Doctor Mama Amon
Platinum Member
- Mar 30, 2018
- 2,311
- 3,490
Zaidi ya 50% ya wajumbe wa kikundi kinachojiita G-55 ni wachaga wa Arusha na Moshi, na walikuwa TImu Mbowe kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa Mwenyekti Lissu wa Januari mwaka huu.
Tangu kuasisiwa kwake hadi mwaka jana, kati ya vikwazo vikubwa vya kisiasa dhidi ya Chadema, kikwazo namba moja kilikuwa ni harufu ya shobo la "umangi wa kichaga".
Yaani imani ya viongozi wakuu wa Chadema kwamba Chadema ni mali ya "kabila bora" la Wachaga, na makabila mengine ni wasindikizaji tu.
Pia soma > Rasmi G-55 wajiondoa CHADEMA
Mtazamo huu ulitoa fursa kwa watu wa usalama kuipiga mkasi Chadema, maana "umangi wa kichaga" ni tishio halisi dhidi ya umoja wa Taifa lenye makabila 120 plus.
Mfano, hayati Samuel Sitta aliwahi kutamka wazi kwamba, kwa hali ilivyo ndani ya Chadema ya miaka ile, hata kama Chadema wangekishinda urais wasingeweza "kupewa" nchi.
Kauli hii ilikuwa inaungwa mkono na Kamisaa wa Dawati la Siasa, Peter Nyamanchi Tyienyi.
Sitta na Tyienyi ni marehemu.
Lakini sasa, uchaguzi wa Lissu kuwa Mwenyekiti umefuta umangi huu.
Sitta na Tyienyi wangefufuka leo watajiunga na Chadema hakika.
Na sasa kuondoka Chadema kwa hawa G-55 kunahitimisha mchakato wa kukisafisha Chadema.
Busara ya "Mafahari wawili hawakai zizi moja" imetimia, na Chadema ya Watanzania wote sasa inachipuka kwa nguvu zaidi.
Nawatakia safari njema hawa G-55, tukutane jukwaani.
No Reform, No Election.
Umangi Never, Utaifa Forever.