Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,745
CUF kuwasilisha hoja kumng'oa Karume
*Yasema kauli yake dhidi ya Wapemba imevunja Katiba ---Hili ni uhakika kabisa na anafaa kuitwa mhani.
Na Reuben Kagaruki
CHAMA cha Wananchi (CUF) kinakusudia kuwasilisha hoja binafsi katika Baraza la Wawakilishi kuomba limuondolee madaraka ya Urais, Rais Aman Abeid Karume, kisha ashtakiwe kwa kutumia Ibara ya 37 ya Katiba ya Zanzibar kwa madai ya kutoa kauli ya kubagua Wapemba.
Hatua hiyo ya CUF ilitangazwa Dar es Salaam jana na Makamu Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Muafaka na Kiongozi wa Upinzania Bungeni, Bw. Hamad Rashid Mohamed alipozungumza na waandishi wa habari.
Alisema kauli ya Rais Karume aliyoitoa Ikulu ya Zanzibar wakati akizungumza na waandishi wa habari mapema wiki hii kuwa hawezi kuwashirikisha Wapemba kwenye serikali yake kwa sababu walimnyima kura ni dhambi kubwa na ni kinyume na Katiba ya Zanzibar.
Bw. Hamad, alisema CUF itawasilisha hoja hiyo kwa kutumia Ibara ya 37 ya Katiba ya visiwa hivyo inayoeleza kuwa; " Bila kujali masharti ya kifungu cha 36 Baraza la Wawakilishi linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja kuhusu Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa kifungu hiki."
Ukiangalia kuna kuoneshana kali Wabara wanawawajibisha Mawaziri ila WaPemba wamevuka lengo wanamwajibisha Raisi ,ingawa hawana uhakika wa kufanikiwa kutokana na kuwa ni minority katika baraza la wawakilishi ila wansema wao ikiandikwa tu katika kumbukumbu basi imetosha yaleyale ya kushindwa tunshindwa lakini chenga twewala.