Karume Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,669
0
- Hizi tetesi ni za kawaida kwenye siasa, kama vile zile za kwamba Dr. Hussein anatayarishwa kuwa rais ndio maana amepelekwa kule Visiwani, Karume ni kiongozi mnyonge sana kuweza kuwa rais wa Muungano, na besides sio rahisi kwake kuyashinda au hata kushindana na makundi ya bara ya kisiasa, infact yatamfukia shimoni kisiasa kama yalivyomfanya Salim.

- Kwa maoni yangu, ili Muungwana arudi tena 2010 anawahitaji sana kina Lowassa na the gang, uchaguzi wa UWT ulikuwa ni utabiri tosha wa yatakayojiri kati ya 2010 na 2015, ninaamini kuwa Muungwana atakata deal na kundi la Lowassa, ili awaachie 2015 na ili wamsaidie 2010.

- Katika mvutano na hii deal ya Lowassa na Muungwana, Karume hana nafasi kabisa, infact wajumbe wengi wa NEC hawajasahau jinsi Karume na kundi lake walivyomuabisha rais kwenye kikao cha CCM Butiama, kuhusu muafaka maana walimvunjia sana heshima Muungwana, huku ikionekana wazi kuwa Karume hana control kabisa over wajumbe wake, na yeye akiwa kama kiongozi mkuu wa CCM huko Visiwani.

- Kiongozi wa Visiwani, aliyekua na nafasi kubwa ya kuwa rais wa Muungano, alikuwa Komandoo, lakini na yeye alijiharibia kwa kuwaudhi wajumbe wa NEC na CC, na yale madai yake ya term tatu, akaishia kukosa yote. Karume ana utata mkubwa sana kifamilia na nduguye Ali, ambaye wajumbe wengi wa NEC wana sympathy naye zaidi kuliko Amani,na kwenye hili Ali atajiunga na kundi moja la Bara na mara utasikia yale yale ya Salim na zamani.

- Halafu kuna Shamuhuna na Khatibu, ambao nao pia wana hamu kubwa sana ya urais, Khatibu ni mtu wa karibu sana tena sana na Muungwana, kama kuna nafasi ya kumpa urais mtu wa Visiwani, Khatibu ndiye atakayekua chaguo la kwanza la Muungwana kabla ya anybody else,

I mean sioni nafasi ya Karume kwenye urais wa Muungano, no way na ni maoni yangu tu!
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,113
2,000
- I mean sioni nafasi ya Karume kwenye urais wa Muungano, no way na ni maoni yangu tu!

Nakubaliana na wewe kuhusu Karume, achilia mbali kupewa Urais wa muungano hata Uwaziri hastahili. Pia nitafurahia sana kama ndani ya CCM kuna watakaokuwa na sauti ya nguvu kupinga kuteuliwa tena Kikwete kugombea 2010. Kwa maoni yangu kazi imemshinda, huu ni mwaka wa nne sasa tangu aingie madarakani lakini hakuna chochote alichofanya cha kujivunia kama Rais wa nchi. Je, kama watatokea wenye sauti nyingi za kumpinga Kikwete ni nani atakayestahili kuwa mgombea wa CCM 2010? Labda Mwakyembe huyu labda anaweza kutufaa sana Watanzania kama hana madudu yake ndani ya chama na serikali.
 

Kaizer

JF-Expert Member
Sep 16, 2008
25,269
2,000
Nakubaliana na wewe kuhusu Karume, achilia mbali kupewa Urais wa muungano hata Uwaziri hastahili. Pia nitafurahia sana kama ndani ya CCM kuna watakaokuwa na sauti ya nguvu kupinga kuteuliwa tena Kikwete kugombea 2010. Kwa maoni yangu kazi imemshinda, huu ni mwaka wa nne sasa tangu aingie madarakani lakini hakuna chochote alichofanya cha kujivunia kama Rais wa nchi. Je, kama watatokea wenye sauti nyingi za kumpinga Kikwete ni nani atakayestahili kuwa mgombea wa CCM 2010? Labda Mwakyembe huyu labda anaweza kutufaa sana Watanzania kama hana madudu yake ndani ya chama na serikali.

Hivi naomba kuuliza, bado ni mjumbe wa baraza la mawaziri la Muungano? Kwa maana ya kwamba anawajibika kwa JK? au imebadilishwa siku hizi?
 

NTIRU

Member
Sep 20, 2007
43
0
Wana-JF, kuna anayefikiria hili zezeta la Zenj kuwa Rais wa Muungano? Jamani acheni utani. Pamoja na kinachoelekea kuwa umbumbumbu wa wapiga kura wa Tz, sidhani kama huyu "Rais wa Kulazimisha" wa Zenj ataweza kupata nafasi ya kuongoza nchi Tz!! Hivyo visiwa viwili tu vyenye watu chini ya milioni na nusu vimemshinda ataweza Wananchi zaidi ya 40m wa Tz? Kwanza kule kusema tu kwamba Karume atagombea hakufai, nani anamtaka rais zebezebe kama alivyo. Aishie huko huko!!!
 

a.9784

Senior Member
Feb 19, 2008
146
0
Kwa sababu Tanzania imekua nchi ya mtu kujifunza uongozi then Karume anaweza kuupata huo urais kama walivyopanga,CCM wakitaka kukiua chama wampe hiyo nafasi wakione cha mtema kuni.

Na hii tabia ya kupokezana vijiti ife,tunahitaji mtu anayeweza kutuongoza na sio suala la kutoka bara au visiwani.

Kama kutakua na ulazima wa kupokezana vijiti basi Nahodha apewe hiyo nafasi na sio Husseini Mwinyi,hii sio nchi ya kifalme.Haapa sio kwa king Mswati.

Karume & Mwinyi NO
 

Stone Town

Senior Member
May 28, 2007
114
195
CCM haina destruri ya kcuhagua ina desturi ya kuweka kwa hivyo watakaoamua kumuweka nani awe rais ni wao suala la kura ni fomalty tu na sio kama ni suala la mtu kupewa demokrasia ya kuchagua kwa maana hiyo wao ndio wenye maamuazi ya kuwachagulia watanzania nani atakuwa rais wa nchi na kama ni hivyo basi watuwekee yeyote wanomtaka wao na sisi tutakuwa tunamheshimu kama inavyotokea kwa hao wengine maana siamini kama hizo chaguzi nyengine zote sio zanzibar wala bara zinafuata misingi ya kidemokrasia ni tunachaguliwa na kupangiwa nani awe kiongozi.

lakini wa kulaumiwa ni sisi watanznaia tuliozowea kuchaguliwa na tukakubali maana hakuna asiyeona chaguzi zetu zinavyokwenda na sisi tumekaa kimya kama tmemwagiwa maji ya barafu.
 

Jamco_Za

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,331
1,225
Tunasahau kitu ambacho kiko wazi tanzania, hakuna uchaguzi bali CCM wanaamua wanataka kumpa nani madaraka mwaka furani wa uchaguzi. wakimsimamisha ataongoza tanzania. tunachotakiwa ni kujadili matokea ya mtu kama karume kuwa rais wa URT na sio uwezekano kwani hilo linawezekana.

Nahiona URT ikitumbukia shimoni wakati wa uongozi wa Karume kwani kila kitu ambacho kimeanzishwa na JK especially little freedom of information we have ambao ndio unasababisha tuwepo hapa JF saa hizi hautakuwepo tena.
 

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,611
1,250
Wana-JF, kuna anayefikiria hili zezeta la Zenj kuwa Rais wa Muungano? Jamani acheni utani. Pamoja na kinachoelekea kuwa umbumbumbu wa wapiga kura wa Tz, sidhani kama huyu "Rais wa Kulazimisha" wa Zenj ataweza kupata nafasi ya kuongoza nchi Tz!! Hivyo visiwa viwili tu vyenye watu chini ya milioni na nusu vimemshinda ataweza Wananchi zaidi ya 40m wa Tz? Kwanza kule kusema tu kwamba Karume atagombea hakufai, nani anamtaka rais zebezebe kama alivyo. Aishie huko huko!!!

Hapana sio zezeta ila huyu jamaa ana asili ya ubabe kama baba yake sasa CCM wameona wakishampa Uraisi huu wa Jamhuri wa Tanzania atavitumia vyombo vya dola vizuri sana ,hawa wapinzani akina Zitto na wenzake watakiona kilichomtoa kanga magoya,atakuwa hawasikilizwi na wataachwa wapige makele kama akina Seif Sharifu halafu anaweza akawasukumizia kesi ya uhaini wakasota jela miaka kibao ,kisha wakaachiwa na yeye atasema amewasamehe.
 

Spear

JF-Expert Member
Jun 21, 2008
510
225
nani ampigie kura huyu kipofu na bubu kiziwi? zanzibar yenyewe hawezi na hajaweza kuiongoza vizuri, anapelekwa tu kama gogo. mimi nitafurahi kama atagombea, ili ccm ipotenza kiti mwaka huo huo wapinzani tuchukue.

Please please Please God mjalie kiuumbe wako Karume angoze Tanganyika (Tanzania)I can`t wait to see that day I would be more than happy
 

bm21

JF-Expert Member
May 12, 2008
774
0
Come on guys lets be determined. It appears we 're not sealing in the same boat! let him stand for who said that he will not win? Leave him if he won in Zanzibar why not in Mainland?. We shouldn't be good sample size for CCM political surveys.
 

Pundamilia07

JF-Expert Member
Oct 29, 2007
1,434
1,195
Ndiyo maana CCM inakuwa na nguvu sana kisiasa kwani washauri ni wengi na haipati shida ya kupata ushauri huo.

Tuendelee kuipatia ushauri ili ipate kujiimarisha zaidi.
 

Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,712
1,225
yakhe tupeni karume nasisi tuwape mtikila, dili safi hiloo!

NO, Wazanzibari wangeprefer Mizengo Pinda kwani pengine angejua uzito wa mzigo wa wananchi wasio na nchi na kutengwa na viongozi wa serikali inayojidai ina jukumu nao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom