Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,337
- 113,178
Kwanza tuendelee kupeana pole kwa Msiba wa Kawawa.
Leo amezikwa na apumzike kwa amani.
Ila pia msiba huu umefungua baadhi ya mambo ambayo hayakupata kujulikana kabla mongoni mwake ni haya...
Rais Karume akizungumza kwenye TBC, amekanusha ule uvumi wa Karume kuyakimbia Mapinduzi.
Akisimulia Rais Karume amesema mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika kwa muda wa saa 2 tuu, tangu saa 8:00 usiku mpaka saa10 alfajiri ya Jumamosi ya tarehe 11/01/1963 kuamkia Jumapili tarehe 12/01/1964.
Hivyo kulikucha salama usalmini.
Hivyo Jumapili hiyo, yeye Karume alikuwa na safari ya kuja Dar es Salaam ili awapeleke watoto wake, Amani na Ali shuleni Malawi (Kuna hoja iliwahi tolewa Karume ni Mnyasa wa Malawi, alikuja Zanzabar kama kuli Bandarini Zanzibar) hivyo watoto kumbe walisoma kwao?.
Karume akaendelea kusema kuwa hiyo Jumapili asubuhi, walitafuta usafiri wakakosa, hivyo wakasafiri na mtumbwi toka Zanzibar saa 7 mchana, wakafika Mbweni saa 11 jioni.
Waliposhuka pwani ya mbweni, Baba yake akaomba lifti kwa bwana mmoja alikuwa na gari ya Volkswagon, yule bwana akamuuliza nikupeleke wapi?.
Ndipo Karume akasema nipeleke kwa Kawawa. Hivyo Karume na wanae wawili ndani ya Vokswagon mpaka getini kwa Kawawa.
Kufika pale, akajitambulisha, walinzi hawana taarifa zake, and by then who was Karume, walinzi wakomgomea kumfungulia. Ndipo akaomba kutuma ujumbe kwa Kawawa aliyekuwa ndani, ili atoe ruhusa waruhusiwe kuingia.
Kawawa kusikia Karume yupo nje, badala ya kutoa amri afunguliwe, alishuka moja kwa toka toka ndani ghorofani, akaja mpaka nje ya geti na kumpokea Karume yeye mwenyewe in person, walinzi kuona mpaka bosi kashuka, wasifungue milango wenyewe?.
Huo ndio ukawa mwanzo wa Amani kumuona Kawawa.
Kesho yake Juliasi akaja kuawatembelea hapo kwa Kawawa na jioni yake Karume akawaacha wanaye kwa Kawawa, yeye akarudi zake Zanzibar, huku nyuma watoto wakaenda shule, na yeye akaenda kutangazwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, hivyo wale wote wanaodai eti Karume aliyakimbia Mapinduzi, si wakweli, wanamsingizia tuu.
My Stake, January mwaka jana nilipata bahati ya kuisikiliza simulizi ya Mjane wa Karume, ambaye ndiye Mama yake Amani, Bi. Fatma Karume akieleza Karume alikuwa wapi wakati wa Mapinduzi, Bi. Fatma alikuwa mkweli zaidi kwa kusema mumewe alijihifadhi mahali, kwa vile hakuwa na uhakika mapinduzi yatafanikiwa, mpaka alipopata uhakika, ndipo akajitokeza. Ikumbukwe iliyeongoza Mapinduzi yale ni Mganda Field Marshal John Okelo na ndie aliyetangaza Mapinduzi kwenye Redio ya Sauti ya Zanzibar alfajiri ya tarehe 12 January,1964.
Hivi jamani, does it really make sense, nchi imepinduliwa usiku wa manane, na wewe alfajiri eti unahangaikia watoto warudi shule baada ya likizo, hivyo mnakosa usafiri, mnapanda mtumbwi, mnashukia Mbeni, mnaomba lifti ya Volkswagon ya watu, mnavamia kwa Kawawa, mnakataliwa kufunguliwa, was it just for watoto Amani na Ali kurejea Shule Malawi?.
Huu ni uthibitisho mwingine jinsi Mzee Kawawa alivyokuwa mtu wa watu. Umati uliojitokeza tangu jana kwenye heshima za mwisho na leo kwenye mazishi, ni uthibitisho wa hili.
RIP Mzee RASHIDI MFAUME KAWAWA, SIMBA WA VITA, UPUMZIKE KWA AMANI.