kluger
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 2,093
- 1,894
Salaam,
Huu ni msimo wa kilimo hapa nchini kwa wakulima wakubwa na wadogo.
Serikali kupitia viongozi wake wakuu imekuwa ikihamisha utumiaji wa mbolea na uanzishwaji wa viwanda vya kutengeneza mbolea.
Kwangu mimi hili nimeliona limekaa kisisa sana kuliko uhalisia.
Kwa nini?
1. Ukweli ni kwamba wakulima walio wengi hawamudu kununua Mbolea hiyo kwa kiasi kikubwa Yaani kuanzia 50 KGs
2. Ujazo huo ni zaidi ya mahitaji ya wakulima walio wengi ambao ni karibia asilimia 75 ambao wanamiliki mashamba madogo madogo tu
3. Nguvu kubwa ya vikosi vya Askari vinapita duka hadi duka kudhiniti upimaji wa mbolea ni ishara ya maagizo ya kisiasa
4. Kwa nini viongozi mnakuwa kama mnaishi dunia nyingine, ongeeni na wakulima kufahamu hali halisi. Wabunge na madiwani mpo kimya kama hamlifahamu na kupitisha kanuni zinazotesa wananchi wa hali ya chini
Mapendekezo nini kifanyike.
1. Kabla ya kupiga marufuku ni vyema kufanya tafiti halisi na kufahamu hali halisi
2. Serikali elekezeni viwanda kufunga mbolea katika ujazo kuanzia kilo 2, kilo 5, kilo 10, kilo 25 na kilo 50, ili kila mkulima anunue mbolea kadri ya uhitaji wake na si kulazimisha ununuzi wa kiasi kikubwa cha mbolea ambacho hawahitaji
Cha kushangaza kuna muuzaji mmoja wa mbolea alijitolea kuandikisha kila mkulima anayekuja na kiasi anachohitaji ili ikitimia idadi fulani ya kilo anawapatia mfuko wakulima hao wakagawane pia alipigwa marufuku.
Sasa serikali kwa nini mnatukomoa wakulima???
Ni hayo tu, wahusika kama hili litawafikia boresheni hali hiyo, mbolea hazinunuliki ni hasara tu, jifunzeni kwa wenzetu wakenya na wengine wanaofanya vizuri kwa kilimo cha kutumia MBOLEA.