Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,805
- 43,230
Nilipokuwa binti mdogo nilikuwa mdadisi sana, nakumbuka nilikuwa nikimuuliza mama Kasie kila mara nikiwa mkubwa ntakuwa nani? Yaani maisha yangu yatakuwaje?
Mama Kasie alinijibu mwanangu Kasie maisha ni kuyapa muda na wakati.... vyovyote utavyokuwa muda haugandi masaa yataenda siku zitapita na hakika utakuwa mkubwa na kuona kuwa utakuwa nani.
Kasie Kigoriii
Muda ukapita nikawa kigori hapo nikapata mpenzi aliye nitoa utando wa mahaba, siku moja kati ya siku zetu tulizo kuwa kwenye mahaba nikimuuliza. ... mpenzi maisha yetu yatakuwaje... tutazeeka pamoja? Tutastaafu pamoja? Tutakuwa na mafanikio gani au penzi letu litazorota? Mpenz akanijibu.....
Kasie Mahaba
Kasie mpenz, vyovyote itavokuwa maisha ni kuyapa wakati, muda na kuvuta subira. Muda haugandi na wakati ukuta.... wakati ukifika utaona tuu jinsi itavokuwa.
Nyakati zote mbili hizo nilikuwa na shauku ya kutaka kujua nini kitatokea mbele.... leo hii naandika hapa nina kurasa na kurasa za Kasie kwa yaliyomtukia.
Basi kwa robo tatu hii iliyobakia kutokana na makadirio ya (analysts) Kasie's future will be........
Kasie Motoo Matata 2018.