Kata ticket ya bus kwenda mkoani kwenye simu yako

Kata ticket ya bus kwenda mkoani kwenye simu yako

ndio maana mteja anayekata ticket kwa app hii hachagui siti ili kuepusha siti moja kuwa booked mara 2 kwa kuwa ofisi nyingi wanafanya booking manual
Hapo ndo ulipoharibu,, et kwamba nisichague siti?

[emoji3]
 
Sasa hizo ni web zao official. Wewe nenda kakate tiketi ya princess muro, champion na raha Leo kwenye app alafu ukifanikiwa kusafiri nakurudishia nauli Mara 5 yake
Duh Inaonekana hzo Kampuni hazna huduma nzuri kwa wateja wake
 
Hapa JF, kuuza bidhaa inabifi uje na marketing strategy ya hali ya juu!!! Tena bidhaa yenyewe ihusishe mambo ya mitandao hapo ndiyo kabisa lazima jasho likutoke.
 
Hapa JF, kuuza bidhaa inabifi uje na marketing strategy ya hali ya juu!!! Tena bidhaa yenyewe ihusishe mambo ya mitandao hapo ndiyo kabisa lazima jasho likutoke.
lakini najua taratibu wataelewa, Mungu akijaalia ndani ya huu mwezi wa 11, nitaweka matangazo kwenye baadhi ya youtube channels za watu maarufu ili watu waamini
 
Daaaah hayo mabasi uliyotaja hata ukienda kukata tickets ofisini kwao kabisa asubuhi wakati wa kusafiri lazima ukutane na magumashi ya mgongano wa siti.

Bongo customer service bado mbobu sana watoa huduma ujanja ujanja mwingi sana.
Bongo bado tupo unproffessional sana, kwa pande zote yaani watoa huduma na abiria. kila ninapoenda kupanda basi nagundua kuwa karibia asilimia 90 ya abiria wanakata tiketi papo hapo muda wa safari, sijui wanawezaje hili maana mimi kutoka nyumbani huku sijui naenda kusafiri vipi huwa haiingii akilini kabisa.

Kuhusu unproffessionalism kwa watoa huduma, ni majuzi tu nimekata tiketi Dar express pale Shekilango siku moja kabla ya safari, nikiamini mabasi wanayolipisha 33000 ni yale luxury, na huwa hivyo siku zote lakini cha ajabu asubuhi walinipandisha kwenye yale mabasi yaliyochoka.

Saa kumi na mbili alfajiri Dada aliyenikatia tiketi jana yake hayupo, ni Wapiga debe tu wanapishana pishana kukimbilia abiria..hakuna wala wa kukusikiliza...mimi huwa ni kati ya wale Watu wachache ambao huumizwa sana na mambo kama hayo. Nilipiga kelele pale wakawa wananiangalia tu kama katuni..nadhani kulikuwa na abiria kadhaa pia waliokuwa wana tiketi za 33000 kama mimi walipandishwa basi lile.

Niliumia sana nikakimbilia Dar lux pale jirani wakaniambia nafasi kwenda Arusha zimeshajaa, nilikuwa tayari kupoteza hiyo 33000.

Siwezi kuamini kampuni kubwa na ninayoiamini inaweza kumfanyia abiria uhuni wa namna ile...na hii ni mara ya pili imenitokea kwa kampuni hii na zote ilikuwa ni kutoka Dar kwenda Arusha.

Ndio maana naona kukata tiketi online ni kama kununua kesi tu, Kampuni nyingi ni za kihunihuni...labda kwa kuwa Wabongo wengi tu mazoba hata kila tukifanyiwa uhuni kulalamika hatuwezi.
 
Safi sana hii itasaidie wale madalali wa stendi wanakeraga sana
 
Safi sana hii itasaidie wale madalali wa stendi wanakeraga sana
hiyo ilikuwa source ya idea hii, kuna siku nilienda kukata ticket ya ndungu yangu mmoja hakika waliniudhi sana ndipo nikapata hili wazo
 
Niliumia sana nikakimbilia Dar lux pale jirani wakaniambia nafasi kwenda Arusha zimeshajaa, nilikuwa tayari kupoteza hiyo 33000.
Na mimi kuna kampuni moja ya mabasi nimeiwekea vikwazo, sipandi mabasi yake ...hata nikienda kituoni nikayakuta mabasi ya kampuni hiyo yenyewe tu, kama hakuna mbadala naharisha safari.
 
taratibu utaondoa hofu
Njia rahisi kwanza ya kuaminika, verify JF ID yako kwanza. Nina hakika utapata zaidi asilimia 60 ya kuaminika. Ukishaaminika itakuwa rahisi 'kupanga unachotaka' kwa wateja!
 
sawa boss, nimekupata nitafanya hivyo
Njia rahisi kwanza ya kuaminika, verify JF ID yako kwanza. Nina hakika utapata zaidi asilimia 60 ya kuaminika. Ukishaaminika itakuwa rahisi 'kupanga unachotaka' kwa wateja!
 
Bongo bado tupo unproffessional sana, kwa pande zote yaani watoa huduma na abiria. kila ninapoenda kupanda basi nagundua kuwa karibia asilimia 90 ya abiria wanakata tiketi papo hapo muda wa safari, sijui wanawezaje hili maana mimi kutoka nyumbani huku sijui naenda kusafiri vipi huwa haiingii akilini kabisa.

Kuhusu unproffessionalism kwa watoa huduma, ni majuzi tu nimekata tiketi Dar express pale Shekilango siku moja kabla ya safari, nikiamini mabasi wanayolipisha 33000 ni yale luxury, na huwa hivyo siku zote lakini cha ajabu asubuhi walinipandisha kwenye yale mabasi yaliyochoka.

Saa kumi na mbili alfajiri Dada aliyenikatia tiketi jana hayupo, ni Wapiga debe tu wanapishana pishana kukimbilia abiria..hakuna wala wa kukusikiliza...mimi huwa ni kati ya wale Watu wachache ambao huumizwa sana na mambo kama hayo. Nilipiga kelele pale wakawa wananiangalia tu kama katuni..nadhani kulikuwa na abiria kadhaa pia waliokuwa wana tiketi za 33000 kama mimi walipandishwa basi lile.

Niliumia sana nikakimbilia Dar lux pale jirani wakaniambia nafasi kwenda Arusha zimeshajaa, nilikuwa tayari kupoteza hiyo 33000.

Siwezi kuamini kampuni kubwa na ninayoiamini inaweza kumfanyia abiria uhuni wa namna ile...na hii ni mara ya pili imenitokea kwa kampuni hii na zote ilikuwa ni kutoka Dar kwenda Arusha.

Ndio maana naona kukata tiketi online naona ni kama kununua kesi tu, Kampuni nyingi ni za kihunihuni...labda kwa kuwa Wabongo wengi tu mazoba hata kila tukifanyiwa uhuni kulalamika hatuwezi.
Tatizo hilo sijui litaisha lini?

Haliwezi isha,, ila cha mhimu ni kukata tiket ktk Mabas ambayo ni konki ya kibabe,,
 
Tatizo hilo sijui litaisha lini?

Haliwezi isha,, ila cha mhimu ni kukata tiket ktk Mabas ambayo ni konki ya kibabe,,
Dar Express mbona ni kampuni 'konki' ni kati ya kampuni kongwe sana kwa njia ya Dar Arusha.

Tatizo nadhani ni usimamizi mbovu tu, Mwenye kampuni angetafuta msimamizi serious.

Anajitahidi kununua Mabasi mazuri na ya gharama ila watendaji ni hovyo kabisa, wakati Kampuni nyingi wanatumia YUNTONG a.k.a Mchina, jamaa yeye ameweka SCANIA....angeweka hata meneja Mkenya labda ingesaidia.
 
Back
Top Bottom