Karamagi Kumshtaki Slaa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Karamagi Kumshtaki Slaa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kevo, Oct 22, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  HATIMAYE Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi, amevunja ukimya dhidi ya tuhuma za ubadhilifu na ufisadi zilizotolewa dhidi yake na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa, na wanasiasa wenzake wa upinzani na kutangaza kuwafikisha mahakamani ili kuthibitisha madai yao.

  Kadhalika, Bw. Karamagi ametangaza kulishtaki gazeti la kila wiki la Mwanahalisi lililoandika habari hizo na kiwanda kilichochapisha habari hizo cha Printech cha jijini Dar es Salaam.

  Bw. Karamagi alitangaza nia hiyo jana Jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari na kudai kuwa anajisikia vibaya kwa kuchafuliwa jina na kushushiwa heshima katika jamii.

  Aidha, Bw. Karamagi alisisitiza hatarajii ng?o kujiuzulu nafasi yake ili uchunguzi ufanyike kwa uhuru bila kuingiliwa na badala yake alisema tuhuma dhidi yake hazina ukweli.

  Katika hali iliyoonyesha kujichanganya, Bw. Karamagi jana aliwaambia waandishi wa habari kwamba hakusaini mkataba wa madini wa Buzwagi nchini Uingereza jambo lililowafanya wanahabari wote wagune.

  Hata hivyo, hakuweka bayana mkataba wa madini wa Buzwagi ulisainiwa wapi na mambo yaliyomo licha ya mara zote kuombwa na waandishi wa habari kuweka wazi mambo yote.

  Mkataba wa Buzwagi ni moja ya hoja nzito zilizotolewa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe dhidi ya Bw. Karamagi katika kikao cha Bunge la bajeti lililopita.

  Tuhuma hizo zilimfanya Bw. Kabwe kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge hadi mwakani kwa madai kwamba alisema uongo.

  Akiwa ameambatana na maofisa mbalimbali wa wizara yake, Bw. Karamagi alitumia muda usiozidi dakika tano kutoa msimamo huo na kisha kunyanyuka ukumbini na kutaka kuondoka huku akikataa kuulizwa maswali na waandishi wa habari.

  Hata hivyo, kabla hajatoka ukumbini waandishi wa habari walikuja juu hali iliyomlazimisha kurudi kwenye kiti na kuwaambia kuwa atajibu maswali matatu lakini kwa kifupi.

  Bw. Karamagi akiwa amehamaki hakujibu maswali ya waandishi wa habari kama alivyoulizwa na badala yake alishikilia msimamao wake na kuwataka wamuulize maswali yanayohusu kile alichokisema tu.

  Sakata hilo liliendelea kwa dakika 10 na baada ya hapo alinyanyuka tena na kutaka kuondoka lakini waandishi walimuwahi kwenye njia iliyo karibu na mlango wa kuingilia kwenye ofisi yake na kuanza kumbana kwa maswali.
  Hata hivyo, aliendelea kuwajibu kwa mkato.

  "Mimi leo sizungumzii mambo ya mkataba wa madini wa Buzwagi kwa kuwa sina ushahidi kama kulikuwa na mtu aliyeniambia mfisadi bali Dk. Slaa nimepata ushahidi wa kanda za video akinikashfu," alisema.

  Alisema Septemba 15, mwaka huu, katika mkutano wa hadhara huko Temeke Mwembeyanga Jijini Dar es Salaam, Dk. Slaa, aliutangazia umma wa watanzania kwamba Bw. Karamagi ni mfisadi na mbadhirifu mkubwa.

  Alisema alifanikiwa kupata kanda ya video iliyomrekodi Dk. Slaa na viongozi wengine wa vyama vya upinzania ambao hakuwataja majina wakati wakitoa madai hayo dhidi yake na kujigamba kwamba wana ushahidi wa yale wanayoyasema.

  Aidha, Bw. Karamagi alikataa kutaja mahakama atakayofungua kesi hiyo pamoja na mawakili watakaomtetea bali alisisitiza kwamba mpango huo utafanyika mara moja bila kuchelewa.

  Akiongea na Nipashe kwa njia ya simu juu ya hatua hiyo ya Bw. Karamagi, Dk. Slaa alimtaka afanye haraka kufungua kesi hiyo.

  Alisema ana mawakili wengi ambao wamejitolea kumtetea mahamakani bure.

  "Mimi nina uhakika na nilichokisema, tena afanye haraka kwenda mahakamani," alisisitiza Dk. Slaa na kuongeza kwamba huko mahakamani ndiko mengi zaidi yataibuliwa.

  "Mtu mwizi ni mwizi tu na sina jina lingine la kumuita bali kumuita hivyo," alisisitiza Dk. Slaa.

  Alisema vyama vyote vya upinzani vitashirikiana kujibu madai yao watakapofikishwa mbele ya mahakama ili hatimaye umma wa Watanzania upate kujua nani mkweli na nani mzushi.

  Aliongeza kuwa Bw. Karamagi anakabiliwa na tuhuma nyingine za rushwa kupitia kampuni ya kutoa na kupakia makontena bandarini (TICTS) ambayo ana hisa nyingi.

  Dk. Slaa alisema, maovu mengine ya Bw. Karamagi atayatoa leo atakapokutana na waandishi wa habari makao makuu ya CHADEMA ili kuendelea kumuanika hadharani.


  Hii habari Nimekutana Nayo Kwenye Gazeti la Rai.
  Imejaa vimbwanga kwa kweli!Yaani Karamagi anakataa hakusaini mkataba wa Buzwagi Uk na ndio anaona ni wakati wa kulishtaki gazeti la Mwanahalisi!
  JK kawarembulia macho sasa wanaona watuonyeshe wao ndio wenye nchi!
   
 2. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  hawajui kama ndo wanampaka uchafu mwenzao 2010 kwa wapiga kura???? no prob....let him....
   
 3. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  The Ironical Part Is that Karamagi wants to show us he is around and no one can mess with him!
  I hope nad pray to God that hata kama tapitishwa na kamati kuu ya CCM kugombea Ubunge 2010 watu kwenye constituency yake will give him a cold shoulder!
  He is too much kwa kweli!
   
 4. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  hana lolote huyu kadanganywa tuu na viwanasheria vyake ambavyo sanasana vinamlia helazake tu, mi nimeshasema .... let him... we are waiting
   
 5. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanzo mzuri
  Akifika mahakamani tutajajua na yale ambayo hatukuyajua mpaka sasa!
   
 6. M

  Masatu JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kevo hii habari ya mwaka juzi wewe unaiweka leo?

  Hivi huna habari kuwa waziri wa Nishati na Madini kwa sasa ni Mh William Ngereja?
   
 7. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mwenyewe nilifikiri labda kawaita jana hao waandishi wa habari maana sijasoma habari yote mpaka mwisho
  Good observation mkuu!
   
 8. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kabwe kasimamishwa tena?..

  Na karamagi kapewa wizara gani tena, siasa inabadilika haraka sana Tanzania, lakini bado ni ile ile.

  Hii habari ni mpya au inajirudia?..
   
 9. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  hii imerejea hapa kwa sababu za msingi au moderator amelala?
   
 10. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #10
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Hata mimi nashangaa...!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...