Katambi: Lissu ni mwehu namjua vizuri atauza nchi asubuhi kweupe, kama anabisha ajitokeze hadharani

TUMI EPAFRA

Member
Jul 12, 2020
59
56
Angalia video hii ujifunze kuhusu matatizo ya Tanzania na mtatuzi wake, jinsi wapinzani wanavyotupotosha. Angalia kabla ya kukurupuka kujibu pumba.

------

Katambi amedai Lissu sio mtu sahihi sana kwani anamfahamu vyema. Katambi anasema Lissu ni mpotoshaji kwamba matatizo ya Tanzania yanasababishwa na Magufuli au CCM. Katambi amesema matatizo hayo ni ya kihistoria yamesababishwa na ukoloni wa zamani ulioondolewa na ukoloni mamboleo.

Amesema matatizo yaliyopo ni 'shared' ambayo ya ni ujinga, maradhi, umasikina na sasa ufisadi. Amesema shared enemy tuliyenae leo ni ukoloni mamboleo ambao wanakuja kupora rasilimali.

Amesema Lissu anayeungana na Zitto Kabwe leo ndio aliyesoma mashtaka ya Zitto kumuondoa CHADEMA wakisema ni msaliti, kinyonga na mnafiki. Wanasema aliondolewa kwa sababu alitaka kufanya mapinduzi ndani ya CHADEMA kwa maslahi yake binafsi.

Moja ya mashtaka amedai alipewa fedha akauza majimbo kanda ya ziwa mkoa wa Mara na alipewa gari pamoja na milioni 40 na Mkono.

Amesema wamtafute mtu kama yeye wafanye nae debate, wasimtafute mtu mkuubwa kama Magufuli kwani hawana hio audacity wala moral authority bali ni saizi yao.

Anasema Zitto alietuhumiwa CHADEMA kwa mambo mengi ya hovyo mpaka Lema kusema bora kumuamini shetani kuliko Zitto Kabwe na amedai ACT ni zao la Membe kwani limetengenezwa na timu ya Membe ili kuweza ku-counter CHADEMA wakati huo..
 
Humo Chadema kuna pande mbili,Katambi aliyoyasema sio kwa bahati mbaya,mbona anazungumza siri za chama bila hata kulazimika kufanya hivyo?

Lowassa na Sumaye mbona hawakutoa siri za CCM walipokuwa Chadema.
Hawa walanguzi wa siasa wafanzie social distancing.
 
Anatafuta uteuzi tena baada ya kuachia ofisi ulivokuwa umepewa dhamana kuiongoza, tafuta taratibu usirukie mada huyo Lisu sasa ni mgombea urais wakujibizana nae ni yule anayegombea urais sasa na wewe unagombea urais wawapi hadi unataka ajitokeze kwako
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom