Kashfa: Mamlaka ya Vitambulisho vya Uraia (NIDA) yaiumbua Tume ya Uchaguzi na Serikali

Kwani viongozi ndio waliokuwa wanaandikisha wapiga kura? Hawa NIDA hawajui sheria inasemaje wakimkuta mtu anaishi Tanzania bila kuheshimu sheria za nchi? NIDA sasa wamekuwa wasanii...
 
Nida hata mtandao huko vitongojini hawana. Hawawezi kutambua vyeti wala kadi/shahada feki zilizoletwa kwao kwa ajili ya kujiandikisha. Watajuaje? Sasa tumeingia Mkoa wa Kuhalalisha Wageni haramu kwa kuwapa Uraia Bureeeeeee. Nchi ya hovyo hovyo kila sekta!!
 
Kwani tz mgeni nani mwenyeji nani? Kwanini tusianzishe taifa la wahamiaji kama USA? Tuachane na utaifa uchwara.
 
Hili zoezi limekuja kuanza bila kufanyiwa Upembuzi yakinifu nina jirani yangu ni mkenya pure yeye na familia yake ya watu 5 lakini Ijumaa tumepanga foleni wanajiandikisha nadhani kwa sababu ni wajaluo watadai kwao ni rorya ama shirati.
 
ningekuwa mhusika mtu akija na kitambulisho cha kupiga kura wakati sio raia kwanza angakula makofi ya kuridhisha ndio nimkokote kwa mikono yangu hadi lupango sipendi kabisa ujinga wa aina hii hata kidogo!
 
Kama siyo raia na ana kitambulisho cha kupigia kura, si anastahili kufungwa huyu? Au ndo tuseme magamba waliwapa ili kuongeza idadi ya kura zao, hii ni hatari sana!
 
Tena kwenye vitambulisho vya uraia ndo balaa zaidi, nimeshuhudia mitaa ya kiwalani wapakistani wanaojificha kwenye ma gowdown wamefika kwa mtendaji kujiandikisha kinyemela,sijui serikali yetu imejipangaje katika hili
 
Tumezidi kulalama, hatuchukui hatua. Let society react! Ni kwa nini aliyetoa vitambulisho vya kupigia kura kwa mtu asiye raia asiadhibiwe mara moja. Tehe, tehe, tehe, pengine naye siyo raia, hapo inakuwaje?
 
Back
Top Bottom