Katavi: Aliyejenga madirisha katika kituo cha Afya cha Katumba ayavunja baada ya Halmashauri kutomlipa

Ni vile kichwa cha habari "ayavunja madirisha"!! kilivyo
Hajavunja madirisha...jamaa alichofanya ni kuchomoa na kuchukua madirisha yake...walichomfanyia ni dhuluma ya waziwazi...mtu mumempa kazi amefanya kazi yake amemaliza vizuri alafu wanamzungusha hawataki kumlipa pesa zake...huo ni ubabe na dhuluma za waziwazi
 
Ndio tatizo la mswahili..huwa hatuna uvumilivu...utafkiri hayo malipo watamdhulumu.
Mtu alipwe kabla ya jua kuzama, tatizo la uswahili mnalo nyie mliotoa Tender.

Umetoa kazi mtu kakabidhisha kazi, mwenye kazi analeta janja janja ya kujifanya oh kazi ni sub-standard ili asimlipe hela yake kwa wakati. Wabongo kuheshimu mikataba bado sana, kama katiba tu mnavunja wangesenjota nyie.
 
N
Kajenga kwa gharama zake

Nyie Halmashauri mmekataa kumlipa kwa kuwa taratibu za Tender hazikufuatwa

Kaamua kwenda kuchukua vitu alivyojenga ili mtafute mtu wenu kwa taratibu ajenge,

Halmashauri zingine ni matapeli, wanakupa tender ukishakamilisha wanaanza kutafuta visingizio

Kama kabomoa alichojenga kwa kuwa taratibu za zabuni zilikiukwa kwanini tukasirike?

Tabia ya dhulma inazidi kuota mizizi nchini
Ndio uswahili wenyewe, mie ningeenda kuyanyofoa moja moja wabakiwe na nondo tu shenz taipu
 
Una uhakika alikuwa anadhulumiwa! Nahisi ni malipo kucheleweshwa tu mengine ni hasira za mkizi!
Kama alikuwa hadhulumiwi kwanini mlikuwa mnamcheleweshea malipo yake...huo mtaji wa kutengeneza madirisha unajua kaukuta wapi,kama kakopa bank na bank inataka chao unataka bank iuze nyumba yake kisa nyi halmashauri mnamcheleweshea haki yake??...mtu akimaliza kazi inatakiwa alipwe hela zake immediately na sio kuanza kumletea janjajanja yenye nia ovu ya udhulumaji ndani yake
 
Kama angeacha ingekuwa alama wazi ya udhalimu aliofanyiwa na kwa vile amevunja hapo ndipo uhujumu unapoanzia na ile mali haikuwa yake na hapo kosa linakuja kuharibu mali ya umma!! Hana uvumilivu

Angeacha ndo ingetoka hiyo, mimi niliwahi kukutana na mtu alijenga ofisi ya mtendaji wa mtaa flani lakini alidhulumiwa malipo yake,

Unasemaje mali haikua yake au ameharibu mali ya uma wakati hao viongozi wa uma hawajamlipa ingekua mali ya uma kama wangemlipa ila kama hajalipwa hiyo ni mali yake. Na njia sahihi sio kubembeleza malipo ni kuondoa kile alichokiweka maana ishakua ujinga kwanini tuzungushane kama watoto?
 
Angeacha ndo ingetoka hiyo, mimi niliwahi kukutana na mtu alijenga ofisi ya mtendaji wa mtaa flani lakini alidhulumiwa malipo yake,

Unasemaje mali haikua yake au ameharibu mali ya uma wakati hao viongozi wa uma hawajamlipa ingekua mali ya uma kama wangemlipa ila kama hajalipwa hiyo ni mali yake. Na njia sahihi sio kubembeleza malipo ni kuondoa kile alichokiweka maana ishakua ujinga kwanini tuzungushane kama watoto?
Na zile gharama alizotumia! ndio zitarudi ? hata hivyo jamaa inasemekana hakuvunja kayatoa na yatamfaa baadae. So hapo ngoma droo hadi hapo atakapozushiwa janga lingine!
 
Mkandarasi aliyefahamika kwa jina la Boniface Exavery, ambaye alitengeneza madirisha ya Almunium na katika Kituo cha Afya cha Katumba, Halmashauri ya Nsimbo ya mkoani Katavi, ameyavunja madirisha hayo, kwa kile alichokidai kutokamilishiwa malipo yake na ofisi ya Halmashauri huku akiwaameshamaliza kazi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera, amedai mradi huo ulikuwa umekiuka taratibu mbalimbali za kisheria, ikiwemo upatikanaji wa tenda hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, mwenyewe ameeleza kushtushwa na hatua ya Mkandarasi huyo, na kueleza taarifa za awali walizipata kutoka kwa wananchi, na kulitaka Jeshi la Polisi kumshikiria Mkandarasi huyo, huku akikiri Halmashauri kutomlipa malipo yake.

Mmoja wa Wakandarasi ambaye anajulikana kama Bulaya Mushi, ambaye na yeye anaidai Halmashauri hiyo kwenye mradi huo wa Kituo cha Afya, amemuomba Mkuu wa Mkoa kuangalia madai yao ili waweze kulipwa na Halmashauri hiyo.
Mfano wa kuigwa ndio dawa yao 🤟 🤟 🤟
 
KUVUNJA ni neno lenye mshiko kwa lengo lako, bahati mbaya hakufanya hivyo aliyachomoa akaacha fremu, madirisha ya aluminiamu mtu yeyote anaweza akayachomoa kwani hupachikwa baada ya kufunga fremu. Tukio ulisemalo lilioneshwa kwenye luninga na hakuna kilichovunjwa japo siku hizi watanzania wengi hufurahia kuwaingiza matatizoni wenzao kwa kukuza mambo.
Hapo ulipo agiza bia naja kulipa
 
Kama angeacha ingekuwa alama wazi ya udhalimu aliofanyiwa na kwa vile amevunja hapo ndipo uhujumu unapoanzia na ile mali haikuwa yake na hapo kosa linakuja kuharibu mali ya umma!! Hana uvumilivu
Hakuna kitu kama hicho.

Mimi si Mwanasheria Ila angalau nafahamu iwapo anao Ushahidi wa kuwadai na Mahakama ikatenda Haki kama inavyotakiwa/kupaswa jamaa hana Hatia.

Wakati Mwingine Unyonge sana haifai.
 
Labda upo upande wa Serikali bila kuangalia upande wa wazabuni namna wanavyoteseka bila kulipwa stahiki zao, na miradi washamaliza.



Sasa kamanda, kuvunja hayo madirisha ndio solution kweli!! Si anaharibu cv yake na kupelekea kutoaminiwa na wateja wengine...alitakiwa apambane mpaka mwisho muhimu asidhulumike!
 
Back
Top Bottom