Madiwani wa CHADEMA wilayani Hai wasusa kuhudhuria kikao cha mkuu wa mkoa Said Meck Sadiki

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375



Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Helga Mchomvu, wamesusa kuhudhuria kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki wakati akizungumza na viongozi wa vitongoji, vijiji, kata, viongozi wa taasisi za serikali na dini.

Sadiki alifika wilayani Hai jana, ikiwa ni moja ya ziara zake katika wilaya zote za Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kujitambulisha pamoja na kuzungumza na viongozi mbalimbali wanaowakilisha wananchi, pamoja na kusikiliza kero zinazozikabili wilaya hizo.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Usharika wa Hai Mjini, madiwani hao ambao wote ni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hawakuonekana hata mmoja huku eneo walilokuwa wameandaliwa likibaki na viti vilivyo wazi.
Awali, Mkuu wa Mkoa alipowasili ofisini kwa Mkuu wa Wilaya kwa lengo la kupokea taarifa ya wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mchomvu aliwasili kwa kuchelewa na muda ulipofika wa kuelekea ukumbini, alitokomea kusikojulikana.

Hali hiyo ilimshangaza Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa ambaye alisema siasa ziliisha baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana, lakini inashangaza kwenye masuala ya maendeleo ya wananchi bado viongozi wanaendelea kuziendekeza.
Byakanwa alisema, licha ya madiwani wote 17 wanaounda Baraza la Madiwani Wilaya ya Hai kuwa ni wa Chadema, bado wanasimamia na kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambacho ndicho chama kilichopewa ridhaa na Watanzania kuongoza kwa awamu nyingine ya tano.
“Ni jambo la kushangaza kuona viongozi waliochaguliwa na wananchi wanashindwa kuwakilisha wananchi wao katika kupeleka na kuzisemea kero zao mbalimbali zinazowakabili, na badala yake wamekuwa wakisusa vikao vya kupanga maendeleo. Kwa siasa hizi wananchi hawawezi kupata maendeleo,” alisema Byakanwa.

Akiwasilisha taarifa za kutofika kwa madiwani hao, Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Hai, Rosemary Kuringe alisema, amewasiliana na madiwani wake na kuelezwa kuwa hawakupata taarifa za ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa.

Akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na viongozi mbalimbali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Saidi Mderu alikiri kutoa taarifa kwa madiwani wote katika kikao cha Baraza Maalumu la Madiwani kilichofanyika Aprili 22, mwaka huu.
“Kwa suala hili la viongozi hawa kususa, namwachia Mungu, niliwapa taarifa madiwani wote tena nilisisitiza, cha kushangaza wakati Mkuu wa Mkoa amewasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri alifika akiwa amechelewa lakini wakati tumekuja kwenye ukumbi hatukumuona,” alisema Mderu.

Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akizungumza katika kikao hicho.

Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Hai,Said Mderu akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa katika kikao hicho.


Chanzo: MPEKUZI
 
Huku ni Hai.....tulikuwua busy na Kushughulikia tatizo la mafuriko...upuz wa kutambulishana ,hautuhusu.....nan asiye mjua said ....
 
Huku ni Hai.....tulikuwua busy na Kushughulikia tatizo la mafuriko...upuz wa kutambulishana ,hautuhusu.....nan asiye mjua said ....
Lakini si jambo la kiungwana mgeni anakuja nyumbani kwako unaenda kujificha. Hii ni aibu ya mwaka
 
hili neno hupenda sana kutumiwa na watoto wa kike... Imekuaje mkuu?
Atakuwa amechanganyikiwa huyo. Kodi ya nyumba imeisha muda wake na anapaswa kulipa pango la mwaka mzima ifikapo kesho. Ndo maana kachanganyikiwa
 
Hivi hawa sio ndio moja ya wilaya zilizopata hati chafu za CAG?
Ni hao hao Mkuu. Mkuu wa Mkoa alitaka kukutana nao na kupeana mikakati ya kuondoa tatizo la hati chafu matokeo yake wamesusa
 
Ni hao hao Mkuu. Mkuu wa wilaya alitaka kukutana nao na kupeana mikakati ya kuondoa tatizo la hati chafu matokeo yake wamesusa
Hiyo ipo wazi kua walikua wanakimbia vivuli vyao vya ufisadi, aibu kubwa kwa ukawa kufuga wezi...
 
huyo ajitambulishe asijitambulishe huyo ndio mkuu wa mkoa wao..waende wakatathmini athari za wahanga huko watu saba wamekufa kwa kudondokewa na nyumba...
 
Hiyo ipo wazi kua walikua wanakimbia vivuli vyao vya ufisadi, aibu kubwa kwa ukawa kufuga wezi...
Nina mashaka na utendaji wa hilo Baraza la Madiwani. Madiwani wote ni wa CHADEMA na bado wamepata hati chafu. Aibu sana hii
 
Nini kilichokuwa kijadailiwa hapo kama sio propaganda zile zile za uongo mtupu,unafiki na ahadi hewa.Watu walikuwa field wanawahudumia wananchi waliokumbwa na mafuriko,wengine wanaleta swaga za kutambulishana.So what???
 
Hivi hawa sio ndio moja ya wilaya zilizopata hati chafu za CAG?
Sasa kwani vocha za malipo, na cheki zinaandaliwa na madiwani? Si ni huyo mkurugenzi ambaye badala ya kwenda kufanya kazi anapoteza muda na utambulisho. Nani hamjui nani?
 
Nini kilichokuwa kijadailiwa hapo kama sio propaganda zile zile za uongo mtupu,unafiki na ahadi hewa.Watu walikuwa field wanawahudumia wananchi waliokumbwa na mafuriko,wengine wanaleta swaga za kutambulishana.So what???
Mkuu, umezijua sababu za wao kutohudhuria kikao hicho? Wamesema kuwa hawakupewa mwaliko. Hiyo sababu unayotoa ya kwenda kuwasaidia wahanga si sababu ya wao kususa kuhudhuria kikao hicho. Hata Mkurugenzi amekiri kuwa aliwapa mwaliko na amemwachia Mungu juu ya hilo
 
Sasa kwani vocha za malipo, na cheki zinaandaliwa na madiwani? Si ni huyo mkurugenzi ambaye badala ya kwenda kufanya kazi anapoteza muda na utambulisho. Nani hamjui nani?
Kaka Salama? Mbona umekuwa mbogo asubuhi hii? au na wewe unadaiwa pango la chumba kama mwenzako Petro Mselewa?
 
Hao madiwani wana uelewa wa hali ya juu sana wakatambulishwe kwa wananchi walio wachagua? Wangewachaguaje kma hawawajui? Au wakampokee mkuu wa mkoa aliefeli Dar akatupwa Kilimanjaro kwani wao ndio wa kuongozwa na viongozi walioshindwa kazi? Acha wakakae wenyewe huko madiwani wako kwenye kata kufanya kazi waliyotumwa na wananchi.
 
Back
Top Bottom