Kumbe JF bado ni source ya habari kwa blogs nyingine. Nimeinasa hii kwenye blog yao yaani wamekata na kupaste kama ilivyo bila hata mention ya jamiiforum as if ni habari yao.
Karume aliyakimbia mapinduzi?
Rais Karume akizungumza kwenye TBC, amekanusha ule uvumi wa Karume kuyakimbia Mapinduzi ya mwaka 1964.
Akieliezea Rais Karume amesema mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika kwa muda wa masaa 2 tuu, kuanzia saa 8:00 usiku hadi saa 10 alfajiri ya Jumamosi ya tarehe 11/01/1963 kuamkia Jumapili tarehe 12/01/1964.Hivyo kulikucha salama usalmini.
Hivyo Jumapili hiyo, yeye Karume alikuwa na safari ya kwenda Dar es Salaam ili awapeleke watoto wake, Amani na Ali masomoni huko Malawi (
Kuna hoja iliwahi tolewa Karume ni Mnyasa wa Malawi, alikuja Zanzabar kama kuli Bandarini Zanzibar) hivyo watoto kumbe walisoma kwao?
Karume akaendelea kusema kuwa hiyo Jumapili asubuhi, walitafuta usafiri wakakosa, hivyo wakasafiri na mtumbwi toka Zanzibar saa 7 mchana, wakafika Mbweni saa 11 jioni.
Waliposhuka pwani ya mbweni, Baba yake akaomba lifti kwa bwana mmoja alikuwa na gari ya Volkswagon, yule bwana akamuuliza nikupeleke wapi?
Ndipo Karume akasema nipeleke kwa Kawawa. Hivyo Karume na wanae wawili ndani ya Vokswagon mpaka getini kwa Kawawa.
Kufika pale, akajitambulisha, walinzi hawana taarifa zake, and by then who was Karume, walinzi wakomgomea kumfungulia. Ndipo akaomba kutuma ujumbe kwa Kawawa aliyekuwa ndani, ili atoe ruhusa waruhusiwe kuingia.
Kawawa kusikia Karume yupo nje, badala ya kutoa amri afunguliwe, alishuka moja kwa toka toka ndani ghorofani, akaja mpaka nje ya geti na kumpokea Karume yeye mwenyewe in person, walinzi kuona mpaka bosi kashuka, wasifungue milango wenyewe?.
Huo ndio ukawa mwanzo wa Amani kumuona Kawawa.
Kesho yake Juliasi akaja kuawatembelea hapo kwa Kawawa na jioni yake Karume akawaacha wanaye kwa Kawawa, yeye akarudi zake Zanzibar, huku nyuma watoto wakaenda shule, na yeye akaenda kutangazwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, hivyo wale wote wanaodai eti Karume aliyakimbia Mapinduzi, si wakweli, wanamsingizia tuu.
January mwaka jana tulipata bahati ya kuisikiliza simulizi ya Bi.Fatma Karume, ambaye ndiye Mama yake Amani. Bi. Fatma Karume akieleza Karume alikuwa wapi wakati wa Mapinduzi, Bi. Fatma alikuwa mkweli zaidi kwa kusema mumewe alijihifadhi mahali, kwa vile hakuwa na uhakika mapinduzi yatafanikiwa, mpaka alipopata uhakika, ndipo akajitokeza. Ikumbukwe iliyeongoza Mapinduzi yale ni Mganda Field Marshal John Okelo na ndie aliyetangaza Mapinduzi kwenye Redio ya Sauti ya Zanzibar alfajiri ya tarehe 12 January,1964.
Hivi jamani, inaingia akilini, nchi imepinduliwa usiku wa manane, na wewe alfajiri eti unahangaikia watoto warudi masomoni baada ya likizo, hivyo mnakosa usafiri, mnapanda mtumbwi, mnashukia Mbeni, mnaomba lifti ya Volkswagon ya watu, mnavamia kwa Kawawa, mnakataliwa kufunguliwa, hii ilikuwa kweli anaharakia watoto warudi masomoni au anakimbia Mapinduzi?
Januari 2, 2010 | Gawanyo
Makala
7 maoni Karume aliyakimbia mapinduzi?
-
mrfroasty
Januari 2, 2010 katika 5:14 um · Jibu
Akiwa aliyakimbia au hakuyakimbia, mie kama mzanzibari wa leo sioni umuhimu wowote.Ninachojua mie, Zanzibar ilipewa uhuru kama nchi nyengine zilizokuwa zimetawalia hapa barani Afrika.
Baada ya uhuru, gurupu fulani halikuridhishwa na waliokamata serekali wakaamua kutumia njia ya nguvu na vita kuindoa i.e Mapinduzi.
Kwa vile hilo gurupu lililopindua lilipata nguvu au hifadhi kutoka Tanganyika (hoja ya msingi ya kuundwa kwa mungano), imebidi hadi leo tuite Mapinduzi ndio uhuru wa kweli.
Lakini hakuna chochote Mapinduzi HAYAKUBALIKI kwenye ulimwengu wa demokrasia, hivyo Zanzibar haina budi kuyaweka kama ni historia na kuendelea kusherehekea uhuru wake wa 1963 kama ilivyo nchi nyengine yoyote iliokuwa koloni.
Huu ndio ufahamu wangu, mimi ni mzanzibari na kijana wa leo napenda kukabiliana na kila aina ya hoja.Lakini hoja hizi za kihistoria ni lazima viongozi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wakubali ukweli, kama mapinduzi sio jambo jema wala lakuomba.Huu ni uvunjwaji wa haki za kibinadamu!
Waliuliwa wote kwenye mapinduzi hayo ni wazanzibari waliopachikwa labels uarabu.Lakini amini usiamini, wafuasi hao waliopinduliwa ni wazanzibari na wengine hata rangi zao ni pure Afrikans au Zanzibaris.Si kweli kwamba Pemba nzima ina waarabu, wenye damu ya kiarabu ni chini ya 10%.Kuna sehemu Unguja pia ambazo zinadaiwa zilikuwa ndio hizo zilizokuwa na wafuasi wa serekali iliyopinduliwa, mfano Uzi, Bumbwini, Stone-Town…hizi sehemu zote hazina waarabu, kama wapo ni wachache kama sehemu zengine zozote za Zanzibar.
Nawakilisha…
-
Mwanambaya
Januari 2, 2010 katika 6:52 um · Jibu
HOJA ZAKO MRFROAST NI ZA MSINGI. NATHAMINI MICHANGO YAKO YENYE KUJENGA. UNAONEKANA NI MTU MJUVI. ENDELEA VIVYO HIVYO…
-
Mzenji
Januari 2, 2010 katika 8:32 um · Jibu
Mie simtetezi wa mapinduzi, ila uhuru wa Zanzibar hauwezi kuwa huo wa 1963 ukizingatia Sultan nae pia alikuwa mkoloni Zanzibar kama hao waingereza. Sasa utasemaje Zanzibar ilipata uhuru 1963 wakati Sultan bado alibaki kuwa ndie mtawama wa Zanzibar
-
mrfroasty
Januari 2, 2010 katika 9:33 um · Jibu
@Mzenji
Ni vyema kwa wazanzibari kuchukulia watu wenye jinsia zote wanaoishi visiwani humo kuwa ni wazanzibari.Kwa kutumia mtazamano wa kuwa Zanzibar kuna jinsia tofauti, waarabu, wahindi, wazungu na waafrika bila ya shaka Sultani nae alikuwa ni mzanzibari.Na huwezi kusema alikuwa mkoloni, kufanya hivyo ni kuonesha ubaguzi na chuki tuu.Ambayo itakubidi useme hadi leo mtu mwenye asili ya kihindi au kiarabu aliomo visiwani humo, hana haki ya kukamata madaraka.
Mie binafsi yangu sipendi mfumo wa kifalme, lakini wakati huo huo siwezi kuyatukuza mapinduzi.Yaliyotokea yametokea, lakini tusiseme kuwa mauaji ya 1964 yalikuwa halali….yametokezea tuu, kuna sehemu nyingi tuu yametokezea mauaji ikiwemo Ruanda, Burundi…hii yote ni mifano tuu ya athari za chuki na ukabila usiokuwa na maana.Na kwa Zanzibar, hakuna tofauti na nchi nyengine yoyote makabila ya watu tofauti yanaishi humo…watu wa dini tofauti wamo humo…kwa hiyo tukubali tuu, hata kama Raza akisema anagombea urais…basi tukubali kama ni mzanzibari madhali anaishi humo na raia wa humo…bila ya kutizama kama asili ya kihindi!!!
Sasa kama Raza tutamkubali, ni kwanini tusiwakubali hao wenye asili ya kiarabu kama ni wazanzibari????Kumbuka kuna nchi ambazo ni pure afrikans, nazo pia zina mifumo ya kifalme…kuna mfalme Mswati n.k…na joho linavaliwa hadi leo Zanzibar kwenye maharusi, tusije tukaanza kupandishiana chuki na kuvuana uzanzibari …ati mfalme alivaa joho, basi si mzanzibari ni mkoloni!!!
Sasa wazanzibari wote waliokuwa wakiishi visiwani humo nao walikuwa wakoloni?Maana utawala huo wa kifalme ulikuwa na support kubwa kutoka Pemba, Uzi, Stone-Town, Bumbwini, humu mote mulikuwa kumejaa wakoloni???Au waarabu???….tuacheni jamani haya mapinduzi tuyawekeni kama ni tukio lilitokezea, baada ya yote hayo hata tukisema lilikuwa tukio jema au baya haitusaidii chochote baada ya kupandiziana chuki baina ya waliondokewa na wapenzi wao kwenye familia zao.
Naamini kwa dhati kama kusherehekea uhuru wa 1963 ni jambo la busara katika kujenga maridhiano na ustahamilivu wa makabila yaliomo visiwani humo.
-
Ustadh Pengo
Januari 3, 2010 katika 5:19 mu · Jibu
Mimi nasema waarab na wahindi bado kupewa urais katika nchi za Kiafrika kama wao msimamo wao ni watu weusi (Waafrica) hawawezi kuwa na hata ukurugenzi katika nchi zao. Tutawakubali kama watanzania au wanzanzibar ndani ya hiyo Tanzania hao wahindi bado wanatubagua na hao warabu pia tunakuwa nao wanapokuwa na shida tu. mapinduzi wache tuyaite vile vile Mapinduzi kama ni mabadiliko tu. Si tunakuoneni watu wa kisiwa cha pili yaani Pemba mnapenda sana kuoa watu wenye asili ya kiarabu hala fu mnadhalilisha mbona wao hawapendi kuoa wafrika halisi , wangeonesha hayo madogo madogo basi tungesahau mapinduzi. Lakini wao ndio wenye kufanya sisi tuone mapinduzi ndio mkmbozi na itabi vile vile.
-
Mzenji
Januari 3, 2010 katika 6:20 mu · Jibu
Mrfroasty, sijasema kwamba huyo Jamshid si zanzibari, Mzanzibari kamili kama mimi na wew ila kwa nin tawala wa kizungu afrika ulikuwa wakikoloni ila wa kisultan ambao ulianzia 1840 usiwe ukoloni? Au hukusoma katika historia Zanzibar kulikuwa na tawala za jado kama usultan? Mapinduzi nakubali kwamba yana connotation mbaya sio Zanzibar tu ulimwengu mzima. Kila alipofanyika mapinduzi, basi kunaashiria kwamba demokrasia ilishindikana au kukiukwa na kupelekea watu chungu nzima wasionahatia yeyote kupoteza maisha.
Swala la ubaguzi halipo zanzibar tu, ulimwengu mzima karne na makarne watu wanabaguana ila huu ubaguzi wa rangi ndio bado culprit hadi leo hii, licha kwamba katika nchi ya marekani tumeona rais wa kwanza mwenye damu nyeusi ila hata huko bado ni tatizo sugu. Watu weupe wanaogoza zaidi kuwaona wenzao weusi inferior na hawana thamani sawa na wao. Sisi wazanzibari culture yetu imekuwa influenced sana na uarabu hadi, hata wale wazanzibari wenye damu kidogo sana ya uarabu basi kuna desturi ya kujiona bora kuliko weusi kabisa.
Waarabu zanzibar hawabaguliwi ila wanabagua, hakuna hata ishara ya kubaguliwa, ubaguzi wa upemba na uunguja ndio sumu, mimi ni mpemba mweusi sina babu wala bibi hata mmoja mwenye asili ya kiarabu ninaemjua ila katika serikali ya Zanzibar ntakuwa outcast sawa na mpemba mwengine mwenye damu ya kiarabu. Mimi sioni tatizo kwa Zanzibar kuwa na rais mwenye asili ya kiarabu au kihindi ilimradi aelewe kwamba yeye si rais wa wawahindi au waarabu bali wa Zanzibar.
Kuhusu suala la ndoa, siku zote mtu huoa mke anaependezewa nae, sasa sioni ajabu kwa mtu mweusi kuamua kuoa muarabu kama kapendezewa, na pia watu wengi wanafikia uamuzi huo ili kupata kizazi kilichochanganya ambapo watoto wataweza kukubalika kwenye jamii zote. Ila ulivosema Ustaadh Pengo ni kweli kwamba ndoa nyingi kati ya weusi na waarabu huwa ni mume mweusi tena mwenye uwezo, kuoa mke muarab na sio vice versa, hapa ndio maana nikasema kwamba waarabu Zanzibar hawabaguliwi ila wao ndio wabaguzi.
Nawasilisha.
-
Pasco
Januari 3, 2010 katika 9:22 mu · Jibu
Heshima Mbele wana Mzalendo Net.
Mimi ndie mwandishi wa habari hii, ni ustaarabu tuu wa kazi za maandishi, unapochukua habari fulani au kazi fulani bila idhini, unawajibika kutoa attribution ya source ‘kwa mujibu wa jamiiforums' ili kutoa haki ulikoipata.
Ni lengo la kila mtoa habari isambae kadri iwezekanavyo ila pia muitendee haki ilikopatikana.
Asante na endelezeni kazi nzuri kuhabarisha jamii.