kisugujira
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 774
- 200
Matatizo ya usajili wa namba za simu hayapo VODACOM peke yao! Ninayo namba ya TIGO ambayo niliinunua toka kwa wauzaji wa TIGO waliokuwa wakifanya mauzo na matangazo kwa gari (Hiace) nilipokuwa Ikwiriri kikazi. Niliwapa nakala ya kitambulisho na kujaza fomu. Lakini baadaye nikaja gundua jina lililotumika kunisajili siyo langu baada ya kwenda kutoa pesa nilizotumiwa kupitia hiyo namba!