Karamu ya vyakula uswazi (Top 10)

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Kwa kiingereza tungeita street food festival).

Hizi karamu sio za msimu bali zimekuwa sehemu ya maisha ya watu daily uswahilini, usijali sana ubora na usalama wake, vina ladha yake fulani ikikukamata huchomoki.

Hivi ni vyakula ambavyo hapo zamani kabla dunia haivua shumizi na kuvaa bikini vilikuwa vinapewa wanyama ama sana sana utavikuta kwenye vilabu vya pombe za kienyeji aka mataputapu, ila kwa dunia ya leo kila kitu ni dili hakuna kinachotupwa kwakuwa hata kondom yenye manii ina wateja

1. Supu ya mapupu/bandama ya ng'ombe
Hivi ni sehemu ya viungo vya ndani kwenye tumbo la ng'ombe lakini visivyo na thamani kama maini figo na utumbo. Hivi vinaitwa faida ya mchunaji, huwezi kuvikuta buchani. Siku hizi huko uswazi utavikuta jioni mitaani watu wakifurahia

2. Supu ya pua ya ng'ombe (sio kichwa)
Hii nayo ni mixer ya kongosho, koromeo, nyuchi kwa maana ya uke na njia ya uzazi na kwa uchache uume ambao siku hizi umekuwa dili sana kwa mambo mengine hivyo ni adimu kwenye supu

3. Mishkaki ya 100
Hivi vimishkaki vina addiction mbaya kabisa ni vitamu na ni laini balaa unaweza kujikuta unamaliza buku bila kutegemea, lakini unajua asili yake ninini? Mwanzoni vilikuwa sehemu ya faida ya mchunaji na mwamba ngozi.. Ngozi kabla ya kuwambwa hutolewa nyama zote sasa hizi huwa vinyama vidogo vidogo! Hivi havitupwi bali hutengenezwa huto tumishkaki twa mia. Kibaya ni kwamba baada ya soko kuwa kubwa wauzaji walifikia kuwalisha watu mpaka ndama waliofia tumboni, paka na umbwa! Hivyo unapokula sikilizia utamu wa ladha zaidi kuliko mengine

4. Mzigo wa kwio
Hapa ni kombinega ya kichwa(halohalo)
Miguu (no 11) na utumbo (cheni block)
Miguu inasokomezwa mdomoni na kutokea shingoni kisha utumbo unaviringwa kushikamanisha vizuri miguu na kichwa kisha vinakaangwa!
Utamu wake acha kabisa, baadhi ya mimba zimepatikana huku.

5. Korodani za mbuzi (wanga tupu)
Kituo maarufu kilikuwa Kwasokota Temeke nje ya ile bar nimeisahau jina.. Watu walikuwa wanatoka Kino kwenda Sokota kula kende za mbuzi za kuchoma! Siku hizi vituo ni vingi Uswazini

6. Supu ya ubongo wa ng'ombe
Hii ina watu wake na oda zake! Ila wengi huhofia kupewa supu ya ubongo wa kondoo maana ubongo wake una mdudu ukimla lazima dishi liyumbe

7. Supu ya jicho la ng'ombe
Hii nayo ina wateja maalum na sio wengi, na wao huitumia kwa mahitaji maalum. Wengi hawaipendi kwakuwa sometimes ikiwekwa kwenye bakuli ni kama lile jicho linakuangalia supu hii hujumuishwa na masikio ya ng'ombe pia

8. Kichuri (damu ya ng'ombe)
Mwanzoni ilikuwa ni kwa baadhi ya makabila lakini siku hizi uswazi unaikuta kichuri iliyokaushwa ikabanikwa nakuwa kama maini

9. Vyakula bahari (ngisi, pweza na kamba)
Mwanzoni vililiwa na watu wachache tena wa Pwani tuu, lakini siku hizi vinasafirishwa hadi mikoani.. Vinawamalizia pesa watu acha kabisa na ndio vyakula pekee ambavyo utavikuta uswazi na ushuani

10. Kacholi, sambusa, ndizi za kuchoma, kababu nk
Hivi ni visindikizi vya baadhi ya vyakula vingi vya vyama vilivyotajwa hapo juu na huwa pembeni yake hukosi mbilimbi, pilipili kachumbari nknk.. Kumbuka kwenye hizo sambusa kuna za nyama na za viazi. Lakini ni afadhali za viazi

Kati ya vyote hivi hakuna kinachozidi 2000 na bei ya chini ni shilingi mia.. Kwa sehemu kubwa ni vyakula visivyozingatia kanuni za afya na usalama wake kwakweli ni mdogo sana kuanzia maandalizi mpaka eneo la kuuzia.. Ila mwili wa binadamu una tabia ya kujibadili na kuendana na mazingira uliopo! Kuharisha na kutapika ni mara moja au mbili tu. Baada hapo ni mwendo mdundo

NB: Usiombe mkeo mjamzito mimba yake ikawa inataka kacholi na pweza wa Kwamtogole. Hata kama unakaa masaki utawasha gari uende na ole wako umpelekee za kwakopa atajua tu
 
2065236497_1630867582_xd.jpg
 
Kende za kondoo, tulikuwa tukiwapa vijana wadogo wa kati ya miaka 14 mpaka 18 wanaojiandaa kwenda jando.

Tukiamini ya kuwa, inakuza mshipa wa dhahabu.

Siyo unaenda kukatwa, una dudu ka la mtoto.

Lazima kuwepo na kibakizio baada ya govi kuondolewa.

Siku hizi hata wazee wanang'ang'ania.
 
Mbona kama umesahau kuweka supu ya kongoro...

Siku hizi pia kuna chapati za mwendokasi zile wanakaanga na vigodoro...
Iko kwenye zile supu nyingine lakini nimeangazia zaidi vyakula ambavyo unavipata mitaani tuu .. Supu ya kongolo ni mult purpose
 
Bro Mshana hujui siku hizi ngozi nayo ni dili tena inaliwa kama supu? Ni hivi, wanaibanika kutoa yale manyoya then inashemshwa na kutanuka, alafu inakatwa katwa vipande. Ukichanganyiwa na kongoro au utumbo huwezi kuigundua haha
 
Kwa kiingereza tungeita street food festival).

Hizi karamu sio za msimu bali zimekuwa sehemu ya maisha ya watu daily uswahilini, usijali sana ubora na usalama wake,
Kuna wakat pia ulikua unakuta Kaa na ngadu na haswa enzi hizo mitaa ya Magomeni pale mataa kabla haijarembwa vile.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom