Katavi: Aliyejenga madirisha katika kituo cha Afya cha Katumba ayavunja baada ya Halmashauri kutomlipa

Tatizo serikali hailipi wakandarasi, halafu mtu anasimama jukwaani TUMESHAJENGA ZAHANATI AU KITUO CHA AFYA KADHAA serikali ya JPM inawajali sana, na bla bla kibao, huku kuna mdai anakufa kwa presha madeni
 
Tukio ulisemalo lilioneshwa kwenye luninga na hakuna kilichovunjwa japo siku hizi watanzania wengi hufurahia kuwaingiza matatizoni wenzao kwa kukuza mambo.


Mkuu msamehe bure mleta mada ameandika kichonganishi nadhani kwasababu kuna ziara inaendelea huko yalikojiri yasemwayo.
 
KUVUNJA ni neno lenye mshiko kwa lengo lako, bahati mbaya hakufanya hivyo aliyachomoa akaacha fremu, madirisha ya aluminiamu mtu yeyote anaweza akayachomoa kwani hupachikwa baada ya kufunga fremu. Tukio ulisemalo lilioneshwa kwenye luninga na hakuna kilichovunjwa japo siku hizi watanzania wengi hufurahia kuwaingiza matatizoni wenzao kwa kukuza mambo.
watanzania wengi ni wanafiki sana
 
Naliomba jeshi la polisi limshikilie Mkurugenzi wa Halmashauri kwa nini halipi madeni, ama hata kupatana na wakandarasi nn kinafuata. Mm kudai changu hamnipi, eti kamateni, lipa changu nisepe, ama nang'oa mtu meno kama cyo madirisha.
Umeongea point ya maana sana mkuu. Serikali kuu, idara zake na hata serikali za mitaa kama huko Halmashauri ndio chanzo kikubwa cha matatizo ya wakandarasi hasa wazawa maana hua hawalipwi kwa wakati

Halmashauri zilishauriwa kutumia mafundi wa kawaida (local fundi) kwenye kazi ndogo kama ujenzi wa vyumba vya madarasa au ukarabati wa kawaida wa shule, zahanati na miradi mingine ya kawaida. Wengi wa hawa ni watu wenye mitaji midogo na usipowalipa kwa wakati unauwa mitaji na uwezo wao wa kufanya kazi zingine na kukua

Ajabu ni kwamba kuna usumbufu mwingi sana kuhusiana na malipo hata baada ya kupeleka certificate ya kukamilisha hatua fulani ya ujenzi

Huu ni uonevu na hata hiyo sheria ya manunuzi ni katika sheria mbaya ambayo kwanza siyo kweli eti inasaidia kuziba mianya ya rushwa. Mimi na support kabisa alichofanya huyo mkandarasi na kiuhalisia kitendo chochote cha kumpa adhabu kwa alichokifanya ni unyanyasaji
 
kazi nyingi za manispaa/halmashauri hata kama ulipitia taratibu zote, ulipwaji huwa tatizo sana......RUSHWA haiwezi kuisha Tanzania...kama kweli hakufuata taratibu, mpaka mradi unakamilika ndio mnalisema......!!!!, nna hakika hajayavunya kama mtoa taarifa alivyodai....sbb atakuwa amejitia hasara mara mbili.....nna hakika kayang'oa, ni mali yake..ila kwa mwendo kasi na mihemko ya watawala wetu, huyo fundi atasumbuliwa sana.....mali yake itamsumbua mno....
 
Kama angeacha ingekuwa alama wazi ya udhalimu aliofanyiwa na kwa vile amevunja hapo ndipo uhujumu unapoanzia na ile mali haikuwa yake na hapo kosa linakuja kuharibu mali ya umma!! Hana uvumilivu
Ameharibu mali ipi ya umma,tulioona kwenye tv hakuna mali ya umma iliyoharibika...jamaa kachomoa madirisha yake ya aluminium tena vizuri tu pasipo uharibifu..
 
Waache kupenda vya bure,,sasa kama kandarasi haitambuliki,ana kosa gani kuyachomoa madirisha yake?,,tatizo safari hii watu wanaona kukomoana ni sifa sana,huyo mkurugenzi ndo awajibike,ni mzembe na dhulmati mkubwa
 
Ukute kampuni yake ni moja ya zile zilizofutwa na Board sasa kawaza itakuwaje na bado sijalipwa akaona ajiongeze bora kuondoka na madirisha.
 
Ameharibu mali ipi ya umma,tulioona kwenye tv hakuna mali ya umma iliyoharibika...jamaa kachomoa madirisha yake ya aluminium tena vizuri tu pasipo uharibifu..
Ni vile kichwa cha habari "ayavunja madirisha"!! kilivyo
 
Back
Top Bottom