema kuwa usiende kwenye siasa kwa kuingiza miguu yote miwili. Pima upepo kwanza, mguu mmoja utakaouacha nje, utakusaidia kukukwamua upepo wa kisiasa utakapokukataa.
Katika siasa muhimu zaidi chukua hii; Tumia mguu mmoja kupima kwanza kina cha maji baharini ukishajiridhisha ndiyo ujiachie majini. Na wakati ukionesha umahiri wako wa kuogelea, kumbuka mahali ambapo ulihifadhi nguo zako ufukweni, maana baada ya kuogolea utatakiwa kuvaa nguo zikutunzie heshima nje ya bahari.
Mwanasiasa tunza nguo zako nje ya siasa ili zikufae. Wanasiasa wengi wakishaingia kwenye siasa husahau mahali ambapo waliacha nguo zao ili ziwafae wanapotoka. Tena wengine hugawa kabisa wakiamini kuwa wataogelea kwenye siasa mpaka mwisho.
Hata uwe mkuu wa kiasi gani kwenye siasa, ipo siku utatoka. Ndiyo maana alipita Mwalimu Nyerere, akafuata Ali Hassan Mwinyi, akatokea Mkapa, Novemba 5, 2015, Dk Kikwete alimkadhi rungu Dk John Pombe Magufuli ambaye naye muda wake utafika, na atakabidhi mamlaka kwa mtu ambaye atafuata.
Hivyo basi, siasa kwa upepo wake huvimbisha sana vichwa lakini vizuri kuzingatia kuwa siasa zina expire date. Ukiwa mwanasiasa tenda mema na ujiandalie pumziko, vinginevyo heshima kubwa ambayo unayo leo kesho hugeuka dharau kubwa.
Lowassa kama Dk Slaa
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, alikuwa ni kila kitu kwenye siasa za Chadema na upinzani nchini. Hata hivyo, upepo wa ghafla wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ulikatisha ukuu wote wa Dk Slaa.
Lowassa alipohamia Chadema, papo hapo na Dk Slaa akaonekana siyo ‘bidhaa’ bora sokoni. Uamuzi wa Dk Slaa kustaafu siasa ulikuwa wa heshima sana. Vinginevyo angeendelea kupambana angeweza kuvuna moja kati ya mawili; heshima au dharau.
Ni kwa kanuni hiyohiyo, itafika siku pia Lowassa aliyetikisa nchi Uchaguzi Mkuu 2015 atapoa. Kama ambavyo Dk Slaa alivyo kimya leo, Lowassa pia atakuwa kimya. Hiyo ndiyo siasa.
Chanzo:Maandishi Genius