karume kungo'ewa, jk kung'olewa, sitta kung'olewa..........ama kweli hapa sasa kumekuwa kama jukwaa la kupoteza hisia !
Sio jukwaa la kupoteza hisia bali viongozi kama wapo wanaopita pita hapa watapata yale ambayo yamejaa mitaani ambayo mashushu hawawafikishii na kuwambia ukweli ulivyo,zaidi ya kuwapa moyo wa kuwa mambo ni mazuri.
Ila kama utaangaza angaza nchi za jirani utaona tuendapo si mbali,sasa lipi litasaidia kuepusha hali kama hiyo isitokee ni hawa viongozi kujali nchi yao na wananchi kwa ujumla na kuona ukaaji sawa kwa nchi zilizofika kunako mapambano,hali ya nchi heshima ya nchi ,kama kuiba lazima wajifikirie kuwa wameshaiba sana ,kama kufisidi ndio hakusemki kwani kila kitu kipo hadharani, sasa tikiwauliza zaidi ya hicho walichokwisha vuna wanataka kitu gani kingine ni lazima wao waliopo madarakani watanabahi na kuona wanakoipeleka nchi na nchi ilipoelekea hakuna mwisho mwema ,na wasifikiri kuwa kama wana marafiki wanao waelekeza vya kufanya ili waendelee na hali ya kahazi inavyokwenda basi wajue marafiki hao hawawatakii mema wao na nchi yao,marafiki hao wantamani na hii Tanzania iingie kwenye machafuko kama zilivyoingia nchi nyengine ,na hawa viongozi wetu waliopo madarakani wasitegemee kama marafiki hao watawambia wanachokitamani kitokee ,naamini kabisa kuna watu wanaitakia tanzania iingie katika matatizo kama yanayotokea nchi za jirani na hili sina shaka nalo kwani ,utawaona viongozi wetu kila wananchi wanavyojitahi kueleza matatizo na jinsi hali ya nchi inavyoyumba utawaona kama hawana habari au hawaoni ,jambo ambalo si kweli ila tamaa ndio iliyotawala katika akili zao kwamba wao ni mashujaa kuliko akina Mugabe ,Kibaki na Oginga ,Mabutu na wengineo hivyo watafanikiwa tu kuwanyamazisha watu kwa kauli za kila siku za "..mambo tunayashughulikia.."...watakaopatikana na hatia watafikishwa kwenye vyombo vya sheria " ...Uchunguzi haujakamilika..."...vyombo vinavyohusika vinafuatilia..."...hakuna ushahidi wa kumfikisha mtu mahakamani mpaka uchunguzi ukamilike.."tumeunda tume...."..tunasubiri kamati...." mambo ambayo yanakatisha tamaa na kuonekana ni udanganyifu wa kila siku ambao wananchi wameanza kuuzoea na kuonyesha kuchoshwa na kauli zisizotimizika au ahadi zisizotekelezwa na mwisho wake ndio kuja kutokea ile hatari wanayoisikia kutokea nchi jirani ,viongozi akina Kikwete na wenzako msijidanganye kabisa tena kuweni waangalifu haya mambo ya kutoa ahadi hewa yana mwisho na mara nyingi mwisho wake huwa mbaya kwa upande wa viongozi walio madarakani ,kwani wakati huo ukifika alie rafiki yako hatakuwa na nafasi na wewe na atakuepuka na kukuruka mbali sana ,sijui kama mnaifuatilia hali ya Bangaladeshi sijaona magazeti yetu kuandika chochote kwani kilichotokea huko ni matatizo ambayo hayana tofauti na haya yalioikumba Tanzania kwa sasa.
Mnaona tunaropoka lakini kwa kweli kabisa hatupendelei nchi iende kule ambako majirani zetu wanajuta kuikaribia hali hiyo,huenda ikawa mnatuona wachochezi ,au watu wa fitna au tunataka kuharibu tonge lakini hapana tunasema na kuandika haya tukitaraji mnasoma na kuelimika japo kwa kiasi kidogo ,tunaamini huenda ikawa mtasikiliza na kufuata au kutafuta suluhisho litakaloiokoa nchi kutumbukia kwenye janga,na haya yote hayatekelezeka ikiwa ahadi zenu ni ndefu na zina woga katika kutekeleza,watu wansema Katiba ibadilishwe ,mngeungana nao na kusema tukaeni na kutunga katiba,tume ina matatizo ,mngelisema tukaeni tuweke tume yenye kukubalika ,sasa kila mnaloambiwa mnalipiga chenga na kujifanya nyinyi ni wachezaji kuliko wengine ,hivyo sivyo watu wenye nia njema na nchi yao wanavyofanya ,someni nini kimetokea na kinaendelea Bangaladeshi,.!!!