Mbezi/Kimara: Usafiri wa mwendokasi karaha tupu

Mbusule

Member
Aug 2, 2011
87
83
MWENDOKASI MBEZI - KIMARA KARAHA TUPU

• Mfumo wa Kadi Waondolewa kwenye Magari
• Kadi zawa Lulu, Bei yake Kufuru
• Abiria warundikana Vituoni wakisubiri kupata Risti

Na Mbusule C. Shillu,
Usafiri wa Mwendokasi umekuwa Kero kwa Wakazi wa maeneo ya Mbezi ya Kimara na maeneo ya jirani kutokana na kujikita katika kufanya biashara badala ya huduma. Lengo lao ni kutengeneza faida kubwa zaidi (Super Profit) kuliko kuondoa Kero ya Usafiri kwa Abiria.

Mara tu baada ya Usafiri huu kuzinduliwa, ulianzishwa Mfumo wa Kadi ambazo ziliuzwa Tshs. 500 tu na abiria angeweka Salio la Nauli anayotaka ingawa kiasi cha juu (kikomo) ilikuwa Tshs. 30,000/- ambayo mtu angeitumia kwa muda mrefu kusafiri.
Nauli kwa kadi kutoka Mbezi kwenda Posta, Ubungo, Kariakoo, Kinondoni na kwingineko baada ya Kimara ikawa Tshs. 800/- tu na inaendelea mpaka sasa.

Hata hivyo, mfumo wa Risti uliendelea sambamba na mfumo wa Kadi kwa maelezo kuwa ulikuwa wa muda mfupi tu wakati abiria wakiendelea kukata Kadi. Risti kutoka Mbezi kwenda Kimara ikawa Tshs. 400/- na kutoka Kimara kwenda Kariakoo, Kivukoni, Morocco, Ubungo, Magomeni na kwingineko kuelekea Mjini ikawa Tshs. 650/- kwa route. Na kwa mantiki hiyo kufanya nauli ya route moja kutoka Mbezi kwenda Mjini kuwa Tshs. 1050/- ukiachilia mbali usumbufu wa kupanga foleni kukata Risti na kupoteza muda mrefu kusubiri gari.
Ghafla Kadi ziliadimika na hazijawahi kutolewa tena mpaka sasa na mbaya zaidi hivi karibuni Magari mengi ya kutoka Mbezi yameondolewa Mashine za kutumia Kadi kwa kile kinachoonekana wazi kuwa wanataka faida kubwa zaidi (Super Profit); yaani kupata Tshs. 1,050/- badala ya 800/-

Kutokana na "Vyuma Kukaza", biashara ya Kadi imepamba moto miongoni mwa abiria ambapo abiria mwenye Kadi anamuuzia Mhitaji kwa bei anayoona inafaa. Leo nimemshuhudia abiria akinunua kadi kwa Tshs. 50,000/- tena isiyo na Salio.

Changamoto zingine za Mfumo huu ni pamoja na;
1. Magari kuchelewa kufika Vituoni na hivyo kupelekea abiria kupoteza Muda mwingi wakingoja Gari. Hii inatokana haswa na Magari mengi kubaki "Depot" (Parking) ilhali uhitaji ni mkubwa vituoni.
2. Magari kujaza kupita kiasi hali inayopelekea abiria hasa wafupi kukosa hewa. Juzi nimemshuhudia Mmama akianguka kwa kukosa hewa. Bahati nzuri, dereva alikuwa mwelewa, akasimamisha gari na kwenda dukani kumtafutia Maji ya kunywa. Abiria walisikika wakisema, "Tutakufa" na walishuka Kituo kilichofuata nikiwemo mimi ingawa nilikuwa sijafika.
3. Kugoma mara kwa mara kwa Mfumo wa Mashine Vituoni. Mfumo wa kuongeza Salio kwenye Kadi mara nyingi hugoma na hivyo kumlazimu abiria kukata Risti.
4. Kukosekana kwa Uongozi. Abiria akiwa na kero Kituoni, hakuna namna ya kuiwasilisha kwa wakati ikafanyiwa kazi. Wafanyakazi waliopo Vituoni hawana majibu ya Kero za abiria.

Nini kifanyike?
1. Kuwe na Kampuni shindanishi la Usafiri. Hii itaongeza uwajibikaji na ufanisi kwa kuwa watajua wakizembea "watapigwa bao" na Mshindani wao. Mfano Mzuri ni kabla ya daladala za kawaida kuzuiliwa, Kadi zilitolewa na ufanisi ulikuwa juu.
2. Kuwepo kwa usimamizi wa Karibu kutoka Serikalini na hasa Sumatra kuhusu Bei, Ufanisi na Upatikanaji wa Kadi.
3. Mamlaka husika ziwe na utaratibu wa Ziara za Mara kwa Mara Vituoni ikiwa ni pamoja na kuhoji abiria.
4. Pawepo na Uongozi wa Kampuni lenyewe unaozungukia Vituo vya Usafiri na kufanyia Kazi Kero za Abiria ikiwa ni pamoja na Mfumo wa Kadi.

Hitimisho;
Mfumo huu wa Usafiri Ukiboreshwa na kusimamiwa vizuri ni mzuri sana na utastarabisha Jiji letu la Dar es Salaam. Lakini ukiendelea kuzorota kama ilivyo sasa, si tu utaumiza abiria lakini pia utakuwa fedheha kwetu na kwa wageni kutoka Mataifa mengine kwa kuwa Dar es Salaam ni USO wa Nchi yetu.

Mbusule Christopher Shillu
FB_IMG_1521094120473.jpg
FB_IMG_1521094138536.jpg
FB_IMG_1521094090580.jpg
 
Nashindwa kuelewa ukifika kariakooo gerezani na kivukoni yamejazana magari lakini hayachukui abiria ukiiuliza wanakwambia wanaondoka kwa shifts, sasa nashindwa kuelewa
Au mpaka aje Mkaburu ndio aoongoze mradi
 
Mwendo kasi kero sana wasimamizi wanacho jua ni kupunguza magari na kuyachelewesha ili mlundikane wengi akiachia gari mgombanie hakuna afadhali iwe mcha jioni asubuhi abiria wanajazana kama mizigo
 
Duuh! Mimi nakerwa zaidi na kuishiwa mara kwa na ticket, abiria wanaopandia Kibo ni mashahidi wazuri wa hili, hichi kituo kila siku asubuhi ticket hazitoshi, usimamizi mbovu na baadhi ya wafanyakazi lugha zao siyo nzuri. Inatakiwa waelimishwe zaidi kuwa kazi wanayoifanya ni huduma na siyo kutengeneza faidi na kutoa lugha mbaya kwa wateja wao.
Upande wa madereva naona wamefunzwa vizuri, wengi wa madereva kwenye haya magari wana lugha nzuri na kutumia utu, lakini wakata ticket siyo.
 
Tutaseeema weee mabadiliko hakuna.Tatizo mradi tumewapa watani zangu nao ni wageni wa mji.Kwao ni bora wakakaa nayo ofisini ili wayashangae vizuri kuliko magari hayo kuwa barabarani.Huyu wa magogoni tu mambo msobwemsobwe sembuse hao wa mwendokasi?Watani zangu hawa bure kabisa.Usafirishaji ni taaluma kama zingine sasa sisi tulipoona wanachunga ng'ombe tukadhani mwendo kasi wataweza wapi!!Mchunga ng'ombe hatabiriki hata kidogo.Tumejitakia.Hawa wanyang'anywe mradi haraka kabla hawajaharibu zaidi.Iundwe timu ya wataalamu wa usafirishaji watujengee mfumo madhubuti wa usafiri.Watani zangu wanachojua ni kuswaga ng'ombe tu,mkijazana pale na kuanza kusukumana kama ng'ombe wanakumbuka mbaaaali huko Sangamwalugesha.
 
Back
Top Bottom