Ilikuwa Jumamosi moja mchana , mimi na rafiki zangu watatu tukawa tunapata bia moja baridi kwenye bar moja maarufu hapa jijini. Mara story zikaanza,. Rafiki yangu akaanza kuelezea jinsi jirani yake alivyopata masuluba ya nguvu usiku wa jana. " Bwana jirani yangu jana kakatwa vdole na mke wake wa ndoa usiku wa saa mbili . Ajabu ni kwamba mwanamke alikuwa anapiga mayowe kuomba msaada lakini sisi tulivyoenda kuangalia ni nini na kutoa msaada hakufungua mlango badala yake alijibanza mlangoni akisema utaniua , sifungui , sifungui. Wakati huo wakaja majirani wengine tukaamua tuite mjumbe wa nyumba kumi ili ikiwezekana tuvunje mlango. Lakini kabla ya hapo mmoja wetu akaingiza kamti dirishani akasogeza pazia ndipo tulipoona maajabu. Mwanamke akiiwa uchi kabisa alikuwa anagugumia kama anayekemea pepo, huku mwanaume akiwa ameshilikia mkono wa kushoto akionekana kuwa na maumivu makali sana ,huku akijaribu kuufunga kwa kitambaa. Ndipo tulipopata uamuzi wa kuvunja mlango kumuokoa jamaa . Mwanamke kusikia mlanago unavunjwa akakimbilia chumbani akajifungia. Ndipo tulipomtoa jamaa na kumpeleka hospitali." Kilichosabaibisha ni simu, mwanamke kapigiwa simu na mwanaume akawa anajifanya ni shoga yake , kumbe simu ilikwa ikisikika. Jamaa kumnyanganya kusikilizia akashangaa kusikia sauti ya mwanaume huku mkewe akitia mbwembwe eti sawa shoga tutaonana basi kesho sweetie.
Tulisikitika wee huku kila mmoja akilaumu jinsi wanawake wanavyowatendea wanaume mambo mabaya hatimaye wanaume kulaumiwa kwa unyanyasaji. Mwingine akisema hamna mwanamke anayepigwa na mumewe bila sababu, mwingine akichangia ooo wanawake wamezidiwa na ufuska amabao huufanya kwa siri lakini wakishtukiwa wanakuja juu kumbe huku anafanya kweli. Kila mmoja alichangia kivyake vyake kiasi kwamba hata jamaa waliokuwa pembeni yute walisogea mezani kwetu na story zikaendelea. Mwingine akisema 'ngaalia sasa wanataka vitu vya bei mbaya na ili kufanikiwa anapanga wanaume hata wanne na wewe wa tano wa nyumbani. Ukiwa kazini yeye aah mara sokoni , mara kwa shoga kumbe anakwenda gesti. Si nusu saa tu inatosha ?
Ikaja mpya ya mwaka . Mmoja wa jamaa waliosogea mezani kwetu akasikiliza wee kisha akasema. Wazee acheni tu. "Mimi Bwana mke wangu hanipigi ila mzee mimi nikiingia tu usiku nimepiga kamtungi kangu hanisemeshi , wala kunipa msosi . Sasa kuingia jikoni na kuanza kupasha naona haingii akilini kwa hiyo nijirusha zangu kitandani. Nikishalala tu yeye hujisogeza taratibu taratibu na kuhakikisha ameniwekea tako lake karibu kabisa na pua yangu halafu anatoa ushuzi, harakaharaka aninifunika na blanketi ili hiyo harufu ibaki humo humo. Da nikiamka asubuhi mchovu kweli kweli nashindwa kujua ni shauri gani. Hili amelifanya kwa muda mrefu kweli hadi binti yangu mdogo aliponiambia siku moja kitu mamayake ananifanyiaga.Sikuamini hadi nikamkamata ready handed. Hebu fikiria chakula chetu kikuu ni makande na maharage. Ushuzi wake ? unaweza kujua jinsi nimenyanyasika" True story.