Karume Kung'olewa -Hoja kufikishwa kwenye Bunge lao.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
CUF kuwasilisha hoja kumng'oa Karume

*Yasema kauli yake dhidi ya Wapemba imevunja Katiba ---Hili ni uhakika kabisa na anafaa kuitwa mhani.

Na Reuben Kagaruki

CHAMA cha Wananchi (CUF) kinakusudia kuwasilisha hoja binafsi katika Baraza la Wawakilishi kuomba limuondolee madaraka ya Urais, Rais Aman Abeid Karume, kisha ashtakiwe kwa kutumia Ibara ya 37 ya Katiba ya Zanzibar kwa madai ya kutoa kauli ya kubagua Wapemba.
Hatua hiyo ya CUF ilitangazwa Dar es Salaam jana na Makamu Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Muafaka na Kiongozi wa Upinzania Bungeni, Bw. Hamad Rashid Mohamed alipozungumza na waandishi wa habari.
Alisema kauli ya Rais Karume aliyoitoa Ikulu ya Zanzibar wakati akizungumza na waandishi wa habari mapema wiki hii kuwa hawezi kuwashirikisha Wapemba kwenye serikali yake kwa sababu walimnyima kura ni dhambi kubwa na ni kinyume na Katiba ya Zanzibar.
Bw. Hamad, alisema CUF itawasilisha hoja hiyo kwa kutumia Ibara ya 37 ya Katiba ya visiwa hivyo inayoeleza kuwa; " Bila kujali masharti ya kifungu cha 36 Baraza la Wawakilishi linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja kuhusu Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa kifungu hiki."

Ukiangalia kuna kuoneshana kali Wabara wanawawajibisha Mawaziri ila WaPemba wamevuka lengo wanamwajibisha Raisi ,ingawa hawana uhakika wa kufanikiwa kutokana na kuwa ni minority katika baraza la wawakilishi ila wansema wao ikiandikwa tu katika kumbukumbu basi imetosha yaleyale ya kushindwa tunshindwa lakini chenga twewala.
 
Hawa wapemba wana matatizo sana wao ndiyo wabaguzi wanajidai wao ndiyo kila kitu walitangaza kujilipua hapa hakuna mtu aliyewauliza.
Wote hao wanajiita waarabu na sera yao sasa hivi kuzaana saana ili wawe wengi.
 
teh tehe tehe funy
 
Umikusudia waarabu koko , ila ndio huko kuzaana usiseme ni madume wa mbegu wamekwisha katisha mikoa kibao ,Dar,Tanga hadi mwanza huko wanamwaga mbegu kwani wewe dada/kaka unatoka mkoa gani ?
 
madhali sheria inawaruhusu wache watimize wajibu wao waliotumwa na wananchi.
karume kusema maneno hayo ni ya kibaguzi, japokuwa kweli wapemba hawakumpigia kura.
does it mean raia wako anakuwa si raia wako tena kwa kuwa hajakupigia kura? demokrasia ipo wapi?
 
[wao ikiandikwa tu katika kumbukumbu basi imetosha yaleyale ya kushindwa tunshindwa lakini chenga twewala.[/I][/QUOTE]

Kufungwa tafungwa lakini chenga twawala

CUF kuwasilisha hoja kumng'oa Karume

*Yasema kauli yake dhidi ya Wapemba imevunja Katiba ---Hili ni uhakika kabisa na anafaa kuitwa mhani.

Na Reuben Kagaruki

CHAMA cha Wananchi (CUF) kinakusudia kuwasilisha hoja binafsi katika Baraza la Wawakilishi kuomba limuondolee madaraka ya Urais, Rais Aman Abeid Karume, kisha ashtakiwe kwa kutumia Ibara ya 37 ya Katiba ya Zanzibar kwa madai ya kutoa kauli ya kubagua Wapemba.
Hatua hiyo ya CUF ilitangazwa Dar es Salaam jana na Makamu Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Muafaka na Kiongozi wa Upinzania Bungeni, Bw. Hamad Rashid Mohamed alipozungumza na waandishi wa habari.
Alisema kauli ya Rais Karume aliyoitoa Ikulu ya Zanzibar wakati akizungumza na waandishi wa habari mapema wiki hii kuwa hawezi kuwashirikisha Wapemba kwenye serikali yake kwa sababu walimnyima kura ni dhambi kubwa na ni kinyume na Katiba ya Zanzibar.
Bw. Hamad, alisema CUF itawasilisha hoja hiyo kwa kutumia Ibara ya 37 ya Katiba ya visiwa hivyo inayoeleza kuwa; " Bila kujali masharti ya kifungu cha 36 Baraza la Wawakilishi linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja kuhusu Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa kifungu hiki."

Ukiangalia kuna kuoneshana kali Wabara wanawawajibisha Mawaziri ila WaPemba wamevuka lengo wanamwajibisha Raisi ,ingawa hawana uhakika wa kufanikiwa kutokana na kuwa ni minority katika baraza la wawakilishi ila wansema wao ikiandikwa tu katika kumbukumbu basi imetosha yaleyale ya kushindwa tunshindwa lakini chenga twewala.

..wazanzibari kwa maneno bwana!
 
Wasiwasi wangu mkubwa ni hapo kwenye minority na majority. Naona mwandishi wa habari husika ameshakuwa na conclusion kwamba motion itapita ndani ya baraza la wawakilishi. CCM tunaijua kwa mchezo mchafu. Na CUF wanaijua CCM kwa mchezo mchafu ndio maana wamekataa kura za maoni kwenye suala la serikali ya mseto. Sasa sijui CUF inatarajia kupata nini kwenye baraza la wawakilishi. Au kule sio rahisi kuiba? Nakumbuka Kenya juzi juzi waliiba hata kura za kumchangua spika wa bunge. Nadhani wengi mnajua nini kilitokea.

Ni jaribio zuri. Lets keep our fingers crossed.
 
sasa imekuwaje, huyo karume keshang'olewa au bado?? wenye updates watupe plz ! this is just another proposal going cold !
 
sasa imekuwaje, huyo karume keshang'olewa au bado?? wenye updates watupe plz ! this is just another proposal going cold !
Hang'oki mtu labda kwa risasi.Wao wamepindua sasa anaetaka utawala lazima nao utumie njia ile ile ya mapanga ,utawala huu wa wahafidhina haukupatikana kwa vikaratasi kama wa huko Tanganyika hapa aliondolewa mtu mzalendo kwa mtutu na ukali wa mapanga ,ila Karume aliondlewa kwa risasi wengine wakadai kilikuwa ni kisasi kwa aliemuua karume na haswa ndivyo inayoshikiliwa kuwa karume aliuliwa kwa kulipiza kisasi na sio madhumuni ya kuipindua serikali ,ni stori maarufu sana pale Unguja..
 
sincerely speaking huyu bwana hana baraka yoyote angengolewa tu .... maana kipindi cha salmini afadhali .... na huyu watu wanazidi ufukara tu .... anawafungulia watoto wake miradi ya hoteli na kuwaozesha wafaransa .... kwanza siyo yeye anaendesha nchi ni yule mamaake maana nasikia amri zote zatoka kwake .... mihashuo .. mtu mzima ho.....
 
mnajua tunapenda kuwadanganywa wakati wote, statement zinazotolewa na viongozi wa CCM zanzibar wakati wakiwa kwenye majukwaa ni za kweli wala hazina ubishi ila tukienda kumuuliza makamba anasemaje kuusiana na staement hizo anasema ni mawazo yao binafsi na sisi tunakubali kuwa ni mawazo binafsi.

Kiongozi mmoja wa CCM zanzibar alishasema kuwa hakuna siku ambayo CUF watapata madaraka labda watumie upanga kama wao walivyoyapata kwa upanga tulipouliza tukaambiwa hayo ni mawazo yake binafsina tukakubali, lakini haya mawazo yanmatoka wapi au yanaaniza kwenye vikao rasmi kwenye maongezi ya off the minutes.

haitawezekana kumtoa karume oohps Dr. karume, madarakani hata kwanini na CUF wasahau madaraka zanzibar labda wayapate kwa ncha ya upanga, lets wait and see.
 
suali la msingi hio hoja yenu iso na mashiko mtaipeleka lini barazani tukuchekeni?

mzee, hold on ! kwanza hawawezi hata in siku moja kufikiria kumfikisha karume barazani kwa kutaka ang'olewa, rais hawezi kung'oka just because watu wanafikiria ang'oke ! watachemsha ! kwanza ilikuwa karume, na sasa jk ang'olewe, lol !
 
CUF wataifikisha hiyo hoja maana hawa CUF ni kiboko ,sema wao hawajali kama wengine wataunga mkono au hawaungi lakini muhimu habari itawekwa kwenye recodi za bunge.
 
karume kungo'ewa, jk kung'olewa, sitta kung'olewa..........ama kweli hapa sasa kumekuwa kama jukwaa la kupoteza hisia !
 
karume kungo'ewa, jk kung'olewa, sitta kung'olewa..........ama kweli hapa sasa kumekuwa kama jukwaa la kupoteza hisia !
Sio jukwaa la kupoteza hisia bali viongozi kama wapo wanaopita pita hapa watapata yale ambayo yamejaa mitaani ambayo mashushu hawawafikishii na kuwambia ukweli ulivyo,zaidi ya kuwapa moyo wa kuwa mambo ni mazuri.
Ila kama utaangaza angaza nchi za jirani utaona tuendapo si mbali,sasa lipi litasaidia kuepusha hali kama hiyo isitokee ni hawa viongozi kujali nchi yao na wananchi kwa ujumla na kuona ukaaji sawa kwa nchi zilizofika kunako mapambano,hali ya nchi heshima ya nchi ,kama kuiba lazima wajifikirie kuwa wameshaiba sana ,kama kufisidi ndio hakusemki kwani kila kitu kipo hadharani, sasa tikiwauliza zaidi ya hicho walichokwisha vuna wanataka kitu gani kingine ni lazima wao waliopo madarakani watanabahi na kuona wanakoipeleka nchi na nchi ilipoelekea hakuna mwisho mwema ,na wasifikiri kuwa kama wana marafiki wanao waelekeza vya kufanya ili waendelee na hali ya kahazi inavyokwenda basi wajue marafiki hao hawawatakii mema wao na nchi yao,marafiki hao wantamani na hii Tanzania iingie kwenye machafuko kama zilivyoingia nchi nyengine ,na hawa viongozi wetu waliopo madarakani wasitegemee kama marafiki hao watawambia wanachokitamani kitokee ,naamini kabisa kuna watu wanaitakia tanzania iingie katika matatizo kama yanayotokea nchi za jirani na hili sina shaka nalo kwani ,utawaona viongozi wetu kila wananchi wanavyojitahi kueleza matatizo na jinsi hali ya nchi inavyoyumba utawaona kama hawana habari au hawaoni ,jambo ambalo si kweli ila tamaa ndio iliyotawala katika akili zao kwamba wao ni mashujaa kuliko akina Mugabe ,Kibaki na Oginga ,Mabutu na wengineo hivyo watafanikiwa tu kuwanyamazisha watu kwa kauli za kila siku za "..mambo tunayashughulikia.."...watakaopatikana na hatia watafikishwa kwenye vyombo vya sheria " ...Uchunguzi haujakamilika..."...vyombo vinavyohusika vinafuatilia..."...hakuna ushahidi wa kumfikisha mtu mahakamani mpaka uchunguzi ukamilike.."tumeunda tume...."..tunasubiri kamati...." mambo ambayo yanakatisha tamaa na kuonekana ni udanganyifu wa kila siku ambao wananchi wameanza kuuzoea na kuonyesha kuchoshwa na kauli zisizotimizika au ahadi zisizotekelezwa na mwisho wake ndio kuja kutokea ile hatari wanayoisikia kutokea nchi jirani ,viongozi akina Kikwete na wenzako msijidanganye kabisa tena kuweni waangalifu haya mambo ya kutoa ahadi hewa yana mwisho na mara nyingi mwisho wake huwa mbaya kwa upande wa viongozi walio madarakani ,kwani wakati huo ukifika alie rafiki yako hatakuwa na nafasi na wewe na atakuepuka na kukuruka mbali sana ,sijui kama mnaifuatilia hali ya Bangaladeshi sijaona magazeti yetu kuandika chochote kwani kilichotokea huko ni matatizo ambayo hayana tofauti na haya yalioikumba Tanzania kwa sasa.
Mnaona tunaropoka lakini kwa kweli kabisa hatupendelei nchi iende kule ambako majirani zetu wanajuta kuikaribia hali hiyo,huenda ikawa mnatuona wachochezi ,au watu wa fitna au tunataka kuharibu tonge lakini hapana tunasema na kuandika haya tukitaraji mnasoma na kuelimika japo kwa kiasi kidogo ,tunaamini huenda ikawa mtasikiliza na kufuata au kutafuta suluhisho litakaloiokoa nchi kutumbukia kwenye janga,na haya yote hayatekelezeka ikiwa ahadi zenu ni ndefu na zina woga katika kutekeleza,watu wansema Katiba ibadilishwe ,mngeungana nao na kusema tukaeni na kutunga katiba,tume ina matatizo ,mngelisema tukaeni tuweke tume yenye kukubalika ,sasa kila mnaloambiwa mnalipiga chenga na kujifanya nyinyi ni wachezaji kuliko wengine ,hivyo sivyo watu wenye nia njema na nchi yao wanavyofanya ,someni nini kimetokea na kinaendelea Bangaladeshi,.!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom