Karibu tushirikiane kuendesha NGO's

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,413
6,134
Wakuu habari za mida hii, poleni na mihangaiko ya kusaka mkate.

Sasa nijikite kwenye mada husika niko kwenye mkakati wa kusajili NGO'S kwa jili ya watoto yatima nina watoto ninaowahudumia kama 20 hivi sasa nilikuwa sijasajili nilikuwa nawahudumia mimi kama mimi sasa nimeona kuna umuhimu wa kuisajili ili niweze hata kuomba misaada baada ya kufuatilia nikaambiwa kuwa watu kama 5 hivi ambao ndiyo bodi halafu ndiyo isajiliwe hivyo ninaomba kama kuna mtu ana vision ya kuanzisha au anataka tushirikiane tuwe pamoja karibu sana ili tujue namna ya kufanya au anaye weza kuchangia mawazo, fedha, nguo, daftari nk maana hawa ni wanafunzi wote naomba tuwasiliane.

0758844240 karibuni wadau.
 
Mkuu unataka misaada Sema tu ili tuchangie, ila usije ukala michango yetu
Mkuu vyovyote itakavyo kuwa nitashukuru maana saivi shule zinafunga hivyo zikifungua mambo yanakuwa mengi nahitaji watu wa kushirikiana nao sana
 
Mkuu, Mungu akusaidie katika hili, maana sio wote wanasaidia kwa moyo, nasikia hata yule mama anaemiliki mashule na lile sinagogi vile vyote alivipata kwa njia ya kujifanya kusaidia, zile shule dhumuni lake ni kusaidia lkn kaulize ada ya pale, na nasikia wahisani wale wakija huwa wanaandaliwa baadhi ya watoto ili kudhibitisha kuwa ni kweli wanasaidiwa, lkn mkuu umeonyesha moyo, kama uliweza kuwahudumia mwaka mzima ama hakika una nia nzuri
 
- Andaa JINA la shirika.
1. Andaa Katiba (3 copies)
2. Muhtasari wa mkutano wa wanachama kupitisha hiyo Katiba kwaajili ya usajili. (miongoni mwa wanachama mchague Mwenyekiti, Katibu, na Mtunza Hazina)
3. Endorsement list ya wanachama wote. Yaani jina na saini.
4. CV na picha passport size mbili za kila Kiongozi. Wale viongozi watatu I.e M/Kiti, Katibu, na Treasurer (mtunza hazina).
5. Jaza Form maalumu ya usajili. (Form hii unaipata kwenye taasisi unayotaka kwenda kusajili au idownload kwenye website yao).
6. Barua ya approval kutoka kwa Afisa Maendeleo Jamii wa Kata. Yaani kwenye Kata husika ambapo mtaweka office ya shirika.
7. Barua ya approval kutoka kwa Afisa Maendeleo Jamii wa Wilaya. Yaani kwenye Wilaya husika ambayo mtaweka office ya shirika.
8. Ada ya usajili. Sikumbuki the exact amount, ila ni around Tsh 100,000 hivi kwa mwaka, for national/countrywide coverage.
9. Kisha pelekeni kwenye taasisi ya usajili.

N.B: Taasisi za usajili zipo kadhaa na kila moja ina sheria yake na requirements/taratibu zake. Kuna BRELA (under the Companies Act). Kuna Wizara ya Mambo ya Ndani (under the Societies Act). Kuna Wizara ya Maendeleo ya Jamii (under the NGOs Act). Pia kama sikosei kuna RITA (under the Bodies & Trustees Act).

So, hizo items hapo juu (1 to 8) ni registration requirements under The NGOs Act, at Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto. Pia ni vizuri zaidi mkaiangalia hiyo sheria (The NGOs Act) inapatikana online, just to get assured on the mentioned requirements for registration.
The registration under The NGOs Act, national coverage ni Tanzania Mainland only. Kwamba hamtaweza kufanya any project or activity in Zanzibar.

Wish you all the best of luck katika kuwahudumia hao watoto yatima. Mungu awabariki.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom