Kati ya prof. Lipumba, James Mbatia na dk Slaa nani anafaa kupeperusha bendera ya UKAWA

Poll: Kati ya prof. Lipumba,James Mbatia na dk Slaa nani anafaa kupeperusha bendera ya UKAWA

  • Dr. Slaa

    Votes: 49 87.5%
  • Prof. Ibrahim Lipumba

    Votes: 6 10.7%
  • James Mbatia

    Votes: 1 1.8%
  • Emmanuel Makaidi

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    56
  • Poll closed .
UKAWA Isifanye kosa kumsimamisha DR. Slaa ,Lipumba au Mbatia.
Hawa wote wana ukomo wa kukubalika.
Hili halina ubishi.Kuing'oa CCM ni kazi pevu inayohitaji maono ya kutafakari sana na maarifa makubwa ya sayansi ya siasa na jamii.

Hii nchi ina tatizo kubwa kwenye madaraka ukicheza vibaya hupati kitu.
Kampeni chafu zilishajenhwa na zitajengwa zaidi na CCM za padri kuongoza nchi yenye waislam 35-45% . Hapa hakuna muislam atakayemchagua Dr.Slaa milele
Hali kadhalika Lupumba alishachafuliwa na CCM kuwa ni mdini na mpaka video yake ikaonyeshwa.

.Tusijidanganye CCM ilishaweka misingi mikubwa ya kucheza na neno udini hapa Tanzaniana na kuzitoa hizo propoganda ni mpaka ccm itoke madarakani na katiba yao inayowapa watawala nafasi za kuwa miungu watu.

Pili ukanda anaotoka Dr.Slaa na Mbatia unapigwa sana vita na makabila madogo yaliyobaki nyuma kimaendeleo na kielimu. Na ikumbukwe kuwa umaskini na Elimu ndogo ni mtaji mkubwa wa CCM.

Lipumba naye hana mvuto mana hata Ukanda wake wenye watu zaidi ya mil.6 haujawahi kumpa hata kura laki tatu.

Hapa pasipo na shaka Kwa sasa kwenye UKAWA Tundulisi ndiye anayefaa zaidi kuleta ushindi wa kishindo.Ataongeza idadi kubwa ya wapiga kura .Nimepita sana vijiji Tundulisu anatajwa zaidi kwenye ukawa kwa vijana.
Zito kabwe umri na misimamo yake isiyoeleweka inamkosesha urais.


Mzee digits....Kwa sasa ni Lissu na Dr Slaa tu
 
Simpigii kampeni wala simuungi mkono. Wala kura yangu hatapata. Lakini,nasema ukweli. Ukweli kumhusu kama mgombea tusiyemtaka aje kutokea upinzani. Vikaoni,mikutanoni na mabarazani mwetu tunamtaja na kumjadili. Tunamjadili kwa mipango ya viwango lakini yenye kingo. Huyu Dr. Slaa wa CHADEMA ni tishio.

Sio kwamba anatutisha saaaaaaana.Wala. Lakini, ni wa kumchunga kama Messi wa Barcelona au Ronaldo wa Real Madrid.Ni hadi mpira uishe. CCM imejipanga kumpata mgombea ambaye hata akiletwa Dr.Slaa wa CHADEMA, kama mgombea wa UKAWA, mambo yatakwenda vyema badala ya mrama. Hatujisumbui kuomba na kukesha kumkwepa Dr.Slaa.Aje tu.Atakutana na..............kama mgombea wetu imara.

Pamoja na yote, mazuri na mabaya yake, Dr. Slaa ni tishio. Ana mtaji wa kura za 2010, ushawishi na mengineyo. Niye hasa anaouweka kweye alert ya kupata mgombea imara na anayekubalika ili tusiyumbe au kuanguka kabisa. Kutoka UKAWA wapo wengi wa kuwachunga kama wakigombea lakini huyu Mkaratu ndiye Captain wao. CCM ikiteleza kupata 'mgombea' itaishia kusema: usiyempenda kaja.

Someni na muelewe. Huo ndio ukweli!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Mkuu umeongea jambo la mbole
Jambo ambalo vijana na wazeee wa CCM hawataki kulisikia
Hivi punde utawaona vijana wako wa CCM watakavyomiminika humu kwa matusi na kejeli kwa Dr Slaa
Hawataacha kuongelea swala la kuoa,swala la amechoka na blablah nyingine
Hawana Jipya
Watanzania Tumaini letu Jipya ni CHADEMA
Tumaini letu ni UKAWA

Forward Ever,Backward Never
Freeland wa JF
 
Mkuu umeongea jambo la mbole
Jambo ambalo vijana na wazeee wa CCM hawataki kulisikia
Hivi punde utawaona vijana wako wa CCM watakavyomiminika humu kwa matusi na kejeli kwa Dr Slaa
Hawataacha kuongelea swala la kuoa,swala la amechoka na blablah nyingine
Hawana Jipya
Watanzania Tumaini letu Jipya ni CHADEMA
Tumaini letu ni UKAWA

Forward Ever,Backward Never
Freeland wa JF

Mkuu tayari Laki si fedha ameshaanza na nimeona anawapigia simu Lizabon, simiyu yetu, faizafoxy, juliana shonza na wengine ili kuendeleza santuri iliyochuja na kuchakaa ya kuwabanjua wake za watu. Huyu Dr ni tishio kubwa kuliko sunami na mwaka huu atatinga magogoni kiulaiiini kama ananawa vile.
 
Sasa iko dhahiri kwamba watu wameichoka ccm wangependa wapate mmbadala wake ili ikajifunze ikiwa nje ya ulingo. Kikubwa tu ukawa mtuletee watu wanaokubalika maeneo husika kuanzia udiwani ubunge hadi urais. Chama cha mapinduzi kimelegalega na kimesahau kwamba nchi ni ya wananchi si ya viongozi peke yao.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom