Kardinali Pengo, Simama au na wewe staafu kama yamekuzidi...

Kardinali Pengo, Simama au na wewe staafu kama yamekuzidi...

kaka upo nchi gani? Serikali dhalimu ya Tanzania imeridhia mauaji ya padri leo asubuhi zanzibar Kwa risasi ya kichwa na zeezi limekamilika. Wiki kadhaa pia iliridhia mauaji ya fr ambrose.. Bado yupo hospitali. Tunamtaka Pengo atoe tamko, tuingie barabarani au magogoni.

Hizi kauli zako na Mwanakijiji ndio zinataka kuchochea vurugu zaidi. Fahamuni tu kuwa kwenye vurugu za kidini hata siku moja hakuna mshindi.
 
Alikuwepo Askofu Mkuu Oscar Romero; alisimama dhidi ya utawala wa kidikteta na akatoa ujumbe wa kinabii (prophetic message). Alifanya hivyo baada ya mapadre wake kuuawa na utawala dhalimu. Pengo amezoea kukaa katika starehe mno, kula na kunywa na wakubwa na ameacha kusimama kama nabii. Anapenda heshima. Wakati umefika kwa Pengo kuonesha kuwa anastahili cheo alichonacho.

Tunahitaji Oscar Romero wetu... vinginevyo huku tunakokwenda kubaya. Oooh ninavyoogopa kusikia Shehe kauawa; Msidhani haiwezi kutokea au kwamba hawa Wakristu ambao ndani ya wiki moja viongozi wao wawili wameuawa nao wataendelea kukaa kimya..

Pengo... utafanya nini....

ni rahisi sana kuwachonganisha watu weusi kwa kuwa huwa hawapati muda wa kutafakari kwa kina nani chanzo cha mogoro wao....haya na nyinyi lipizeni kisasi kwa kuwaua masheikh , kisha NATO waje kuweka kambi mtwara kulinda amani yenu!...unafikiri wataweka kambi wapi?
 
Alikuwepo Askofu Mkuu Oscar Romero; alisimama dhidi ya utawala wa kidikteta na akatoa ujumbe wa kinabii (prophetic message). Alifanya hivyo baada ya mapadre wake kuuawa na utawala dhalimu. Pengo amezoea kukaa katika starehe mno, kula na kunywa na wakubwa na ameacha kusimama kama nabii. Anapenda heshima. Wakati umefika kwa Pengo kuonesha kuwa anastahili cheo alichonacho.

Tunahitaji Oscar Romero wetu... vinginevyo huku tunakokwenda kubaya. Oooh ninavyoogopa kusikia Shehe kauawa; Msidhani haiwezi kutokea au kwamba hawa Wakristu ambao ndani ya wiki moja viongozi wao wawili wameuawa nao wataendelea kukaa kimya..

Pengo... utafanya nini....

188749_517616428260540_705215873_n.jpg
 
haya ni matokea ya utawala ulipo kwani imepandikiza dhambi ya udini baina ya waislamu na wakristo.unaposema chama fulani ni cha kidini au cha kikanda maana yake unawafanya watu wachukiane wenyewe na si vyama vyao.ukiangalia matukio ya zanzibar utapata picha hii mapadre ni wa kanisa katoliki na wote ubini wao ni wakaskazini.labda ungetaka kwa nafasi yake PEngo afanye nn?
 
Kama serikali imeshindwa kuwapata wahalifu basi wawaachie wakatoliki hiyo kazi. Naamini kanisa katoliki lna makachero wa kutosha kupembua kujua muhusika ni nani na hata kumtia mikononi...just my guess!
 
Walipofuatwa Waislamu msikitini na kuwawaa pale Mwembechai, Mtukufu Pengo alitoa tamko kuwa wale waliuwawaa ni wahuni, hakujua anachokipanda na PHD zake za Theolojia

Leo mmeanza kuona kumbe Waumini wenu wakiuwawa inaumaaa eenh ? Mkuki kwa Noah.....

Akili gani hii!! Padri kafa akiandamana kwa walivyoandama Mwembe chai?....
Yule kureshi alharibu sana akili zenu....!
 
Ni kweli hatuuoni msimamo wa Pengo kama mkuu wa Kanisa Katoliki Tz. Anaonekana dhaifu kama Kikwete alivyo dhaifu kwa serikali ya Tz.
 
Mauaji ya padri ni kitendo cha kinyama kinachostahili kufanyiwa uchunguzi na wale wote watakaopatina na hatia ni lazima wachukuliwe hatua kali. Kadinali pengo ni kiongozi mwenye busara ya hali ya juu, anajua nini cha kufanya na anatambua kuwa kuchochea vurugu zaidi siyo utatuzi wa tabia hii ya kighaidi inayofanywa huko Zanzibar.
 
Alikuwepo Askofu Mkuu Oscar Romero; alisimama dhidi ya utawala wa kidikteta na akatoa ujumbe wa kinabii (prophetic message). Alifanya hivyo baada ya mapadre wake kuuawa na utawala dhalimu. Pengo amezoea kukaa katika starehe mno, kula na kunywa na wakubwa na ameacha kusimama kama nabii. Anapenda heshima. Wakati umefika kwa Pengo kuonesha kuwa anastahili cheo alichonacho.Tunahitaji Oscar Romero wetu... vinginevyo huku tunakokwenda kubaya. Oooh ninavyoogopa kusikia Shehe kauawa; Msidhani haiwezi kutokea au kwamba hawa Wakristu ambao ndani ya wiki moja viongozi wao wawili wameuawa nao wataendelea kukaa kimya.. Pengo... utafanya nini....
Huo ushauri haufai hata kidogo ni sawa na kumwaga petroli kwenye moto. Silaha ya mkristo ni sala kisasi kingine mungu ndo anajua
 
Kweli! Something has to be done. Ila tumefika hapa tulipo kutokana na mafundisho tunayoyapata katika nyumba za ibada. Wahubiri/Mashehe badala watangaze mazuri ya dini zao wao wanatumia muda mwingi kusema dini zenye msimamo kinyume na wao. Kila dini inajiona bora kuliko nyingine. Hali ni mbaya zaidi kwa wenzetu wa kiislamu, kwa kweli wanakosa uvumilivu. Huwa napenda kusikiliza radio Imani na haya yanayotokea ni reflection ya ninachokisikia. Huwezi amini radio ni ya waislamu lakini huenda wanataja ukristo mara nyingi kuliko wanavyotaja uislamu! Mpaka nikajiuliza, hivi kama serikli ilifungia gazeti la mwanaHalisi kwa sababu za uchochezi (kama wasemavyo), serikali hiyo inasubiri nini kuifungia radio imani kwa sababu hizo hizo?

Nina uhakika angelikuwa Shehe kauwawa hapa, sasa hivi pengine tungekuwa tunazungumza mengine.
Vitendo hivi vinapaswa kukemewa na watanzania wote.

Haaaaah haaaaah ! Kwahiyo Radio Imaan ndio imemuuwa Padre Mushi huko Zanzibar
 
Mbona huyu Ndg hayupo nchini hata ikitokea vurugu ana hasara gani?
 
Kama serikali imeshindwa kuwapata wahalifu basi wawaachie wakatoliki hiyo kazi. Naamini kanisa katoliki lna makachero wa kutosha kupembua kujua muhusika ni nani na hata kumtia mikononi...just my guess!

Hii ni sahihi kabisa. Nashindwa kuelewa kisiwa kidogo kama Zanzibar wanashindwa vipi kuwakamata maghaidi hao. Wakishirikisha makachero wa kanisa itakuwa njia muafaka.
 
We mzee umechoka matukio mangapi ya uhalifu wa silaha yametokea zanzibar?
 
Hizi kauli zako na Mwanakijiji ndio zinataka kuchochea vurugu zaidi. Fahamuni tu kuwa kwenye vurugu za kidini hata siku moja hakuna mshindi.

tukiondoa serikali dhaifu na dhalimu. Tukaendesha nchi kwa law and order ya kweli. Hakutakuwa na vurugu za kidini kama huko awali. Jiunge nasi tufanye mapinduzi ya kweli yatakayoleta tija na amani ya kweli kwa watanzania wa imani zote.
 
Hii ni sahihi kabisa. Nashindwa kuelewa kisiwa kidogo kama Zanzibar wanashindwa vipi kuwakamata maghaidi hao. Wakishirikisha makachero wa kanisa itakuwa njia muafaka.
Wawapeleke vijana wa pale Mabibo watamaliza kila kitu ndani ya muda mfupi...Hii sasa ni too much! wakati mwingne hata huenda hajatoka hospitali wameua na mwingine...hii ni fedheha kwa tanzania!
 
ZeMarcopolo vipi hapo Chadema wanawezakuhusika na tukio hilo, na vipi wake zenu CUF nao. Ninachoogopa mimi serikali ya Magamba itasema polisi bado wanafanya uchunguzi na kesi itaishia juu juu tu. Hakuna hatua zozote zitakazochukuliwa
 
Alikuwepo Askofu Mkuu Oscar Romero; alisimama dhidi ya utawala wa kidikteta na akatoa ujumbe wa kinabii (prophetic message). Alifanya hivyo baada ya mapadre wake kuuawa na utawala dhalimu. Pengo amezoea kukaa katika starehe mno, kula na kunywa na wakubwa na ameacha kusimama kama nabii. Anapenda heshima. Wakati umefika kwa Pengo kuonesha kuwa anastahili cheo alichonacho.

Tunahitaji Oscar Romero wetu... vinginevyo huku tunakokwenda kubaya. Oooh ninavyoogopa kusikia Shehe kauawa; Msidhani haiwezi kutokea au kwamba hawa Wakristu ambao ndani ya wiki moja viongozi wao wawili wameuawa nao wataendelea kukaa kimya..

Pengo... utafanya nini....

Unafikiri unaweza kumshawishi Pengo kama ulivyojaribu kwa Ulimboka?
 
Alipopigwa risasi padri kule ZNZ serikali ikasema "itachukua hatua kali kwa waliohusika kwenye tukio lile";Walipochoma nyumba za mawaziri kule Mtwara serikali ikasema "tutachukua hatua kali na kuwafikisha mahakamani wote waliohusika";Alipouawa mchungaji wa kanisa kule Geita serikali ikasema "tutachukua hatua kali kuwafikisha mahakamani wote waliohusika" HATA HUYU PADRI ALIYE UAWA ZNZ LEO serikali itasema "tutawasaka na kuwafikisha mahakamani wote walio husika"!Neno"tuta"ndiyo linaiongoza serikali ya TZ

Tumechoka maneno sasa tunataka vitendo;ZNZ ingedhibitiwa mapema udini usingekuwa wa kutisha kama huu!Watu wanaosambaza vipeperushi vinavyosema "wakristo ondokeni ZNZ" wanajulikana lkn hawakamatwi!

Udini,ukabila na ukanda uliangamiza nchi nyingi sana duniani!Serikali chukueni hatua sasa na acheni kabisa kauli zenu kuwa"tutawakamata"bali tunataka kusikia"tumewakamata"
 
Kwa kuwa Serikali ya CCM haiwezi tena kulinda hata watumishi na hasa wakristo namsaidia Pengo kutoa tamko .It is timr Wakristo kuandamana Nchi Nzima kwa amani .Ibada zifanyike kwenye viwanja vya wazi mwa madhehebu yote ikiwa ni ishara ya kuiambia Dunia kwamba Tanzania si salama tena .Na ulinzi wa raia na mali sasa hakuna .Iwe hatua ya kwanza na baadaye nitawatangazia cha kufanya baada ya hapo .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom