TANZIA Kardinali Pengo afariki Dunia akiwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

TANZIA Kardinali Pengo afariki Dunia akiwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,360
Reaction score
3,742
Pumzika kwa amani mwadhama Kardinali Pengo. Tuonane mbinguni asubuhi iliyo njema.

=====

YAH: TANGAZO LA KIFO

Ninayo masikitiko makubwa kuwatangazieni kwamba leo tarehe 19/02/2026 saa 04:00 usiku huu mpendwa baba yetu Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, ameitwa nyumbani kwa Baba wa Milele akiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.

Taarifa za mazishi zitawajia mara baada ya mipango kukamilika. Tumwombee apumzike kwa amani.

Raha ya milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie, Apumzike kwa Amani; Amina.

Katika Kristo,

Thaddaeus S. Ruwa'ichi OFM Cap
Askofu Mkuu wa Dar es Salaam

IMG-20260220-WA0000.jpg
Soma Pia
 
Dahaah!

Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa yote na haswa kwa askofu na kadinali pengo .

Kanisa na taifa litamkumbuka kwa mchango mkubwa sana alio utoa katika nyanja mbali mbali, hata kama kulikuwa na makosa ya hapa na pale ila alikua na mchango mkubwa sana na siasa za Tanzania .


Nakumbuka sana mahubiri yake kwenye msiba wa mwalimu nyerere
20260220_011238.jpg
 
Back
Top Bottom