Karibu Mkuu wa Mkoa, Said Meck Sadiki

Feb 26, 2014
52
46
Nakukaribisha mkuu wa mkoa mpya hapa Kilimanjaro.Tuna changamoto zetu kule Rombo za kupombeka lakini hapa mjini daladala(Hiace) zinazotoa huduma nyingi zilipaswa ziwe dampo au kufanywa vyuma chakavu.

Hakuna hata daladala moja inayofanya safari za humu mjini zinazo kuwa na tiketi sasa sijui hao SUMATRA kama wanalijua hili.
Karibu tu changamoto nyingine utajionea mwenyewe.
 
Hivi jamaa kuletwa Moshi itakuwa ni demotion ama promotion..Ishu ya Umeya itakula wengi mno...
 
Nakukaribisha mkuu wa mkoa mpya hapa Kilimanjaro.Tuna changamoto zetu kule Rombo za kupombeka lakini hapa mjini daladala(Hiace) zinazotoa huduma nyingi zilipaswa ziwe dampo au kufanywa vyuma chakavu.

Hakuna hata daladala moja inayofanya safari za humu mjini zinazo kuwa na tiketi sasa sijui hao SUMATRA kama wanalijua hili.
Karibu tu changamoto nyingine utajionea mwenyewe.
Lazima afanye kazi kweli kweli mjini kuruhusu gari chakavu ni hatari sana. Mji unachakaa kila siku na mabadiliko ni madogo mno japokuwa aliyepita alijaribu kurudisha nidhamu
 
Automatic demotion!Magu alitaka haki itendeke lakini Huyu jamaa akaonyesha upendeleo wa hali ya juu,sasa hapa moshi sijui kama ataziweza Hiace ya Majengo kwa Mtei,yaani zimeozA,zinaendeshwa na wanywa viroba wasokuwa na leseni na 80% zinamilikiwa na Ma-traffick na wale walio staafu ndio maana hazikamatwi,
 
Nakukaribisha mkuu wa mkoa mpya hapa Kilimanjaro.Tuna changamoto zetu kule Rombo za kupombeka lakini hapa mjini daladala(Hiace) zinazotoa huduma nyingi zilipaswa ziwe dampo au kufanywa vyuma chakavu.

Hakuna hata daladala moja inayofanya safari za humu mjini zinazo kuwa na tiketi sasa sijui hao SUMATRA kama wanalijua hili.
Karibu tu changamoto nyingine utajionea mwenyewe.
Mkuu mpya wa mkoa...Kilimanjaro sio mkoa mpya.
 
Mkuu anatakiwa apambane na kero zifuatazo mkoa wa kilimanjaro kama unywaji pombe uliokithiri, kamari, pool table, wizi watu wa bodaboda, ujambazi wa kutumia silaha/majambazi wasalimishe silaha.
 
Kilimanjaro ni mkoa rahisi sana kuongoza, watu wake wengi wameelimika kitambo na wana ustaatabu mzuri. Watu wake wamefuata sheria za mipango miji na ni nadra sana kukuta kesi za waliojenga kwenye hifadhi za barabara au migogoro ya ardhi kama sehemu nyingine.
Changamoto kubwa kwa viongozi wapya ni kubuni njia mpya za kuboresha uchumi wa mkoa uweze kukua na kutoa ajira za kutosha.
 
Sadik anachotakiwa kufahamu Kilimanjaro chama chake cha CCM Ni cha upinzani,atambue hili na aache undava wake wa Dar
 
Mwenyekiti wa ulinzi na usalama mkoa.kaa na kamanda wa polisi mkoa mpange vikosi vyakufanya kazi kwa uaminifu.askariwengi mkoani klm haswa wanaokuwa kwenye hayo madefender yao wanashirikiana na majambazi wauza mirungi bangi na gongo.wengine ni wala mirungi.pambana na hilo pia katika kusafisha mkoa huo wa klm
 
Karibu sana ktk mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick. Mkoa huu una changamoto nyingi, japo si mkoa mkubwa sana kama Dar.
Kwa sasa mkoa wa Kilimanjaro na hasa mjini Moshi na viunga vyake hasa zile za KCMC, Rau, Njiapanda na Kariwa kuna tatizo kubwa la maji. Kwa sasa ndoo ya maji imefikia shs 1000 na hata kwa bei hiyo maji yamekuwa hayapatikani.
Wakuu wanaopaswa kushughulikia tatizo la maji katika mkoa huu wamekuwa ni wazembw sana..na hata hawatoi taarifa pindi maji yanapokatika, tena kwa kipindi kirefu. Ni aibu na fedheha kubwa kwa wakazi mkoa Kilimanjaro hususan maeneo tajwa kulilia tatizo la maji wakati kuna vyanzo vingi vya maji.
Naomba Mhe Sadick aanzie hapo...amalize tatizo hili. Ni aibu kubwa sana...
 
Back
Top Bottom