Kati ya Oppo na Samsung ipi nzuri kutumia?

Eeh hio sina wasiwasi itakuwa nzuri tu! Flagship zao zikogi vizuri!

Yani kuliko nikanunue A21, A51 sijui ni aheri ninunue S8 Plus, S9 plus au S10. These were the best built phones kuliko hizo nyenginezo za low range zilizotoka sasa
Kwanza hawatengenezi wao 😂😂 wenyewe! Juzi nilikuwa na a51, wanasema ni super amoled lakini siioni ile super amoled mule
 
Kwanza hawatengenezi wao 😂😂 wenyewe! Juzi nilikuwa na a51, wanasema ni super amoled lakini siioni ile super amoled mule
Hamna super amoled kioo kimepauka kinoma yani ukiilinganisha na S8 ni mbingu na ardhi 😅😅😅 ndio maana nakwambia Samsung kama sio flagship save pesa yako tu maana uhakika ni kwamba haitakaa na chaji na itakuboa tu
 
Mkuu samsung bado ni simu nzuri parefu sana aseee, nimeona unasema hazitunzi chaji sijui za wengine hizo, lakini M20 yangu ya mwaka 2019 inatunza chaji sijawahi ona, na data on mda wote.
Hio simu ni midrange na emphasis ilikuwa kwenye battery! Siwezi shangaa kwa simu yenye 5000mAh kukaa na chaji
 
Ndio nafahamu, na nimeitumia yangu kama mfano kwenye suala la chaji, ambalo nadhani ilikuwa hoja kuu.
Ni chache sana lakini! Na trend iliokwisha zoeleka ni kuwa Samsung na pawa bank ni kama Waya na kichwa cha charge lazma viwe complemented!
 
hahahahah sahizi naona kuna mediatek wide dimension ndio zinasumbua sokoni! Dimensio 1000, 800
Dimensity 1200 iko very impressive. Ikipita miaka 2 naanza kununua simu zA mediatek. Pia kuna Dimensity 900 ambayo inachuana na midrange ya SD kama 765G
 
Dimensity 1200 iko very impressive. Ikipita miaka 2 naanza kununua simu zA mediatek. Pia kuna Dimensity 900 ambayo inachuana na midrange ya SD kama 765G
Yah inaonesha anything 800 or above iko na performance nzuri
 
Acha ushabiki mandazi wewe! Samsung simu zake bora ni ile top of the line tu sijui ni S21ultra na zote zilizowahi kukaa katika hio rank!

Zingine zote ushuzi tu hasa camera na battery! Wanabadilisha makasha na size ya vioo tu! Na sahizi wameamua kuleta simu zenye mediatek chips kama walivyo akina tecno tu!
Ndugu kuna simu za makundi matatu samsung.

Kuna highend yaani S na note.

Kuna midrange hapo A series kubwa kama a50,51,52,70,71,80,s10e nk.

Halafu kuna lowend,huku unawakuta akina a10,20,02,21,a30 nk

Sasa tafuta oppo yako zote utakuta zinaishia kati hapo kwa ubora ila wana bei sana hawa jamaa oppo.
 
Mkuu samsung bado ni simu nzuri parefu sana aseee, nimeona unasema hazitunzi chaji sijui za wengine hizo, lakini M20 yangu ya mwaka 2019 inatunza chaji sijawahi ona, na data on mda wote.
Pia hazina matatizo ya kijinga jinga.
 
Ndugu kuna simu za makundi matatu samsung.

Kuna highend yaani S na note.

Kuna midrange hapo A series kubwa kama a50,51,52,70,71,80,s10e nk.

Halafu kuna lowend,huku unawakuta akina a10,20,02,21,a30 nk

Sasa tafuta oppo yako zote utakuta zinaishia kati hapo kwa ubora ila wana bei sana hawa jamaa oppo.
Simu ya uhakika oppo hawatumiagi soc za kindezi
 
Simu ya uhakika oppo hawatumiagi soc za kindezi
OPPO ni hatari na nusu Mzee, nimeinunua ya kiwango cha chini kabisa RAM 2, GB 32 320,000/= pale China Plaza Kariakoo lakini kiukweli kwa betrii kukaa na chaji muda mrefu, chaji kichaji kwa muda mfupi, camera, fast internet, screen display wako vizuri sana kupita maelezo.

Nimeamua naiuza hii hata kwa 280,000/= kwa mtu nachukua ile ya RAM 4.

OPPO NI BORA SANA KAKA.
 
Hawana ubabaishaji hao jamaa! Simu zao ni ghali ila ni nzuri battery zinakaa chaji mpaka unapenda
 
Dimensity 1200 iko very impressive. Ikipita miaka 2 naanza kununua simu zA mediatek. Pia kuna Dimensity 900 ambayo inachuana na midrange ya SD kama 765G
Siku hizi Qualcomm Ana RE use Flagship Soc kwa kuzi rename na kutumika kwenye midrange na upper midrange.

Mfano snapdragon 870 ama 860, ngumu ku recommend dimensity 1200 over sd 870, hasa vile Mediatek wana limitation za kutokua na drivers nzuri za Open Gl na kutotoa source code kwa developers.

Ila kwangu mimi low end ndio wamejitahidi, soc kama G80 ama G70 zinasaidia sana kwenye simu za laki 3 kushuka, leo kuna Redmi 9 yenye G80 ambayo ni bora kuliko snapdragon 400 series yoyote ile Ukitoa 480G.
 
Back
Top Bottom