Katavi: Afariki dunia baada ya kunywa maji ya baraka Msikitini

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linamsaka Hamim Mussa na wenzake wawili wakituhumiwa kuwanywesha wananchi maji yanayodaiwa kuwa ya Baraka katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa uliopo Mpanda Mjini na kusababisha kifo cha mtu mmoja na mwingine kulazwa.

Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo Mkoani Katavi Benedict Mapugila ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Mpanda Radio kuhusu tukio hilo ambapo mtuhumiwa amesemekana kuwa ametoroka mara baada ya kutokea kwa madhara hayo.

Mmoja wa manusra wa katika tukio hilo Kulusum Shabani pamoja na mambo mengine amesema tukio hilo limetokea Jumamosi ya Oktba 6 mwaka huu baada kunywa maji hayo kwa maelekezo ya Hamim Mussa anayetajwa kuwa ni Mganga kutoka Mkoani Mwanza.

Hata hivyo Uongozi wa Hospitali ya wilaya ya Mpanda umesema haujapata taarifa za tukio hilo kwa kuwa waathiriwa wa tukio hilo walikuwa wamelazwa katika Zahanati ya Afya iliyopo Mpanda Mjini.

Kwa mjibu wa Shehe wa Mkoa wa Katavi Mwalimu Ally Hussein amesema wamelipokea tukio hilo kwa maskitiko na kulikuwa kuna watu 3 kati yao wanawake wawili waliokuwa wakishughulikia matibabu hayo ambao ndio wanaosakwa na jeshi la polisi baada ya kutokomea kusikojulikana.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt.Omary Sukari amesema atatoa taarifa kamili mara baada ya kupata ripoti ya tukio hilo.
 
Muda wake wa kuishi duniani ulikwisha huyo ndugu wasitafute namna, cha msingi huyo anaeshikiliwa na polisi basi wafanye uchunguzi wa kitaalamu wa hayo maji kama yana kemikali, au sumu za kuweza kudhuru na kuua binadamu vinginevyo ushahidi wa kumpata na hatia huyo anaeshikiliwa ni mdogo sana,
 
acha uongo wewe msikitini hakuna maji ya baraka na wala hakuna msikitini mkuu wa ijumaa.. na wala hakuna utaratibu wa kunyweshana maji msikitini jaribu kumuuliza vizuri huyo aliyekupa habari hizi usikurupuke.
Kwani mkuu wewe ulikuwepo? Acha kubishabisha vitu usivyovijua
 
acha uongo wewe msikitini hakuna maji ya baraka na wala hakuna msikitini mkuu wa ijumaa.. na wala hakuna utaratibu wa kunyweshana maji msikitini jaribu kumuuliza vizuri huyo aliyekupa habari hizi usikurupuke.
Kwa hiyo unabishia habari?Holy Moly!😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom