Je, umefuta ujumbe kwenye simu yako kwa bahati mbaya? Fanya hivi kurejesha

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,546
Umefuta Message kwa bahati mbaya ??

Kuna wakati unajikuta katika kupunguza punguza vitu basi kwa bahati mbaya ukafuta (sms) au taarifa zako muhimu. Je unatakiwa upate stress๐Ÿค”? Hapana!

Kuna mbinu kadhaa unaweza kuzitumia ili kurejesha sms zilizopotea kwenye simu yako. Katika andiko hili tutaangazia njia mbili rahisi.

1. Kutumia Google Drive
2. Kutumia App

1. Kutumia Google Drive
Njia ya kwanza kwa kutumia ๐—š๐—ผ๐—ผ๐—ด๐—น๐—ฒ ๐—ฑ๐—ฟ๐—ถ๐˜ƒ๐—ฒ, kupitia google drive unaweza rudisha ujumbe ulizofuta kwa bahati mbaya kwenye simu yako. Sio ujumbe tu mpaka picha , audio , contacts nk.

Ingia kwenye setting ya simu yako Kisha chagua About system halafu ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฐ๐—ธ๐˜‚๐—ฝ๐˜€ & ๐—ฟ๐—ฒ๐˜€๐˜๐—ผ๐—ฟ๐—ฒ.
โ€ข ukingia kwenye backups hapo unafanya kazi ya kuhifadhi vitu vyako kwenye email yako contact, picha, calendar, audio.
โ€ข Kama hujafanya backups na unaogopa data zako utapoteza basi bonyeza backups
โ€ข Katika mbinu hii pia unaweza fanya backup za Apps zako.

1655702774209.png

โœ“ Ukingia kwenye restore sasa unafanya kazi ya kurudisha vitu vyako ikiwa umefuta kwa bahati mbaya basi utavipata bila shida yoyote.

2. K๐˜‚๐˜๐˜‚๐—บ๐—ถ๐—ฎ A๐—ฝ๐—ฝ๐˜€
Kupitia app itakusaidia kurudisha vitu vyako ikiwa umefuta kwa bahati mbaya kama vile message & mms pamoja na call logs.

1655702855972.png

๐—ฆ๐—บ๐˜€ ๐—ฏ๐—ฎ๐—ฐ๐—ธ๐˜‚๐—ฝ & ๐—ฟ๐—ฒ๐˜€๐˜๐—ผ๐—ฟ๐—ฒ ๐—ป๐—ถ ๐—ฎ๐—ฝ๐—ฝ ambayo itakusaidia kufanya backups pamoja restore call zako Ikiwa
โ€ข umefuta kwa bahati mbaya
โ€ข ikiwa unahitaji kuhamisha sms zako kwenye simu mpya bila kutumia na mtu
โ€ข ikiwa unataka kuhamisha call logs zako kwenye simu mpya au nk

Hii App inakupa nafasi ya kuhifadhi vitu vyako kwenye Google drive , Dropbox pamoja na One drive vitakaa muda mrefu bila kupotea โœŠ.

ZINGATIA: Ili Kufanikisha njizi Hizi yakupasa kuwa na SD-CARD(memory) katika simu yako ili kuweza kutumia njia ya Backup & Restore.

Memory Itakusaidia kuhifadhi vitu ulivyobackup kwa urahisi hata ikatokea ume flash simu yako baati mbaya basi kama ulitumia memory kuhifadhi data basi ni rahisi kuzirudisha.

Pia washauriwa kutumia Google Massages ili kupata uwezo wa ku backup massage zako kila baada ya muda kadhaa mfano 24Hrs, 2Day, 1Week.

Kumbuka Data zitakazorudi ni zile ambazo uli backup kabla ya kupoteza chochote, lakini haiwezi rudisha sms zilizotumwa baada ya backup process kufanyika

Credit: Bongo Tech
 
Simu zinakula bando sio ubwabwa
Nenda maeneo ya free wifi ukale bando la kodi yako.
Ilitakiwa maneno ya umma yote mfano stand ya mabus na daladala,masokoni, vivuko vya pantoni, nk kote kufungwe free wifi sababu Hakuna Mtanzania anaingia bure maeneo hayo yote tunalipa na ushuru wanakusanya.
 
Back
Top Bottom