Kati ya Mbagala na Gongo la Mboto wapi kuna watu wengi?

Kati ya Mbagala na Gongo la Mboto wapi kuna watu wengi?

Issue iko hivi mbagala ina watu wengi sana kuliko ukanda wa goms ila ukweli ni kwamba wakazi wengi wa mbagala mission zao zinaishia mbagala na wengi ni jobless hawaendi sana mjini na maeneo mengine ila gongo la mboto haina watu wengi sana ila ina mission town wengi wanaofanya kazi sehemu tofauti tofauti kama unabisha fanya research nenda mjini anza kuuliza makazi ya watu wengi itagundua wanaishi gombs
Umeongea ukweli
 
Wakuu mambo vipi?

Nawasogezea mada hapo ni hivi kati ya Gongo la mboto (Goms) na Mbagala(Mbajara in mateja voice) je ni sehemu gani ina watu(nyomi) wengi kuliko mwenzie ukija na hoja yako weka na sababu.

Binafsi na naanza na Mosi kusema Gongo la mboto ina watu wengi kuliko Mbagala kwa sababu Gongo la mboto kuna treni la mwakyembe ambalo lililetwa naamin linabeba sio chini ya watu buku au zaidi kwa tripu moja na kwa siku linapiga tripu 3 asubuhi na tripu 3 jioni ila pamoja na hivyo bado daladala za kkoo na posta zinazoenda Gongo la mboto zanapiga kazi kama kawaida wakati mbagara majuzi Mwendokasi wamefanya majaribio madaladala wameeanza kulia kulia abiria hakuna.

Mbili Mbagala wengi sio wakazi wa pale wengi wanatoka mikoa ya kusini kuja kufanya biashara na kutawanyika makwao wakati Gomsi ni makazi ya watu na Gari za Mbagala kwenda gomsi jioni hazikamatiki.

Yote kwa yote kwenye madaladala kuna vituko na vimbwangwa sana.

Nawasilisha.
mtakapomaliza hii ligi yenu mtuambie.
 
Gongolamboto nafahamu Kuna benki mbili tu NMB na CRDB. Goms imepakana na mkoa wa pwani wilaya ya kisarawe. Goms Kuna kikosi cha jeshi JWTZ na chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala. Eneo karibia lote la goms ni skwata halijapimwa. Hakuna hoteli yoyote ya nyota za juu zaidi ya lodge na guest house. Wakazi wengi wa eneo hili ni wa kipato cha chini. Hakuna muhindi, muarabu au mzungu anayeishi goms isipokuwa awe anaishi katika taasisi ya chuo kikuu au jeshini. Mengineyo madada poa, mashangazi, mapusha na mateja wapo kitaa.

Mbagala Kuna benki kama zote CRDB, NBC, AKIBA, NMB, KCB, DCB pia mbagala imepakana na mkoa wa pwani wilaya mkuranga pamoja na njia kuu ya mikoa ya kusini mtwara na Lindi bila kusahau ndio njia ya kuingia Msumbiji na kufanya muinguliano wa kibiashara. Mbags pia Kuna kikosi cha JWTZ. Mbags hakuna hoteli yoyote ya nyota za juu pia sijawahi kuona mzungu, muindi akiishi mbagala isipokuwa kwenye taasisi kama ya misheni ndio unakutana na wazungu au wageni kutoka nje ya nchi. Mbags eneo kubwa ni skwata halijapimwa isipokuwa sehemu ndogo sana ndio imepimwa. Kipato cha wakazi wa mbags ni wa kipato cha chini. Mengineyo pisi Kali zipo za poa sana pia mateja, mapusha, mashangazi, madada poa wapo kibao ni wewe tu na waleti Yako.

Mbags Vs Goms wapi Kuna idadi kubwa ya watu?
 
Kati ya hizo sehemu nyama zisizo eleweka wapi zinakwenda mfano utumbo,miguu ya kuku,vibudu,dagaa wengi sio samaki wakubwa,vyumba unafuhuu
 
Back
Top Bottom