Kashfa nzito ndani ya Benki ya NMB

Kashfa nzito ndani ya Benki ya NMB

- Mimi ni mkazi wa Tabata na mwajiriwa wa Benki ya NMB. Kwa maslahi mapana ya taifa na ya Benki hii, nadiriki kuyaweka maisha yangu na ajira yangu hatarini kwani nikijulikana either ntatoweka au ntafukuzwa kazi. Niko tayari kwa yote mawili, Ila siwezi kunyamaza kwenya kashfa la ajabu, aibu na la kijinga linalotia kinyaa kama hili linalotendeka ndani ya hii benki. Kwa lugha nyingine huu ni uozo, ambao nadhani serikali au Takukuru walichunguze. Hii benki haitaki kitu chochote kizuri kisichokuwa na maslahi binafsi kwa wakubwa. Nimeamua kuwa mpiga mbiu au kafara ikibidi.

- Kuna kampuni ya wajerumani walioleta teknolojia (suluhisho la uhakika) ambayo imeonekana kuwa ni ya hali ya juu kwenye maswala ya nishati. Wakazi wa Tabata tumeliona hili pale Kimanga kwa miaka miwili sasa. Ila hii teknolojia imepigwa vita kali sana ndani ya benki, na hatimaye hao wajerumani wakafukuzwa. Nimeambiwa walifukwa vibaya sana, wakiambiwa hawana vigezo kwa sababu walikubaliwa kufunga mitambo yao na afisa wa ngazi ya chini, huku hawa hawa viongozi wakiendelea kuchukua vitu vya hovyo kariakoo kuja kufunga kwenye hii saiti. Zaidi waliambiwa hawawezi kufanya lolote, wakitaka waende mahakamani

- Siku ya ijumaa 18/11/2016 niliondoka kazini mapema kidogo, mida ya saa 7 baada ya dada wa kazi kunitaarifu kwamba , mwanangu wa pili alirudishwa kutoka shule mapema baada ya kuonyesha dalili za kuwa na malaria. Pale Tabata Kimanga nina kabiashara kadogo, kwa hiyo nikaamua kupapitia kuangalia maendelo kabla ya kwenda nyumbani. Biashara yangu haipo mbali na jengo la ATM la NMB. Baada ya kuwasili, niliona umati mkubwa mbele ya jengo hilo, kidogo nilishtuka na kutaka kujua kulikoni. Wengi wa waliokusanyika pale, walionyesha kukerwa sana kwa sababu wajerumani walikuwa wanang’oa mitambo yao za kufua umeme walizofunga kwenye hizi ATM tatu za hapa Kimanga.

- Kwa wakazi wa Segerea, Kigogo, Buguruni, Ubungo, Tabata na viunga vyake vyote, wanalijua hili ATM kwa sababu ni sehemu pekee hapa DAR pakukimbilia umeme unapokatika kwa kipindi kirefu na huduma za ATM zikawa hazipatikani. Nina maana kwamba umeme unapatikana hapa masaa 24 na hakuna foleni. Waendesha bodaboda, wafanyabiashara wadodgo wadogo, na walinzi katika eneo hili walilitegemea sana hii mitambo ya wajerumani iliyokuwa inafua umeme na kutoa mwanga mkubwa pale umeme unapokatika hasa usiku. Kwa kifupi, hii sehemu haikuwa tu ni ya uhakika, ila pia ilikuwa ni kivutio kikubwa sana hapa Kimanga, ilitengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu, kila aliyepita alisimama na kupashangaa. Jana nioni mida ya saa mbili nilipita pale, ni giza !

- Kutaka kujua zaidi kinachoendelea, nilimpigia simu mshikaji wangu wa kitengo cha IT. Mshikaji aliogopa kuongea nami kwenye simu, na kuniomba tukutane jioni ili tupate Kinywaji, ingawa naye alionyesha dhahiri kukerwa na huu uamuzi. Basi jioni yake tukakutana maeneo ya Bima, Cha kwanza kabisa, mshikaji alichoniambia, aisee, hii issue ni nzito, hawa wajerumani ni tishio, teknolojia yao imegusa maslahi ya wakubwa, jamaa wamechachamaa kule ndani. Walikuwa wanakula sana kwenye hizi ATM. Inveter na betri zimekuwa zinafungwa na makampuni yao. Hawataki kabisa kusikia juu ya hawa wajerumani. Kwa miaka miwili sasa, ATM ya kimanga ndio sehemu pekee ndani ya Benki ambako umeme ulikuwa haukatiki na wala simu za mitambo kusumbua zilikwisha kabisa. Idara inayoshugulikia maswala ya umeme na ATM maintenance zilifurahi sana na kudhania viongozi wangelipokea hii teknolojia kwa furaha zaidi na kuisambaza nchi nzima, lakini ikawa kinyume chake. Cha kushangaza zaidi, ni kwamba, hao wajerumani walifunga hiyo mitambo iliyotumika kwa miaka miwili bila kulipwa hata senti tano, na walipoanza kudai malipo ndio mambo yakaharibika

- Habari zilizovuja za ndani kwa ndani ambayo ndiyo sababu yangu kubwa ya kuvuja hii habari, ni kwamba, Mkurugenzi wa kitengo cha Ugavi, alitamba mbele ya wajerumani akiwaambia kwamba, aliyewapa ruhusa kufunga hii mitambo, ni mtu mdogo sana ndani ya benki. Kwa maana hiyo hawana vigezo kufanya biashara na NMB na hawatalipwa, kwa hiyo wao wakaondoe madude yao, na wawe tayari kusikia habari za huyo ofisa aliyewapa hidhini kufukuzwa ndani ya benki siku chache zijazo. Wakitaka wampe kazi. Habari zaidi zinadai kwamba, siku hiyo hiyo wajerumani walipong’oa mitambo yao pale kimanga, kampuni ndogo isiyoeleweka kutoka Kariakoo ilipewa hiyo kazi. Na kichekesho cha mwaka, pale wajerumani walipoanza tu kung’oa mitambo yao, ATM mbili ziligoma kufanya kazi na foleni ikaanza kwenye ATM moja iliyosalia. Huu ni uozo na uwenda wazimu, tangu lini vifaa vya kichina kutoka kariakoo vikawa na ubora zaidi ya vifaa vya Kijerumani?

- Sasa Napata picha ni kwanini Rais Magufuli anatumbua watu bila huruma. Ni kutokana na tabia za ajabu na ubinafsi uliopitiliza kama hizi hapa. Wewe kitu ambacho kimeonekana kuwa ndio suluhisho dhidi ya kero na matatizo siyo tu kwa benki, bali kwa wateja na wananchi, inapigwa vita kiasi hiki na hata vendor kufukuzwa? Kama siyo maslahi binafsi ni nini? Viongozi wangu ndani ya Benki, tendeni haki. Chunguzeni hii kitu kwa undani kabla ya huyu jamaa hajafukuzwa. Huyu ofisa asitolewe kafara. Bodi ya wakurugenzi wa NMB, ikibidi ingilieni kati. Vinginevyo serikali iingilie kati. Takukuru wawachunguze hawa viongozi wanaoweka maslahi binafsi kwenye taasisi za umma na kuzuia vitu vya maana vinavyoweza kutatua kero za wananchi huku wakiangalia matumbo yao binafsi. Huyu ofisa kwangu mimi ni shujaa kwa sababu alileta suluhisho. Kwanini ageuzwe kuwa kafara?

Kwani NMB wanafanya kazi kienyeji hivyo? Mtu mmoja anaweza kutoa tenda halafu mwingine akaja kuwafukuza waliopewa tenda?

Was it a pilot program? na kama ni pilot mtu mmoja anaweza luidhinisha kweli watu wafunge mitambo kwenye ATM? umefanya vizuri kuleta huu ujumbe ila bado nina maswali mengi kuliko majibu
 
= writing is an art. Siyo "arts".

Halafu mbona post yako hukuweka spacing sehemu zingine?

Nyani haoni kundule...
Asante kwa masahihisho.Ningeweka wewe Bibi Kifimbo Cheza ungekosa cha kukosoa.Hata hivyo mimi haikuwa lengo kumkosoa jamaa,bali kumuonyesha kuwa achukue ujumbe wa mleta mada na si namna ya uandishi.

Wasalimie Wajukuu zako,habari za K'koo au upo kwenu Canada?
 
Mkuu werrason jamaa mjanja sana huyo!!kujiondoa kabisa asifahamike kazunguka sana.Huo utangulizi haukuwa wa bahati mbaya,ni kuwaondoa relini wale wote watakaofanya juhudi za kumfahamu.Amefaulu,maana wengi wameamini utangulizi huo unamuhusu haswaa yeye kambw hapana
Ok, nami nimekamatika Hahahaa.
 
Habari zaidi zinadai kwamba, siku hiyo hiyo wajerumani walipong’oa mitambo yao pale kimanga, kampuni ndogo isiyoeleweka kutoka Kariakoo ilipewa hiyo kazi. Na kichekesho cha mwaka, pale wajerumani walipoanza tu kung’oa mitambo yao, ATM mbili ziligoma kufanya kazi na foleni ikaanza kwenye ATM moja iliyosalia. Huu ni uozo na uwenda wazimu, tangu lini vifaa vya kichina kutoka kariakoo vikawa na ubora zaidi ya vifaa vya Kijerumani?

- Sasa Napata picha ni kwanini Rais Magufuli anatumbua watu bila huruma. Ni kutokana na tabia za ajabu na ubinafsi uliopitiliza kama hizi hapa. Wewe kitu ambacho kimeonekana kuwa ndio suluhisho dhidi ya kero na matatizo siyo tu kwa benki, bali kwa wateja na wananchi, inapigwa vita kiasi hiki na hata vendor kufukuzwa? Kama siyo maslahi binafsi ni nini? Viongozi wangu ndani ya Benki, tendeni haki. Chunguzeni hii kitu kwa undani kabla ya huyu jamaa hajafukuzwa. Huyu ofisa asitolewe kafara. Bodi ya wakurugenzi wa NMB, ikibidi ingilieni kati.


Nadhani NMB serikali ina share za kutosha-kama kweli kuna uhuni huu nadhani hatua itachukuliwa.
cc.
Mhe. Mwigulu Nchemba
 
- Kuna kampuni ya wajerumani walioleta teknolojia (suluhisho la uhakika) ambayo imeonekana kuwa ni ya hali ya juu kwenye maswala ya nishati. Wakazi wa Tabata tumeliona hili pale Kimanga kwa miaka miwili sasa. Ila hii teknolojia imepigwa vita kali sana ndani ya benki, na hatimaye hao wajerumani wakafukuzwa.


Wakati huo kwa faida ya washindani wengine hiyo Teknolojia inaitwaje Mkuu? Na nikupitia Kampuni gani ya Kijerumani?
 
Hao wakubwa wa NMB wanawaza tu kupiga dili wakati huduma zinazorota hakuna usimamizi, branches zao unakaa kwenye foleni mpaka miguu inazama tumboni. Unakuta kuna tellers watano, wanne wamefunga anahudumia teller mmoja msururu wa watu. Tabu sana hawa watu.
 
Kama unaongea ukweli, ondoa hofu utakuwa salama. Tutakulinda!

Mzee Tupatupa

NMBCzar,

Kama ni taaarifa sahihi na ina ukweli ondoa shaka.
JPM atakulanao sahani moja. Ila siku nyingine ukiwasilisha taarifa kama hizi usitake kuwapa adui zako mwanya wa kuanza kuku-trace(fuatilia) kwa urahisi. Kwenye taarifa yako hukupashwa ufanye haya mawili:
  1. Kusema wewe ni mwajiriwa wa NMB.
  2. Kutaja mpaka eneo unalokaa.
Hayo ni makosa ya kiufundi ambayo yanaweze kugharimu ajira na uhai wako. Ujue nchi hii imejaa mafisadi kila kona na wako mpaka Ikulu. Next time please be careful!
 
Ni namna tu ya uandishi,wewe chukua lile la maana aliloliandika,haya mengine unayoona 'hayastahili" achana nayo.Writing is an Arts,not all do posses and learn.Hata ukoko wa juu wa wali hauwekwi meza kuu,lkn una umuhimu wake kwa wali kuiva vizuri.Kula wali na achana na ukoko...
Mi nikajua NMB wamekula hela ya Mwanae labda.. kumbe wala . Ni kweli si kila mmoja anajua kuwa specific. ila wajifunze.
 
Akili ndogo huwa inafocus kwenye vitu vidogo
Ndo ninyi ambao mnatongoza dem badala yakuwa specific unaanza muhadithia tamthilia ya Isidingo. Huwezi elewa umuhimu a kuwa straight to to the point ktk formal writing kama shule yako ndogo.

Hapa sio chit chat hivyo ilibidi awe makini na kutoweka porojo zisizo za maana.
 
Hili ni tatizo kweli Mkuu hapa umelileta sehemu sahihi linawafikia NMB NUSU INIFANYE NILALE NJE nilifika usiku mbeya zunguka Atm zote hazina pesa ninapoona huu ujinga ukiendelea masikitiko sana NMB BAHATI YENU NI BANK YA UMMA
Nani aliyekwambia ni Benki ya uma?? Thubutu. Wewe unafikili CEO NI MSWAHILI.
 
Back
Top Bottom