Karume Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Karume Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwiba, Feb 2, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kuna tetesi kuwa Rais wa Seikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Abeid Amaan Karume kuwa atapewa nafasi ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM 2015,habari zimezidi kuelezea kuwa yeye ndie atake kuwa mrithi wa Kikwete baaada ya Mheshimiwa Kikwete kumaliza ngwe yake 2015. Maandalizi ya kumuwezesha Mheshimiwa Karume kukubalika ifikapo mwaka 2015 yameanza na kufanya ziara za mara kwa mara katika mikoa ya Tanzania Bara ili kumjenga kwenye macho ya wananchi.

  Hii inasemekana imetokana na utamaduni ambao kuna haja ya kuona unaendelezwa wa kupokezana nafasi ya kiti cha Urais wa Tanzania kwa upande wa bara na visiwani.Baada ya kokosekana wakati alipoondoka Mheshimiwa Benjamin Mkapa.

  Pia habari zimezidi kutonya kuwa upo uwezekano wa mgombea huyo kupitia CCM kusimama katika kugombea kiti hicho kwa uchaguzi mkuu ujao 2010 endapo Rais Kikwete akiamua kupumzika, habari za wachunguzi wa mambo ya siasa wameona jitihada za Mheshimiwa Karume kuwekwa mstari wa mbele katika shughuli nyingi za Kichama hapa Tanzania Bara na Chama chake.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hana mvuto wakutosha kugombe URT!
   
 3. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Huyu jamaa hawezi uraisi wa Tanzania. Kwanza swala la CUF ameshidwa kulitatua, pili sasa wanasema mafuta yakipatikani zanzibar hayatakuwa ya Tanzania. Huyu jamaa ataivunja nchi yetu na kuturudisha nyuma tunataka kizazi kipya.
   
 4. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Itakuwa vigumu sana kumuuza. Iwapo atapewa nafasi ya kugombea Urais wa Tanzania basi wasahau ikulu.
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Itakuwa vigumu kumuuza katika CCM au CCM kumuuza kwa wananchi?

  Hivi wananchi wa Tanzania wana uchaguzi kweli? Au wanachaguliwa rais na CCM?
   
 6. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  KUDO'S Kiranja,you are spot on
   
 7. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  NAdhani Tanzania hatujakosa watu wakuweza kuongoza hata Karume alazimishiwe kuandaliwa kuwa mrithi wa Jk. Binafsi ningeshauri apumnzike maana toka babu yake mpaka yeye wanmekuwa viongozi wa Zanzibar na sasa wanataka kuja Mainland. Sidhani kama an ushawishi wa kuja bara. Hakuna makubwa saana aliyoyafanya zanzibar yatakayotulazimu tuamini kwamba yeye anaweza kuwa bora kuliko wengine wote.By the way habri hii inapwaya can u put more authorities?
   
 8. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  I real hope this is just a rumour, i real hope for TZ's sake!!mmmh tunapoelekea ndipo sipo!
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapo ndipo ninapowashangaa hao wanaosema hapiti,sijui hana sifa,hawajakosa watu wa kuongoza,itakuwa vigumu kumuuza wengine hana mvuto wa kutosha.
  We hang the petty thieves and appoint the great ones to public office.Hiyo ndio CCM haikuhitajii wewe unauona vipi uteuzi wao
  Jamaa ndo kishaanza vijiziara vya chatichati kama ni kweli tutaona.
   
 10. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  nani ampigie kura huyu kipofu na bubu kiziwi? zanzibar yenyewe hawezi na hajaweza kuiongoza vizuri, anapelekwa tu kama gogo. mimi nitafurahi kama atagombea, ili ccm ipotenza kiti mwaka huo huo wapinzani tuchukue.
   
 11. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Aliuzwa Mkapa akiwa ndani ya gunia itakuwa karume yupo kwenye tenga!!
   
 12. K

  Kwaminchi Senior Member

  #12
  Feb 2, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama katiba ya CCM na katiba ya nchi inamruhusu mtu yeyote aliyemaliza muda wake wa U-rais Zanzibar kugombea U-rais wa Tanzania au aliyemaliza muda wake wa U-rais Tanzania kugombea U-rais Zanzibar, uwezekano wa Rais Amani Abeid Karume kugombea U-rais wa Tanzania upo, ikiwa hivyo ndivyo CCM yenyewe inavyotaka.

  Tatizo la chaguzi nchini Tanzania si la leo, hasa ukiiangalia Katiba ya Jamhuri ya mwaka 1962 ya utawala wa chama kimoja. Katiba hiyo ndiyo tuliyonayo mpaka hii leo. Haina tofauti kubwa sana na ya mwaka 1977 na wala haijabadilika sana pamoja na kutiwa viraka kadhaa wa kadha.

  Mwananchi wa kawaida amenyimwa uwezo wa kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa nchi aitakayo na hana nafasi ya kumchagua kiongozi yeyote amtakaye katika nafasi yoyote ya uongozi.

  Mwananchi anapewa nafasi ya kugombea na chama na anapewa nafasi ya kumchagua yule tu ambaye chama kimekwisha mchagua.

  Sasa, kama mtu amechaguliwa na chama na sisi wananchi hatumtaki, hatuna uwezo wa kumzuia mtu huyo asishike nafasi ya uongozi. Tukisusa kumchagua, atachaguliwa na tukimpigia kura atachaguliwa.

  Hatamu za nchi zimeshikwa na chama na mwananchi hana upenyu. Ni chama tu ndio chenye nchi na serikali.
   
 13. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Sidhani leo hii kuna muuzaji aina ya Nyerere ...
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Feb 2, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Naona hizi ni ndoto za mchana. Tanzania ya 2015 si ile ya 1972. Ningewashauri hawa watoto wa wakubwa, Karume na Mwinyi wakapumzike.
   
 15. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #15
  Feb 2, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kilaza huyo Karume atakuwa rais wa nani? Kawatosha Wazanzibari, kwenye muungano asahau.
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Feb 2, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nobody believes a rumor here in Tanzania until it's officially denied so let us wait and c.
   
 17. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #17
  Feb 2, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Muuzaji si nyerere wala Malecela et al, muuzaji ni mfumo wa Katiba inayompa madaraka ya mwisho "Jaji Lewis Makame" kumtangaza yule anayetaka ashinde bila kuhojiwa na mahakama wala chombo chochote cha sheria. CCM hata ikisimamisha PAKA kugombea urais atatangazwa mshindi. Elewa hilo!. Yaani uchaguzi bongo hufanywa na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM, ukishinda uteuzi basi unasubiri kuapishwa tu. Haya mengine ni mazingaombwe tu.
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  Feb 2, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hivi huna lugha nzuri zaidi ya hapo? Ndio maana JK kawaita walevi wa tende huku Makamba akiwafananisha na Mapaka
   
 19. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #19
  Feb 2, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Madamu ana PhD nadhani anafaa kabisa. Hatujawahi kuwa na mgombea uraisi wa CCM mwenye PhD......
   
 20. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #20
  Feb 2, 2009
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Yaani pamoja na CCM kuwa madarakani tangu zamani hizo bado kuna Watanzania wenzetu hawakielewi vizuri chama hiki na mbinu zake za kuhodhi madaraka....

  Kwa taarifa ni kwamba hata CCM ikiamua kwamba badala ya Karume wamsimamishe Chenge,Lowassa,Karamagi au Makamba,na wakatumia "kamati za ufundi" basi mtu anaingia Ikulu.Tusijidanganye kuwa mazingira yaliyotumika kumnadi Mkapa yamebadilika kwani ushahidi tosha ni namna JK alivyoweza kuingia Ikulu licha ya kuzungukwa na maharamia waliojificha katika joho la mtandao.

  Ni vema tukatofautisha matamanio yetu na hali halisi ya siasa zetu.Matamanio ni kuona kiongozi mwenye sifa stahili ndio anashika madaraka,hali halisi ni kinyume:wanapendekezana,zinatafutwa fedha (kama za EPA) kusaidia kumuuza mgombea,wenye njaa ambao ndio wengi wanaleweshwa na porojo za ahadi lukuki.....mtu anaingia Ikulu
   
Loading...