Kashfa: Mamlaka ya Vitambulisho vya Uraia (NIDA) yaiumbua Tume ya Uchaguzi na Serikali

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Mamlaka hiyo ya vitambulisho vya uraia {nida}imelalamikia kuwapo kwa watu ambao sio raia wa tanzania wanaomiliki vitambulisho vya kupigia kura.kitu ambacho kinapelekea zoezi hilo kuwa gumu

watu hao wametambulika katika zoezi linaloendelea sasahivi la kuandikisha watanzania kwaajili ya kupata vitambulisho vya uraia.

Chanzo:itv habari.
 
watu wameshachakachuwa wanachakachuwa mafuta na kura sembuse vitambulisho
 
Hii nchi kuna siku tutakuja kuongozwa na foreigner turushwe vichula mpaka tukome.Maana vitu vinavyofanyika ni wazi kwamba wahusika hawafikirii madhara kabla hawajatenda.Jamani tuwe makini hasa ktk ishu serious kama hizi
 
Hasa maeneo ya Kigoma, Kagera na Tabora tatizo hilo ni kubwa sana. Tunawajua hata wenye vitambulisho na raia zaidi ya moja!
 
Ni ufinyu wa kufikiri,ubinafsi na uzembe wa kushirikisha akili wa viongozi wa serikali yetu!

Unampa mtu card ya kupigia kura leo ili tu akupigie kura wewe siku hiyo, madhara ya baadae hujui na hutaki kujua!!
ni hatari!

Pia utaratibu wa NIDA wa uandikishaji na MBOVU!
 
Huko TISS tumejaza Wanyarwanda kibao,
hata Museven Rais wa Uganda baada ya kumaliza Masomo UDSM,
alikosoma bila kulipa hata senti moja,
alikuwa mwajiriwa wa UWT na kfanya kazi Ikulu.

Kabila naye siku zote aliishi na status ya UWT,
2015 tutaona Wachina nao wakipiga kura.

Wa kwanza kupata vitamburisho vya Uraia,
ni Wahindi, Waarabu Wasomali, Wakenya, Wacongo, Wanyarwanda na Wachina,
ndipo tunafuatia sisi raia wa Tanzania kwa taabu sana.

Kwao Kwao kwetu pia kwao.
Hii nchi kuna siku tutakuja kuongozwa na foreigner turushwe vichula mpaka tukome.Maana vitu vinavyofanyika ni wazi kwamba wahusika hawafikirii madhara kabla hawajatenda.Jamani tuwe makini hasa ktk ishu serious kama hizi
 
Hii nchi kuna siku tutakuja kuongozwa na foreigner turushwe vichula mpaka tukome.Maana vitu vinavyofanyika ni wazi kwamba wahusika hawafikirii madhara kabla hawajatenda.Jamani tuwe makini hasa ktk ishu serious kama hizi

Mbona tayari tumeongozwa na M'meto toka Msumbiji kwa miaka 10 toka 1995-2005.
 
Jambo la ajabu kwa serikali hii ya CCM, unaweza kuta sasa wanafanya mipango ya 'kupunguza' kasi ya NIDA. Wanaandaa mipango ya kuihujumu NIDA - maana kasi ya NIDA inatishia serikali - kuna uwezekano wa serikali kuachwa uchi zaidi.

Ingekuwa ni taifa linalojali uongozi bora, NIDA wangepaswa hata kuongezewa bajeti yao ili waweze kufanya kazi zaidi - ikiwa kupewa maslahi bora zaidi na hata kuhakikisha usalama wao.

Lakini katika inji hii ya wagagagigikoko - utashangaa NIDA 'itakavyokufa'.
 
Duh! ila hili twende nalo taratibu kidogo.... kwani hao tume ni akina nani? Are they super intelligent beings kung'amua uraia kwa kuangalia orodha ya majina au wakati wa kuandikisha tu..... Kwa nini nasema hivi.....

Wakati wa zoezi la kuandikisha wapiga kura katika kitongoji nilichopo walijichomeka wageni wa ki-congo hivyohivyo ila kwa utaratibu wa tume ni kwamba baada ya kuandikisha wanarudisha orodha ya majina (voters list) kwenye kata husika na wananchi wanatakiwa kukagua na kung'amua wageni.

Sisi tulichofanya ni kuwataja wageni kwa viongozi husika na mchakato wa kuong'oa ulifanyika, niseme tu sio mchakato straight-forward kama wengi tunavyofikiri, as it turned out wengine walishaomba uraia kwa taratibu stahiki na walikuwa raia, wengine waling'olewa kweli....

Mdau aliyefika kwenye kituo cha kuchukua form ya kujiandikisha kitambulisho cha uraia amenishuhudia ni total anarchy, naona wao ndi wata-swallow kila aina ya raia wageni, sijaona mtu wa RITA, Uhamiaji etc kama ambavyo nilisikia wakijinadi wakati fulani. Tetesi

My take:
1. Tume si wakulaumiwa, tuwalaumu wakazi wa eneo husika na viongozi wao wa mitaa/vijiji
2. Nahisi hawa NIDA mambo yanawashinda na wanatapatapa kulaumu, mara polisi/wanajeshi, mara tume ya uchaguzi
 
Hao wanaojiita NIDA ngoja mkulu awasikie; walipaswa kukaa kimya ili kulinda amani na utulivu wa nchi!!!!
 
Hii nchi kuna siku tutakuja kuongozwa na foreigner turushwe vichula mpaka tukome.Maana vitu vinavyofanyika ni wazi kwamba wahusika hawafikirii madhara kabla hawajatenda.Jamani tuwe makini hasa ktk ishu serious kama hizi

Tuongozwe na foreigner mara ngapi. Maana ya foreigner si ni yule anayefanya kazi Ministry of foreign,..right?!! Teh..teh...teh..walishatuongoza wawili tayari aaahaaa...aahahaa...aaaahha.
Sina dikshenari, natumia kamusi ya Kongo.
 
Kwa hili NIDA haana makosa ifwakti ni sisi wenyewe mimi na wewe ndo wenye wajibu wa kuilinda nchi yetu dhid ya wahamiaji haramu. Ni jambo la kuwapongeza angalau kuweza kujua kasoro kama hizo ndio maana wanathubutu kusema hawatatoa vitambulisho kwa haraka watajaribu kufuata utaraibu kuweza kubaini kasoro zote na kuwapa vitambulisho raia halisi. Shaka yangu ni kwamba ukishafungua dirisha ili upate upepo utakusanya upepo na wadudu vumbi kelele n.k vyote vitaingia ndani kuvingamua ni ngumu sana
 
Back
Top Bottom