Ni kweli nchi ina matatizo tena mengi, kisiasa na kiutawala, kiuchumi, kifamilia na kijamii...yote hayo viongozi wetu wanapaswa kuyaangazia, wawe wa kidini au kijamii au kisiasa.
Pamoja na kuwa matatizo haya yote yanatofautiana athari zake kwa mtu mojamoja au jamii au hata taifa, sio vyema kabisa kulifanya tatizo moja liwe kubwa zaidi ya mengine maana kila tatizo ni kubwa kwa mwenye nalo.
Viongozi wetu wa dini ni wanajamii wenzetu, wanaona tunavyoishi na wanajua namna bora ya kushauri ili mambo yaende. Mtindo ulioanza wa kutaka wazungumzie aina fulani tu ya matatizo (ya kisiasa) ni mbaya sana. Wanasiasa ni wangapi na je wao wenyewe wameshindwa? Au hawajui kama wana shida?
Tunapofikia mahala tunataka hadi kuwapangia mahubiri viongozi wa dini eti kwa sbb ya demokrasia, haiwezi kukubalika. Viongozi wetu wanapaswa kuwa huru kutukemea sisi sote ktk upotofu wetu bila kujali tuko wapi, kama ni wanasiasa, watawala, mamantilie, wasomi wote tunapaswa kurekebishwa kwani maandiko yanasema "wote tumeoza".
Sasa inakuwaje kiongozi akemee " utoaji mimba" kwa mfano afu useme hafai kwa vile hajakemea ukosefu wa utawala bora ktk nchi? Kila kiongozi afundishe na awe huru kujiandaa kadiri ya hadhira yake na malengo yake kwa namna Mwenyezi anavyomuongoza. Hii "dhambi ya dunia" sasa naona inatutafuna watanzania ya kutaka kujitoa katika ukosefu na kumtafuta mkosefu mwingine mmoja kumvika dhambi zetu zote kama vile taifa zima ni la watakatifu isipokuwa mtu mmoja tu ndie mdhambi anaepaswa "kutubu" huku tukisahau ya kwetu ambayo nayo ni mengi.
Mwelekeo huu wa kuwataka makasisi na mashekhe wote wamuhubirie mtu fulani mmoja ktk nchi, wamkemee yeye tu, sisi watuache na maovu yetu, ni mwelekeo wa kishetani maana yeye ndie hupenda kuwachukua walio wengi na makuhani wa kweli lazima wanalijua hilo na tayari wamempiga chenga shetani.
Mintarafu makasisi wa kanisa katoliki wanafundisha kadiri ya utaratibu wa kanisa unaoratibiwa na vipindi vya mwaka wa kanisa na litrujia, kipindi kama hiki cha Noel, yanatolewa mafundisho ya kina kuhusu huruma ya Mwenyezi Mungu iliyomfanya achukue mwili aje kukaa kwetu binadamu na kutukomboa.,,,sitegemei watoke nje ya hayo kwa vile tu tunataka wamseme fulani, na wakimsema tuwapongeze, wasipomsema tuwachukie na kuwatukana.
Jamii yetu hasa vijana wengi wetu hasa humu mitandaoni hatuna kabisa hata sifa ya kumkosoa kiongozi yeyote wa kidini au wa kijamii, hali zetu ni mbaya, hatuna adabu wala nidhamu, hatuna malezi ya pande mbili, bangi pombe na madawa, ujinga na wengine tuna umwa akili zetu tunazijua wenyewe, faraja yetu kutukana, kuzini na kuiba eti ndo tunamkosoa hadi kadinari, kama sio tunatumiwa tu na nguvu za giza sio zaidi.
Chonde chonde viongozi wa dini zetu msiingie ktk mtego huu wa kufata matakwa ya mitandao ktk kufanya shughuli zenu za kichungaji, humu piteni nendeni, sikilizeni machache, tendeni mengi kadiri ya dhamiri zenu na tafakari zenu, msimpe shetani wa mitandaoni nafasi atazidi kutubomoa.
##tubu wewe kwanza kwa maovu yako mwenyewe## dhambi zako mzigo kwako utue##akitubu yeye ni faida kwake sio kwako wewe mdhambi mwenzangu usietaka kutubu###tutubu sote kwani hakuna alive mkamilifu###Mungu atusaidie##
Heri na baraka za mwaka Mpya ziwe nasi sote, amina.