Yusufu Manji alinuia kujenga 'Jangwani complex' Miaka ya mwanzoni 2010 Jangwani

kinje ketile

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
4,297
8,294
Yusuf Mehboob Manji alikuwa ni mmoja wa Wafadhili waliowahi Kuifadhili Yanga Afrika kwa Mafanikio Makubwa.

Baadhi ya Wachezaji aliowahi kuwasajili alikuwepo Kiungo Kamusoko mzimbabwe aliyetesa soka La Bongo.!

Kipindi cha ' Kampa Kampa tena' Yanga Afrika ilitawala Soka La Bongo.

Pamoja na hayo yote Alitangaza nia yake Ya Kujenga Uwanja pale Jangwani (Jangwani complex) utakaokuwa na Uwezo Kuingiza watu 40,000 pamoja na Magari yasiyopungua 1,000.

Yalitokea yaliyotokea na imekuwa ni stori kama stori zingine tu.

Ni nini Kilikwamisha ? Majibu anayo Manji, Wengine inabakia dhana tu.

Leo, injinia Hersi ambae ni Raisi wa Klabu anakuja na lile lile kwamba GSM ameahidi Kujenga Uwanja.

Wapi.? Pale pale Jangwani.

Wapo wanaodhani ni Siasa zile zile za Soka.

Pia,wapo wanao shangilia nia hiyo na Washaanza kutoa shukurani kwa GSM kana kwamba Kashajenga Uwanja.

Ni vema bila shaka,wakati ahadi kama hizi zinatolewa zingetazamwa kwa kina ni Sababu zipi zilisababisha Jangwani complex ya Yusufu Manji isifanikiwe. Na sasa kipi kimebadilika Ya GSM ifanikiwe.

Wakati tunasema Daima mbele Nyuma Mwiko....tutafakari hii pamoja..!
 
Aliyoyapitia manji kila mtu ana yafahamu haina haja ya kuelezea tena huyo GSM apewe mudu tu, ila wale wa kuchangia bukubuku na mudi pwagu akatia Bilion kadhaa ndy tuwaulize umekwamia wapi huo uwanja.
 
Mkuu mbona umeumizwa sana naa hii taarifa ya utopolo kujenga uwanja? Nini kinakusumbua?
Hao ni watani zangu, najuaga jinsi ya kuwazingua watoke huko vichakani waje kunishambua. Jibu hoja ya mleta mada. Kama haujaona alichouliza, ameuliza nini kilimkwamisha Yusufu Manji isifanikiwe. Na sasa kipi kimebadilika Ya GSM ifanikiwe?
 
GSM anakarabati Kaunda Stadium ya kufanyia mazoezi iwe na Uwezo Wa kubeba Watu 500.
Manji alikuwa na Wazo tofauti...
 
Back
Top Bottom