Kasi ya utendaji wa Rais wa awamu ya tano inawabeba watendaji wake wengi mno na ni hatari sana wakibweteka

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,542
3,451
Miongoni mwa mambo ninayoyaona kama hatari sana katika maisha ya watu ni " kubebwa na mfumo" badala ya kuandaa nao.

Watendaji wa Rais walio wengi wanaonekana kubebwa na mfumo na kwa maana hiyo utendaji wao hauakisi jona kwa moja kasi ya Mheshimiwa Rais.

Wananchi wengi wamejenga imani kubwa sana juu ya kasi ya utendaji wa Rais kuliko viongozi wao wanapokuwa nao mara kwa mara.

Jambo hili linaipa sifa nzuri CCM ila linaweza likawawekea mfumo ngumu na hatari sana wale wote wanaobebwa na mfumo kwenye uchaguzi ujao.

Ni vyema kiongozi kuwajibika kwa kuendana na mfumo na siyo kubebwa na mfumo kwa sababu kitakachokuwajibisha na kukuwekea mazingira mazuri ni jitihada zako za kuendana na mfumo na siyo kule kubebwa na mfumo.
 
Naomba niulize swali Rais Magufuli toka aingie madarakani amefanya nini kwa mwananchi wa kijijini?
.
Vijijini ndo ccm inakovuna kura na ndipo kuliko na idadi kubwa ya watu
 
Naomba niulize swali Rais Magufuli toka aingie madarakani amefanya nini kwa mwananchi wa kijijini?
.
Vijijini ndo ccm inakovuna kura na ndipo kuliko na idadi kubwa ya watu
Ameboresha huduma za Afya,miundombinu,ametatua kero za wachimbaji wadigowadogo wa madini,amepunguza urasimu katika ofisi za Serikali,ameongeza nguvu ya sauti za watu wa chini(nenda vijijini ukienda kwenye vituo vya afya utakuta namba ya Mganga mkuu imewekwa wazi na kama kuna kero Mwananchi anaweza kupiga simu na kuonesha dukuduku lake)....ni mengi mno Kaka .
 
Unyankhanya Singida,Moshi Vijijini Kilimanjaro,Bitale Kigoma, Boko Dar es Salaam,Songambele Dodoma...bado havitoshi kwa mfano Mkuu?
Hapa kuna mchango mkubwa wa walipa kodi na viongozi wa wananchi (siyo hawa wa juzi waliopita bila kupingwa) kwa hyo wewe kusema kwamba walimezwa na mfumo ni kweli kutokana na mfumo wenyewe ambao hata wewe ukiwekeza kijijini kwenu lazima sifa apewe Mh.
Ila hao viongozi walipiga kazi sana na wanakubalika na wananchi wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kasi ya utendaji wake katika sekta zote anazozisimamia

Magufuli ana kasi au tunalazimishwa kuamini kuwa ana kasi? Wananchi wengi wana imani na kasi ya rais, je ni kipi kinafanya wasijitokeze kupiga kura?
 
Ameboresha huduma za Afya,
Ameboresha huduma za afya vijiji gani au unafikiri hospital ni majengo?
Nitakuwa tayari kutoa ushahidi wa jinsi vituo vya afya na zahanati zilivyo tupu hazina vifaa wala dawa ushahidi huu utatoka kwenye vijiji sita.
Watu hadi wanasema ni bora wangejenga mabwawa tukaogelee
.
miundombinu,
Miundo mbinu kajenga vijiji gani?
Kumbuka swali langu halikulenga mijini

ametatua kero za wachimbaji wadigowadogo wa madini,
Hapa ndio kwenyewe sasa mimi nalala juu ya ardhi yenye madini.
Ametatua migogoro gani maana hadi leo hii ukifata magwangala umeumia ambush wakikushika huna miguu.
Pengine unieleweshe katatua dhidi ya nani?

amepunguza urasimu katika ofisi za Serikali,
Ungezitaja baadhi ya hizo ofisi ingekuwa jambo jema sana.
Maana vijijini tuna ofisi si zaidi ya tano za serikali
Kuna polisi, mahakama, ofisi ya kijiji, hospital na pengine magereza.

ameongeza nguvu ya sauti za watu wa chini(nenda vijijini ukienda kwenye vituo vya afya utakuta namba ya Mganga mkuu imewekwa wazi na kama kuna kero Mwananchi anaweza kupiga simu na kuonesha dukuduku lake)....ni mengi mno Kaka .
Wewe wewe wewee nahmala kijijini mganga ni Mungu huwezi msema vibaya jaribu uone upate shida hata panadol hupati unakufa kwenye stuli
 
Back
Top Bottom