Kati ya Lissu aliesema "tutakinukisha" na wanaotuhumiwa kuingiilia mifumo ya uchaguzi kwa mujibu wa Polepole, nani anapaswa kushitakiwa kwa uhaini?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,144
Reaction score
162,539
Baada ya Polepole kutoa tuhuma nzito za mifumo ya uchaguzi kuingiliwa huku akitaka uchunguzi huru utaohusisha vyama vyote ufanyike ili umma ujiridhishe kama alichosema ni kweli au laa, nimejikuta na hili swali hapa chini:

Kama Lissu anashitakiwa kwa tuhuma za kusema atakinukisha kuvuruga uchaguzi; je, hawa wanaotuhumiwa kuingilia mifumo ya uchaguzi kwa kuiunganisha na chama fulani cha siasa, wao hawastahili kushitakiwa kwa uhaini?
 
Polepole na Lissu, ni project ya Mwenyezi Mungu, wanaopambana na hawa watu, wajue wanapambana na Mungu na ndio maana hali iko hivi.

Ni Mungu huyo huyo aliewapa watu fulani viburi vya kutomsikliza Polepole mpaka akafikia hatua ya kutoa siri ili tu umma wa watanzania ujue kinachoendelea.

Hata Farao alijawa na kiburi ili baadae aanguke.

Mungu fundi sana!
 
Wanqoingilia mfumo wa uchaguzi
 
Jana (juzi) wakati anatangaza kuhusu press ya leo alisema mambo mawili ambayo nimeyapatia majibu leo:

1) ^Kwa namna ambayo pengine sitaieleza vizuri^ (kitu kama hicho), ^TAL aachiliwe bila masharti yoyote.^

Implication: kuna tuhuma kubwa zaidi dhidi ya washtaki (hili bomu la leo) kuliko lile analodhaniwa kutenda mshtakiwa (uhaini).

2) ^Mama Samia, waulize watu wako (CCM) eti kuna kitu anachojua Polepole kinachoweza kuleta madhara?^
 
CCM kwa hili MCHUTAME...Uchaguzi usogezwe mbele..iteni Meza ya Mazungumzo ya dhati , mtupatie Katiba Mpya iliyo BORA na Tume huru kwelikweli ya Uchaguzi....

Jaji Mwambogele Wa Mahakama ya Rufaa na Mwenyekiti NEC "Huru" kulinda hadhi ya nchi, hadhi ya Mahakama na hadhi yako mwenyewe JIUZULU
 
Ila alichosema leo sio tuhuma bali katoa siri kubwa ya wizi wa chaguzi
 
Hawakutarajia kabisa kama Polepole angelisema hili alililolisema leo.
 
What's a way forward after disclosure of this very confidential info?
Mkuu hapa ni kujipanga tu, kuwang'oa wadhalimu ukiniuliza how ntakujibu "I don't know" , lakin either way these goons must go kwakweli..The more they stay the more they fuckup this country...
 
Aisee hili ni bomu kubwa sana kuliko yote, yatakayofuata yatakuwa ni matokeo ya hili bomu. HAYA WATANZANIA TUMESHAJUA KITULACHO, NINI CHA KUFANYA SASA?
 
Niliwahi kumhoji mjumbe wa nyumba 10 kwanini alikuwa anadai apewe namba Za Nida, akiwa anapita mtaani kwetu na wale watu wa kufunga anuani za makazi. Ilinipa mashaka sana hiyo...kumbe mifumo yote imeungwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…