Kardinali Pengo asema bado kuna akina Herode uchwara duniani!

Akisema Herode pia ndiye Yule aliyemuua YOHANA MBATIZAJI baada ya kumueleza ukweli mfalme HERODE????
JE WANA UHUSIANO AU HUYU NI HERODE MWINGINE ANAYEMAANISHWA KATIKA MAHUBIRI HAYA??

AMA KWELI BIBLE NI MPYA KILA SIKU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Ndiyo maana nasema kumlinganisha msomi wa theology kama Pengo na Kakobe kwadababu kawafurahisha ama kasema kile watu wanataka kukisikia bila kuweka uwiano na siku yenyewe ni kutokujua.
Pengo ni mtu makini sana katika homily zake.
Herodi mambo Leo atubu full stop
 
Siamini kuwa kuna nchi yenye demokrasia ya kweli ,haki na kufuata utawala wa sheria halafu ikawa na vita na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe.

Machafuko na vita za wenyewe kwa wenyewe zinztokana na kukosekana kwa demokrasia , kupuuza maoni ya watu, kuvuruga chaguzi halali zilizoko kisheria , upendeleo na ubaguzi.
 
Akisema Herode pia ndiye Yule aliyemuua YOHANA MBATIZAJI baada ya kumueleza ukweli mfalme HERODE????
JE WANA UHUSIANO AU HUYU NI HERODE MWINGINE ANAYEMAANISHWA KATIKA MAHUBIRI HAYA??

AMA KWELI BIBLE NI MPYA KILA SIKU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
naona umetumwa kuanzisha hoja za kidini na si vyema sana kukashifu vitabu vitakatifu ukitaka kuelewa vzur usome na historia ya watawala wa kipindi hicho sio unaongea bila fact..
Familia ya Herode Mkuu
Mke Watoto

Doride
  • Antipatro, alifariki 4 KK
Mariamne I
  • Aleksanda, alifariki 7 KK
  • Aristobulo, alifariki 7 KK
  • Salampsio
  • Cypro
Mariamne II
  • Herode II, alifariki 6
  • Herode Filipo
Malthace
  • Arkelao, mfalme mdogo wa Yudea
  • Herode Antipa, mfalme mdogo wa Galilaya
  • Olimpia
Kleopatra wa Yerusalemu
  • Herode Filipo II, mfalme mdogo wa Perea
  • Herode
Pallade
  • Fasaele
Fedra
  • Rossane
Elpide
  • Salome
herode mkuu ndo alikuwepo kipindi yesu anazaliwa na ndio aliyeleta maafa ila herode antipa ndo mfalme wa galilaya aliyemtesa na kumkata kichwa yohana mbatizaji na hakuwa na tabia sawa na za baba ake huu ulikuwa n koo ya kifalme so walitawala kina herode wengi
 
Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Tanzania kama sehemu ya utamaduni wake, Alhamisi tarehe 28 Desemba 2017 ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa la Parokia ya Msimbazi, kwa ajili ya Watoto wa Utoto Mtakatifu Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Maandiko Matakatifu yanasema kwamba, sauti ilisikiwa Rama, kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako!

Mfalme Herode alisababisha maafa na msiba mkubwa; kilio na majonzi kwa watu wake. Aliwauwa watoto ili kulinda na kudumisha Ufalme wake. Alihofia uwepo wa Kristo Yesu, akamtafuta kwa udi na uvumba, lakini hakufanikiwa kumpata.


Kardinali Pengo anaendelea kufafanua kwamba, katika tukio hili, Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu wanaonesha jinsi ambavyo walijitahidi kutekeleza mapenzi ya Mungu katika maisha yao, wakajisadaka kwa ajili ya usalama na tunza ya mtoto wao mchanga kiasi hata cha kukimbilia uhamishoni Misri.

Kwa upande mwingine, kuna Mfalme Herode aliyezua msiba mkubwa, mateso na huzuni, kwa kuwatoa watoto kafara ili aweze kutawala.

Anasema, hata leo hii, bado akina Herode wamo katika ulimwengu mamboleo. Hawa ni baa la njaa, umaskini na ujinga. Kuna watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kwa vile tu ni watoto yatima!

Lakini pia kuna watoto wanaofanyishwa kazi za suluba na hata wakati mwingine kutumbukizwa katika mazingira hatarishi kama chambo cha uchumi wa familia au kwa baadhi ya watu waliokengeuka ambao hata wakati mwingine wanawajeruhi watoto wao ili waweze kuwatumbukiza katika biashara ya omba omba mitaani badala ya kwenda shule!

Kuna watoto wanaotolewa mimba hata kabla ya kuzaliwa, hivi ni vitendo vinavyofanywa na watu wakatili.


Kardinali Polycarp Pengo, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, amewataka watoto kusali kwa ajili ya kuwaombea akina Herode mamboleo ili waweze kutubu na kumwongokea Mungu kwa kusimama kidete kutetea Injili ya uhai tangu pale mtoto anapotunga mimba tumboni mwa mama yake, hadi mauti ya kawaida inapomfika kadiri ya mpango wa Mungu!


Amewataka wazazi na walezi kuwajengea watoto wao mazingira bora zaidi yatakayowawezesha kuwa ni mashuhuda amini wa Mtoto Yesu katika maisha yao. Waamini washinde ubinafsi kwa kuongozwa na upendo wa Mungu kwa ajili ya maskini na wahitaji zaidi.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii, anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi kusali kwa ajili ya kuwaombea watoto wanaoteseka sehemu mbali mbali kwa kutolewa mimba kabla hawajazaliwa; kwa kuteseka kutokana na baa la njaa na magonjwa na wale ambao wanabebeshwa silaha na kutumwa mstari wa mbele kama chambo kwenye mapigano.

Huu ni ujumbe makini kabisa unaotolewa na Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 28 Desemba 2017, Mama Kanisa anapoadhimisha Siku kuu ya Watoto Mashahidi waliouwawa na Mfalme Herode kwa hofu ya kupoteza kiti chake za kifalme, baada ya kuambiwa kwamba, Kristo Yesu, Mfalme wa Mataifa amezaliwa mjini Bethlehemu.

Tangu mwanzo, Mama Kanisa amewaangalia watoto hawa kama mashuhuda wa Fumbo la Umwilisho, watoto ambao hata kama hawakumwona Kristo Yesu, lakini walibahatika kupata Ubatizo wa Damu, kumbe, wao ni mashuhuda wa Kristo kwa njia ya sadaka ya maisha yao.

Mama Kanisa daima anafundisha kwamba, kifodini ni sadaka kubwa ambayo Mwenyezi Mungu hupenda kuwakirimia waja wake.

Siku kuu ya Watoto mashahidi wa imani ilianza kuadhimishwa kunako karne ya tano. Watoto hawa wanafuatana na mashuhuda wa imani kama Stefano shahidi na Mwinjili Yohane ambao daima wamekuwa mstari wa mbele kusimamia imani, utu na heshima ya binadamu.


Wakati huo huo , Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF linasema, Mwaka 2017 umeshuhudia idadi kubwa ya watoto duniani, ikikabiliwa na mashambulizi mbali mbali hasa huko Iraq, Siria, Yemen, Nigeria, Sudan ya Kusini na Myanmar, maeneo ambayo pia yametajwa na Baba Mtakatifu Francisko wakati akitoa ujumbe wa Noeli kwa Mwaka 2017 kwa ajili ya mji wa Roma na Ulimwengu katika ujumla wake, maarufu kama “Urbi et Orbi ”.

Huko nchini Nigeria na Cameroon, Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram kimefanya mauaji ya watoto 135. Huko DRC, watoto 850 wamelazimika kukimbia makwao. Takwimu zinaonesha kwamba, zaidi ya watoto 350, 000 wanakabiliwa na utapia mlo wa kutisha.
Hali ya maisha ya watoto Sudan ya Kusini ni mbaya sana kutokana na vita, njaa na utapiamlo wa kutisha. Zaidi ya watoto 19, 000 wamelazimishwa kwenda kupigana mstari wa mbele kama chambo na kwamba, zaidi ya watoto 2, 300 wameuwawa kikatili tangu vita ya wenyewe kwa wenyewe ifumuke upya nchini humo kunako mwaka 2013. Nchini Somalia zaidi ya watoto 1, 740 wameingizwa kwenye vikosi vya kijeshi na kupelekwa mstari wa mbele! UNICEF inawataka wadau mbali mbali kushikamana katika kuwahudumia watoto, ili waweze kupata chakula na lishe bora; elimu, malezi; ulinzi na usalama, ili waweze kufurahia maisha ya utoto wao!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!

My take: asante sana baba mwadhama kwa tafakari ya kimataifa.


Huyu mtu anaeitwa Pengo naona anatumia vimafumbo tu..come straight wewe mtu...
 
Ndiyo maana nasema kumlinganisha msomi wa theology kama Pengo na Kakobe kwadababu kawafurahisha ama kasema kile watu wanataka kukisikia bila kuweka uwiano na siku yenyewe ni kutokujua.
Pengo ni mtu makini sana katika homily zake.
Ni wachache sana wanaomwelewa
 
Nilitaka kuandika Neno zito la karne kwa huyo "Pango" sema nimekumbuka kuna Ban humu Jf

Kukomaa kwa demokrasia ni pamoja na kusikiliza hata yale yasiyopendeza masikioni mwako.....

Kwanini utake kumtusi mtu kwa kuandika au kuongea maoni yake...!!?kwa kuwa tu maoni yake hayakufurahisha wewe....!!!!?
 
ameandika nini kisichojulikana. haya ni mastory ya siku zote, miaka yote, karne zote. Sidhani kama ana reflection ya kinachoendelea hapa kuwa akina Ben wamepotezwa na mtu kulinda ufalme wake, NEVER!
Si lazima aongelee hayo mambo kila mara. Ameongea kutokana na maudhui ya siku husika. Kila tarehe 28 Desemba 2017 huwa anaadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya Watoto wa Utoto Mtakatifu, Jimbo kuu la Dar es Salaam.
 
Wakati Pope anaomba radhi kwa matendo yaliyotendwa na kanisa kipindi cha utawala wa Rumi Kadinali Pengo yeye bado anaishi nyakati hizo kwa kuambatana na utawala dhalimu.
 
Na kina Yuda Iskariote wa bandia wasiokwisha. Wanaoweza kumsaliti bwana wao mpendwa kwa busu murua...
 
Pengo ashanogewa breakfast ya ikulu aha
Acheni hizo, Kardinali Pengo hawezi kuwa mtegemezi hivyo wakati Jimbo analoongoza linatoa ruzuku nyingi tu sehemu nyingine za ukatoliki kutokana na kuwa na rasilimali za kutosha ikiwemo watu. Msidhani Pengo huwa anaongea yale kwa njaa njaa, ana maana yake ambayo pengine si lazima watu waijue, maana unaweza ukaweka vitu hadhharani ukasababisha vurugu
 
Back
Top Bottom