Karimjee kumuaga Sumari

Karimjee kumuaga Sumari

Huyu marehemu alishawahi kumwambia Dr Slaa kama hana hoja nyingine zaidi ya Ufisadi wa EPA hakae kimya.
My take; huyu marehemu Sumari inaonesha ilikua ikimuhuma sana Dr Slaa kukomalia kashfa ya EPA, binafsi namuonahuyu marehemu ni fisadi tu wale wale.

kabisaaaaa mkuu ccm wengi mafisadi tu. Kwangu hata kuwa kwenye chama cha mafisadi huku ukijua na ukaamua kunyamaza tayari nawe unakua fisadi mtarajiwa ambaye unasubir upate nafasi upige deal.
 
Jibu langu lili-reflect statement yako...
Ilionesha mambo manne ama zaidi ndani yake:
1. JF ni ya chadema (membaz wa chadema). Hili uongozi wa jf ulishalikanusha tangu katibu mwenezi wa chama chenu alipotoa tuhuma kama hizo.
2. Memba wa jf huwa wanahudhuria kwenye misiba ya membaz wenzao tu (hata kama ni kweli sioni tatizo hapo)
3. Msiba ukiwa ni wa mwanachadema basi wanachadema lazima wahudhurie (hili pia sioni tatizo lake)
4. Ukiona watu maelfu kwa maelfu wamehudhuria msibani basi ujue kuwa aliyekufa ni mwanachadema.

Hiyo ya nne ndo iliyonifanya niamini kuwa kweli Dr. Slaa aliibiwa kura. Kama wanachadema wanaweza kujitokeza kwa wingi namna ile kwenye msiba ni wazi kuwa kwenye uchaguzi ni vivyo hivyo kwani nchi yetu sasa hivi ni kama ipo msibani, na kama umati huo wote una mapenzi na chadema ni aglabu watu hao wataichagua chadema. na kama wameichagua chadema halafu eti haikushinda...kura zimeenda wapi?

Na kwa kuwa nimeona mara nyingi ukiikejeli chadema na ukijiweka karibu na magamba, nakuchukulia kuwa wewe ni mmoja wao.

Kama wewe ni dereva wa taxi, majambazi watatu wakakukodi mkafanye uhalifu, askari wakiwatia mbaloni watasema tumekamata majambazi wanne.
Mkuu Mkeshaji, kama kipimo chako cha ushindi wa Chadema ni makundi ya watu, na kama unaamini makundi makubwa ya watu ndio kipimo cha wapiga kura wenu, then ile 1995 ni Mrema aliyeshinda maana yeye alivuta umati mkubwa hadi gari lake kusukumwa kila siku!, Hivyo vigezo hivyo vya umati wa watu ndio wingi wa kura wa ule umati watu kwenye mikutaö yenu na kujumlisha na zile kura zote za washangaa helicopter vikiwemo vile vitoto, then ni hakika alishinda!.

Hili la dereva-taxi na wote ni abiria wangu nalikubali na uthibitisho safi utapatikana 2015 maana nadhamiria kuacha biashara ya udereva sasa nataka kumiliki gari langu langu mwenyewe na sio la tajiri hivyo nitakuwa na nguvu ya kulichagulia abiria.
 
Back
Top Bottom