Katazo la uvutaji sigara katika maeneo ya umma, Wizara ya Afya yampongeza Makonda

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
logo.jpg

Wizara ya Afya, Maendejana ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inampongeza Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kupiga marufuku matumizi ya Shisha na uvutaji wa Sigara hadharani kama afua ya kupunguza madhara ya tumbaku na madawa ya kulevya katika jamii.

Uchunguzi wa kitalaam uliofanyika umebaini kuwa Shisha ina madhara kwa afya ya watumiaji hasa vijana na watoto. Watumiaji wa Shisha wanatumia kiwango kikubwa cha tumbaku kwa muda mfupi, hali inayoongeza madhara yatokanayo na tumbaku kama vile: – Saratani, Magonjwa ya Mapafu, Kibofu cha mkojo, Tezi dume, Koo, Mdomo na Kiywa, Ngozi, Ini, Ubongo.

Pia imebainika kwamba matumizi ya Shisha huambatana na kuongezewa dawa nyingine za kulevya na hivyo hufanya watumiaji wa Shisha kupata uraibu wa dawa za kulevya. Matumizi ya dawa hizo za kulevya ni kosa la jinai.

Wizara ya Afya, Maendejana ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kurejea na kusisitiza agizo lake la tarehe 12 Machi 2015 la kuzuia matumizi ya sigara na matumizi ya bidhaa za tumbaku katika maeneo ya umma

Inakumbushwa kwamba agizo hili limezingatia utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Bidhaa za Tumbaku, Sura ya 121 T.L 2002, ya Sheria za Tanzania kipengele cha 12 (1) ambacho kinakataza matumizi ya Tumbaku katika Maeneo ya Umma.

Madhumu ya Agizo hili ni kuilinda Jamii kwa ujumla kutokana na madhara yatokanayo na moshi wa sigara. Wizara inawakumbusha wananchi wanaotumia bidhaa za tumbaku kupunguza au kuacha kabisa matumizi ya tumbaku. Aidha, agizo hili linaijumuisha jamii yote katika kubaini madhara ya tumbaku na umuhimu wa kuzuia matumizi ya tumbaku katika maeneo ya kazi na maeneo yote ya umma.

Agizo hili linawahusu wananchi wote nchini wanaopata huduma katika maeneo ya umma kama ilivyotafsiriwa na sheria husika.

Matumizi ya tumbaku hayaruhusiwi katika maeneo yote ya umma. Maeneo haya yanajumuisha ofisi zote za Serikali na tasisi zake zote, watu binafsi, vyuo, vituo vya huduma za Afya zikiwemo Hospitali, vituo vya Afya na zahanati, vituo vya usafiri wa Anga, Mabasi, bandari na treni, sehemu za mikutano, mapumziko, bustani na fuko za maji,sherehe,michezo,masoko,maduka makubwa pamoja na sehemu za kuabudu.Na kwa mtu yeyote anayeendesha shughuli katika maeneo ya umma analazimika kutenga eneo maalum kwa ajili ya wavuta sigara.

Kwa kuwa Mhe. Waziri mwenye dhamana na masuala ya Afya nchini ameona hatari hii ya Uvutaji wa sigara na utumiaji wa bidhaa za tumbaku kwa afya ya Wananchi, kuanzia jana tarehe 4/7/2016 matumizi ya Shisha nchini yamepigwa marufuku kwa wote wanaojihusisha na matumizi hayo, na kwa wafanyabiashara wote wanaojihusisha na upatikanaji wa Shisha nchini

Hivyo basi, kwa agizo hili katika maeneo yote nchini ambako matumizi ya Shisha hufanyika ni marufuku matumizi hayo kuendelea kutumika.

Aidha vyombo vya Dola na mamlaka husika vinahimizwa kusimamia kwa ukamilifu katazo hili.(P.T)
 
Lazima wampongeze mana ni moja ya Ilani ya CCM..mambo makubwa yanawashinda mnakimbilia huku kwa wavuta sigara.
 
Da Kauli ya Mkuu wa Mkoa Mh Makonda inakuwa kauli ya Serikali na kupewa nguvu na Wizara ya Afya nzuri zaidi na Waziri Mkuu anaibeba kama tamko la Serikali,kwa Jicho la tatu na la kipekee Makonda ana nafasi kubwa kwa Mkuu wa Nchi kuwazidi Mawaziri Mh Rais aangalie aina ya mfumo wa Uongozi wake na wasaidizi wake,kwa Mtindo huu Makonda anaweza kudumu kwa serikali hii kwa Muda Mrefu.
 
Lazima wampongeze mana ni moja ya Ilani ya CCM..mambo makubwa yanawashinda mnakimbilia huku kwa wavuta sigara.
Wewe BAVICHA akili zinazidi kuyoyoma kwa kasi ya ajabu. Njoo tukutane dodoma ili mpime kanguvu kenu na nguvu kubwa ya UVCCM.
 
Da Kauli ya Mkuu wa Mkoa Mh Makonda inakuwa kauli ya Serikali na kupewa nguvu na Wizara ya Afya nzuri zaidi na Waziri Mkuu anaibeba kama tamko la Serikali,kwa Jicho la tatu na la kipekee Makonda ana nafasi kubwa kwa Mkuu wa Nchi kuwazidi Mawaziri Mh Rais aangalie aina ya mfumo wa Uongozi wake na wasaidizi wake,kwa Mtindo huu Makonda anaweza kudumu kwa serikali hii kwa Muda Mrefu.
Makonda ndiye rais wa Dar. Au hujui?
 
kuna kitu nakiona shisha itapanda chati na itakuwa na thamani na kuwa kama madawa ya kulevya kwa sababu itakuwa ni kituadimu,ili kitu kiwe na thamani lazima kiwe adimu au kiwe haramu,cocain,kitimoto,bangi,tanzanite,gongo etc
 
Waziri Mkuu Apiga Marufuku Matumizi ya Shisha Nchi Nzima..

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amepiga marufuku matumizi ya shisha na kulitaka Jeshi la Polisi kufuatilia kutokomeza matumizi hayo ili kuwaokoa vijana.

Ameongeza kusema kuwa shisha ni aina ya tumbaku inayokuwa na ina mchanganyiko wa vilevi mbalimbali kama gongo na viroba na mtumiaji anapotumia kilevi hicho hukosa nguvu na hutaka kutumia kila siku na kufuata popote...
 
Kwa tafsiri ya maelezo hayo hapo juu, "ni kosa la kisheria kwa MTU YOYOTE kuvuta sigara ndani ya gari ya SERIKALI au kampuni ama taasisi yoyote. Waandishi wa habari kaeni na kamera zenu tayari.
 
Da Kauli ya Mkuu wa Mkoa Mh Makonda inakuwa kauli ya Serikali na kupewa nguvu na Wizara ya Afya nzuri zaidi na Waziri Mkuu anaibeba kama tamko la Serikali,kwa Jicho la tatu na la kipekee Makonda ana nafasi kubwa kwa Mkuu wa Nchi kuwazidi Mawaziri Mh Rais aangalie aina ya mfumo wa Uongozi wake na wasaidizi wake,kwa Mtindo huu Makonda anaweza kudumu kwa serikali hii kwa Muda Mrefu.

Kudumu kwa muda mrefu si tatizo, tatizo ni pale ambapo safu ya juu itapigia mstari kila tamko la huyu muheshimiwa kama standard ya matamko na maelekezo. Kuna mida fulani baadhi ya viongozi wakiongea unagundua kuwa ana hitilafu kubwa kwenye akili kama nanliu mwenye taaluma kwenye vichuguu
 
Huku wanatamani kodi za sigara huku wanapiga marufuku.. Ca'nt they be systematic?
 
afadhari wizara imemsahihisha huyu mkuu mkurupukaji...

ni marufuku kuvuta sigara ktk mikusanyiko ya umma.

na sio kama mkuu mkurupukaji alivyozuia uvutaji wa sigara hadharani...
 
Mambo mengine bwana, hivi ni katazo la mkuu wa mkoa kutovuta sigara hadharani au ni takwa la kisheria ???. Sheria hiyo ipo siku nyingi sema kwa kuwa tunakuwa mabingwa wa wa kutunga sheria nyingi na kuziacha bila usimamizi/utekelezaji mpaka zingine tunazisahau ndiyo maana tunaona hilo ni jambo jipya. Mambo mengi yana sheria tena nzuri tu, tatizo ni usimamiaji wake tu.

(Wanaoafiki waseme NDIO wasioafiki waseme SIO. Nadhani Walioafiki wameshida mswada umepitishwa kuwa sheria tunasubiri saini ya MH. RAIS)
 
kuna kitu nakiona shisha itapanda chati na itakuwa na thamani na kuwa kama madawa ya kulevya kwa sababu itakuwa ni kituadimu,ili kitu kiwe na thamani lazima kiwe adimu au kiwe haramu,cocain,kitimoto,bangi,tanzanite,gongo etc
Hapo sijakubali.
 
Back
Top Bottom