Katavi: Aliyejenga madirisha katika kituo cha Afya cha Katumba ayavunja baada ya Halmashauri kutomlipa

Kajenga kwa gharama zake

Nyie Halmashauri mmekataa kumlipa kwa kuwa taratibu za Tender hazikufuatwa

Kaamua kwenda kuchukua vitu alivyojenga ili mtafute mtu wenu kwa taratibu ajenge,

Halmashauri zingine ni matapeli, wanakupa tender ukishakamilisha wanaanza kutafuta visingizio

Kama kabomoa alichojenga kwa kuwa taratibu za zabuni zilikiukwa kwanini tukasirike?

Tabia ya dhulma inazidi kuota mizizi nchini
Kwani kwenye mkataba alisema wasipomlipa atabomoa?
 
Utamlipaje mtu ambae wanasema alipewa tenda pasipo kufuatwa kwa taratibu?

Kwani yeye huyo mzabuni hiyo tenda aliipataje?Alipora hiyo tenda Kwa nguvu Kwa kutumia silaha??? Je huyo mzabuni hiyo tenda alijipa mwenyewe?? Je huyo mzabuni Ni mfanyakazi ktk hiyo Halmashauri ya Wilaya??


Watumishi WA Halmashauri ya Wilaya waliotoa hiyo tenda bila kufuata Sheria ndio walipaswa kuadhibiwa lakini siyo kumuadhibu mzabuni peke yake
 
Kwani yeye huyo mzabuni hiyo tenda aliipataje?Alipora hiyo tenda Kwa nguvu Kwa kutumia silaha??? Je huyo mzabuni hiyo tenda alijipa mwenyewe?? Je huyo mzabuni Ni mfanyakazi ktk hiyo Halmashauri ya Wilaya??


Watumishi WA Halmashauri ya Wilaya waliotoa hiyo tenda bila kufuata Sheria ndio walipaswa kuadhibiwa lakini siyo kumuadhibu mzabuni peke yake
Ndio maana naona yuko sahihi kung'oa madirisha yake,maana amefanya kazi yake baadae akaambiwa kulikosewa procedures za kumpa tenda.
 
Mkandarasi aliyefahamika kwa jina la Boniface Exavery, ambaye alitengeneza madirisha ya Almunium na katika Kituo cha Afya cha Katumba, Halmashauri ya Nsimbo ya mkoani Katavi, ameyavunja madirisha hayo, kwa kile alichokidai kutokamilishiwa malipo yake na ofisi ya Halmashauri huku akiwaameshamaliza kazi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera, amedai mradi huo ulikuwa umekiuka taratibu mbalimbali za kisheria, ikiwemo upatikanaji wa tenda hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, mwenyewe ameeleza kushtushwa na hatua ya Mkandarasi huyo, na kueleza taarifa za awali walizipata kutoka kwa wananchi, na kulitaka Jeshi la Polisi kumshikiria Mkandarasi huyo, huku akikiri Halmashauri kutomlipa malipo yake.

Mmoja wa Wakandarasi ambaye anajulikana kama Bulaya Mushi, ambaye na yeye anaidai Halmashauri hiyo kwenye mradi huo wa Kituo cha Afya, amemuomba Mkuu wa Mkoa kuangalia madai yao ili waweze kulipwa na Halmashauri hiyo.
WEZIIHAOO HIZO HELA WAMEKYLAA.NDIOMAANA LEO RAISI KATISHIA WATU.MTAMA ATAKAEKULA.HELA ZA HOSPTAL ATAZITAPIKA

UNAHISI MKUU WAMKOA HAJUU HAYA NDIO MAMBO.MH RAISI ANATAKIWA KUAMBIWA UKO ANAKOPITA ANATOA PESA WATU WANAKULAA

KAKUTA LINDI WATU WAMEJILIPA MIL 50 ATI WALISIMAMIA UJENZI NA HOSPTT HAIZIDI HATA MIL 200 AISEE

KAKUTA MHASIBU KAUZIWA GARI LAHOSPT LINATEMBEA KAPEWA MASAA APELEKE.MWENYEWE HILO GARI HOSOTLN..NA HOSPT HAINA GARI ATI..KHA
 
kuna jipu litatumbuliwa hapa iweje taratibu za tender hazijafuatwa na bado mtu ajenge mnamuona halafu hamumlipi?Hapo sasa ukisikia gharama za ujenzi unaweza shangaa.
 
hata mimi nilikuwa nashangaa kwanini ayavunje wakati anaweza kuyachomoa akasepa nayo
Waandishi wengine pumbafff sana. Jamaa aliyeweka hayo madirisha alipoambiwa hiyo tenda siyo yake akayachukua akaondoka nayo wala hakuvunja chochote na halmashauri waliona sawa maana ni wao walimwambia hawamtambui. Sasa akitoa madirisha yake ndo wanataka atambulike?
 
KUVUNJA ni neno lenye mshiko kwa lengo lako, bahati mbaya hakufanya hivyo aliyachomoa akaacha fremu, madirisha ya aluminiamu mtu yeyote anaweza akayachomoa kwani hupachikwa baada ya kufunga fremu. Tukio ulisemalo lilioneshwa kwenye luninga na hakuna kilichovunjwa japo siku hizi watanzania wengi hufurahia kuwaingiza matatizoni wenzao kwa kukuza mambo.
Akili za Wana CCM hizo za kufurahia wenzao kutolipwa
 
Back
Top Bottom