Karata ya Mahusiano Ilivyomnufaisha Harmonize (Konde Boy) katika mziki wake

ChizzoDrama

JF-Expert Member
Sep 29, 2019
1,317
1,229
IMG_c591on.jpg

Katika Ulimwengu wa Utandawazi wasanii wamebahatika kuwa na uwanja mpana sana wa kuzitangaza
Kazi zao, na moja ya karata muhimu ni mahusiano. Hii hutumiwa na wengi sababu ya urahisi wake (haina gharama).

Ukizingatia muziki, ndiyo kwanza matunda yameanza kuonekana hapa kwetu, tofauti na nchi kama Marekani. Kupitia mahusiano Harmonize amekuwa hakauki midomoni mwa Watanzania wengi, kubwa zaidi ni kuwa imemuongezea fan base, kwani wanawake wengi anaokuwa nao ni maarufu pia.

Wanawake hawa amewatumia kibiashara sana 'Iin the same of love'. Tunakumbuka alipoanza na Wolper aliachia ngoma ya Gambe na katika video ya wimbo huo alimtumia Wolper kama video queen, ngoma ilienda mjini na kuvutia wengi kuitizama.

images - 2023-05-13T135638.394.jpeg
Pia baada ya wawili hao kuachana, Harmonize, aliachia ngoma iitwayo Nishachoka, ilielezea zaidi nini kilicho tokea kati yao na kupelekea mahusiano yao kuvunjika. Hivyo kimsingi penzi hili lilizalisha ngoma mbili katika catalogue ya harmonize; Gambe (video) na Nishachoka.

Katika mafanikio ya Harmonize huwezi acha kumtaja Sarah, kimsingi huyu hakuwa maarufu lakini alikuwa na kitu muhimu zaidi ya umaarufu nacho ni Pesa. Huyu ndiye aliyesaidia sana Harmonize kusimama as solo artist. Pia hakuacha ipite hivihivi.
images - 2023-05-13T135538.765.jpeg

Ndani ya Goma liitwalo Niteke moja ya goma kutoka katika ep yake ya Afro Bongo lilifanya vizuri, jamaa hakuwa na hiyana ndani ya video akamtupia mzungu wake ndani, audio ilifanya poa na video ikaenda sana mjini. Penzi hili pia alinufaika nalo zaidi.

Ilikua dhahiri kuwa Harmonize hafanyi tu Muziki Biashara bali hata mapenzi kwake ni biashara. Hapo kati alimchukua Abriana, jamaa akaona kabisa she was just a gold digger, hakuwa na cha ku offer, hakuwa maarufu pia hakuwa na pesa, Harmonize akaona kabisa atatumia nguvu.

images - 2023-05-13T143403.344.jpeg

Fasta mtoto wa Kimakonde akazichanga vyema karata zake, ile (Puuuuuuf): nchi nzima inaimba Harmonize na Kajala, hapo script ilikuwa ndefu sana lakini director alicheza kama Pele.

images - 2023-05-13T135557.558.jpeg

Ilikua hivi;
● Public announcement
● Kajala kwenye management
● Vacations
● Engagement
● Tattoos
● Mkonga sagas
● Break up
● Range

Hapa konde alijipata haswa, penzi lilizalisha hits kibao kama;
♤ Mtaje
♤ Nitaubeba (video)
♤ Single again

Anko nchumari ukiacha kuwa anajua sana mziki, lakini upande wa drama amekuwa masta kabisa. Mahusiano yamemuongezea vingi kuliko alivyo poteza

Amefanikiwa amejipata sana✍✍
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom