Hiyo sio kweli, nenda kamchunguze mkinga uone anaamka saa ngapi kufungua biashara na anafunga saa ngapi na anawahudumiaje wateja wake. Chunguza matumizi yake na anakula nini na kiasi gani kwa siku. Mchunguze uone kama ana roho nzuri ya kusaidia ndugu zake na kunywa pombe na starehe nyingine za wanawake, chunguza kama anafiwa uone kama anafiwa na kuhudhuria misiba Kila siku, nenda kaone namna anavyoongea na mteja wake na usafi wa bidhaa yake, hakuna uchawi kaka anajilipua TU na kufuata misingi ya biashara. Wewe Kila siku uko kipalang'anda kuzika mjomba mara kaka yake mdogo mkazamjomba mara rafiki yake wa utotoni mdogo wake bibi Yako.
Biashara ni mapato na matumizi