Karibu tujuzane viungo vya chai ya rangi

Hii ni nzuri zaidi na hata ladha yake
1. Vitunguu swaumu
2. Pilipili manga
3. Mdalasini
4. Mafuta ya alizeti
5. Vitunguu maji..

Kaaanga mpaka viive kabisa viwe vya brown...halafu mimina maji yako chai.acha ichemke sana. Hapo tayari kwa kunywa.
Hapo kwenye vitunguu swaumu mmmmmh! Chai pilau au MCHUZI mkuu
 
Ndi
Mkuu unapata chai nzuri yenyerangi ya dhahabu harufu ya kuvutia na kuifanya iwe tamu,
Ukipenda pia waweza tumia chai ya mbegu za parachichi
Hiyo chai ya mbegu za parachichi niliwahi kupewa Mwanza niliuliza chai ya nini mbona ladha siilewi? nikajibiwa daah! nusu nirudishe 'chenji'
Nikawaambia imenishinda.
 
Hiyo chai ya mbegu za parachichi niliwahi kupewa Mwanza niliuliza chai ya nini mbona ladha siilewi? nikajibiwa daah! nusu nirudishe 'chenji'
Nikawaambia imenishinda.
Pole mkuu hiyo Haikuandaliwa vema ikiandaliwa na mtaalamu ni chai nzuri mno
 
Karafuu+majani ya mparachichi
Tangawizi+Hiliki
Mdalasini + Tangawizi
Hiliki + Mdalasini+Mchaichai
Mchaichai + Mint+ mdalasini
Majani ya Mlonge+ Mchaichai + karafuu
Karafuu tupu
Mdalasini + pilipili manga
Majani ya limao+ majani ya mparachichi
Unga wa mbegu za parachichi + mdalasini
Hii ya majani ya mparachichi ndo naisikia leo.
 
1)Karafuu
2)kungu manga (Nutmeg)
3)hiliki
3)pilipili mtama/manga (black peper) kidogo tu
4)mdalasini

Unavikaanga ivo (dry roasting).

Vikipoa unasaga unaweka kwenye chupa.

Siku ukipika chai sasa.

Weka maji kwenye sufuria .
Para/twanga tangawizi.
Na zile spices ulizosaga tayari
Unachemsha

Chai ️ nzuri hii.

Cc THOMASS SANKARA.


Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana farkhina
 
Daaah!mchanganyiko wa "ankasus"wenyeji wa pwani (tanga,pemba,unguja)wanavijua vizuri hivi viungo.😋😋😋😋
 
Mie chai ya rangi niwekee mchai chai tu na hiliki kidogo na vitumbua kama saba hivi na mchuzi wa kuku mkata mitaa si yule anayependa kubweteka.

Habari zenu wapishi.
Naomba kufahamu jinsi ya kuandaa viungo vya chai ya rangi. Yaani niweke viungo pekee bila majani ya chai iwe tamu na kunukia vizuri.
 
Back
Top Bottom