DOKEZO Kashfa afisa elimu Longido, walimu ni Ngono na ulevi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Baadhi ya walimu katika shule ya Sekondari Kitumbeine, wilayani Longido, akiwemo Makamu wa shule hiyo Renatus Mwijage, wamekithiri kwa ulevi na vitendo vya ngono kwa wanafunzi.

Madai ya tuhuma hizo yametolewa na baadhi ya wananchi wilayani humo baada ya kulio chao kutosikilizwa , wakimlalamikia kaimu afisa elimu sekondari wilayani hapo,Gilbert Sombe kwa kufumbia macho matukio na mwenendo walimu hao ambayo yanatishia kudhorotesha maendeleo ya shule hiyo.

Taarifa zaidi zimedai kwamba makamu wa shule hiyo, Renatus Mwijage, amekuwa akifanya jitihada za kusaka nafasi ya ukuu wa shule baada ya kufanikiwa kumrubuni kwa fedha kaimu afisa elimu huyo ambaye alimemwahidi kumpatia nafasi hiyo katika moja ya shule wilayani hapo.

"Afisa elimu anatuhumiwa kula fedha za baadhi ya walimu akiwemo Renatus ambaye anadaiwa kutoa sh,milioni 5 ili kupatiwa ukuu wa shule"

Pia mwalimu Petro Mosses ambaye alihamishiwa katika shule ya sekondari Kitumbeine kutoka shule ya sekondari Longido akituhumiwa kufanya ngono na baadhi ya wanafunzi wake na wengine kuwapachika mimba.

Wazazi wanadai kuwa idara ya elimu imeshindwa kuwachukulia hatua walimu hao kwa sababu kaimu afisa elimu anawakumbatia kwa sababu amekuwa akichukua fedha na kuwaacha wafanye uchafu wao bila kukamewa.

Mwalimu mwingine chapombe ni ,Vickta Bayo ambaye anatajwa ndio kinara wa ulevi ambapo amekuwa akilewa muda wote wa kazi na wakati mwingine anajikojilea barabarani na kushindwa kufundisha darasani jambo ambalo kaimu afisa elimu analalamikiwa kwa kishindwa kuchukua hatua kiasi cha baadhi ya wazazi kuhoji ukaribu wa walimu hao na kaimu afisa elimu huyo.

Mwalimu Petro anatuhumiwa kutengeneza akaunti feki inayochafua viongozi mitandaoni na ana line feki inayotumika kuwatumia ujumbe baadhi ya wizara ya maendeleo ya jamii jinsia ,wazee na watoto , akidai shule hiyo kuna ukatili wa kutisha kwa wanafunzi unafanyika na pia kuwachongea viongozi wilayani hapo wakiwemo wakuu wa shule.

Wamemwomba rais Samia Suluhu kupitia wizara ya elimu kutuma timu ya uchunguzi juu ya mwenendo wa walimu hao pamoja na kaimu afisa elimu.
 
Baadhi ya walimu katika shule ya Sekondari Kitumbeine, wilayani Longido, akiwemo Makamu wa shule hiyo,Renatus Mwijage wamekithiri kwa ulevi na vitendo vya ngono kwa wanafunzi.
Enzi zetu tulikuwa tunawaheshimu sana walimu walevi. Hawakuwa wanahangaika na wanawake, siku akija darasani hajalewa hata hatufurahi maana tunajua siku hiyo namba hazitashuka. Walikuwa vipanga sana wa hesabu, physics na chemistry......waalimu wa siku hizi wakoje?
 
HIZI NI TAARIFA MUHIMU SANA,
MTOA MADA BARIKIWA, TUKIWA JAMII YA WATU WEPESAI WA KUTOA TAARIFA NI RAHIS MABADILIKO KUTOKEA.
KUNA MAENEO YA NCHI WATU WAKO KAMA MIUNGU.
 
Elimu inayotolewa kwenye shule za kidumu na ufagio zinamsaidia mtoto kuvuka MTO Tu ,watawala wote watoto wao wamepeleka kwenye shule wanazotoa elimu Bora huku wale wapigakura wao wakiwahadaa kwa madarasa yasiyokuwa na viti ,madawati ,hayo yote yanatokea Kwa sababu watoto wao hawasemi kwenye hizo shule,hivi ingekuwa mtoto wa Samia anasoma hizo shule huo uhuni wa kumtongoza mtoto ungekuwepo!

Morals hazipo tena Tanzania kuanzia familia ,kitongoji,kijichi,mtaa yaani ni Kansa inayotafuna dini na madhehebu yake ,njia raising ni kizazi hiki na serikali kiweke mitaala na katiba mpya iwekemwongozo WA watawala kumsomesha kwenye hizi shule za vidumu la sivyo taifa hili litakuwa la watu Malaya kama uwanja wa fisi
 
Baadhi ya walimu katika shule ya Sekondari Kitumbeine, wilayani Longido, akiwemo Makamu wa shule hiyo Renatus Mwijage, wamekithiri kwa ulevi na vitendo vya ngono kwa wanafunzi.
u kupitia wizara ya elimu kutuma timu ya uchunguzi juu ya mwenendo wa walimu hao pamoja na kaimu afisa elimu.
Dah nashukuru sikuwa na hata kuwaza kuwa mwalimu yaani ji majungu majungu mwanzo mwisho..
 
Back
Top Bottom