Karamagi asisitiza 'tulionewa'adai tume ya majaji iundwe

Kevo

JF-Expert Member
Jun 12, 2008
1,333
54
Karamagi bado kashikilia uzi palepale kwamba walionewa baada ya Mwakyembe kusema walizuia baadhi ya taarifa kulinda heshima ya serikali.karamagi kadai tume ya majaji iundwe ifanye uchunguzi zaidi.
 
Baadaye kwa kadiri hizi tume za uchunguzi zinavyoundwa kila kukicha, stoona ajabu kuona ikiundwa tume kuchunguza kama nchi hii tunayokaa kama ni kweli ni Tanzania
 
Tume, tume zimezidi, zinapoteza maana za tuhuma na hata hadhi ya tume na viongozi. Yote haya ni katika kulindana. Hata jambo lililo wazi badala ya kuchukuliwa hatua moja kwa moja inaundwa tume, mambo yanaenda kama mahakama mwizi anakamatwa live tuseme kaiba simu lakini anawekwa ndani anasubiri uchunguzi ukamilike. Mimi sielewi dhana nzima na utawala kwa nini hakuna uchukuaji hatua bali kuchelewesha na kisha tuhuma inapotea machoni kwa watu - inakwisha. Ndio maana hata maendeleo yetu pia hayaji, wananchi wengi maisha yao duni, tunasubiri tume pia.
 
Inaundwa tume....> wanawahonga kwa hela nyingi ..> wanassafishwa..> wananchi wanasahau..> ufisadi unaendelea..> Maishayanaendelea..> Umasikini unaendelea..
 
Dawa tunayo lakini hatutaki kuitumia, ni kutokipigia kura CCM na kuelimisha watanzania wasiojua hilo
 
Naona alitaka Raisi na PM wake ndiyo wawajibishwe kwani ndiyo walikuwa wenye dili..... kwani hata Lowassa alisema alijaribu kuizuia Richmond hakusikilizwa!!!!!!!! Jamani nani yuko juu ya PM??
 
Tume, tume zimezidi, zinapoteza maana za tuhuma na hata hadhi ya tume na viongozi. Yote haya ni katika kulindana. Hata jambo lililo wazi badala ya kuchukuliwa hatua moja kwa moja inaundwa tume, mambo yanaenda kama mahakama mwizi anakamatwa live tuseme kaiba simu lakini anawekwa ndani anasubiri uchunguzi ukamilike. Mimi sielewi dhana nzima na utawala kwa nini hakuna uchukuaji hatua bali kuchelewesha na kisha tuhuma inapotea machoni kwa watu - inakwisha. Ndio maana hata maendeleo yetu pia hayaji, wananchi wengi maisha yao duni, tunasubiri tume pia.

Dont ever forget hizi tume zinalipwa mamilioni ya fedha zikiwemo za usafiri,malazi hata kama wana lala kwao pamoja na hizo wanazoita sitting allowance.Huu ni ufujaji wa pesa.
 
Jamani tume zimezidi mno kuundwa au ndo miradi ya kujipatia fwedha??
Tume zinaundwa mafanikio na maoni/mapendekezo tunaona hayatekelezwi kabisa.
 
Karamagi bado kashikilia uzi palepale kwamba walionewa baada ya Mwakyembe kusema walizuia baadhi ya taarifa kulinda heshima ya serikali.karamagi kadai tume ya majaji iundwe ifanye uchunguzi zaidi.

Ifanye uchunguzi au awahonge kwa hela alizonazo. NO MORE TUME, Watanzania tunaheshimu maamuzi ya bunge kuliko anavyotaka yeye.
 
Huyu jamaa anataka tume coz Mwakyembe amesema walizuia baadhi ya taarifa ili kulinda heshima ya serikali.Sasa Karamagi insunuates hizo taarifa probably ni zakuwasafisha ndio maana he is pushing for tume ya majaji.
Ila he is so mistaken nadhani ndio watamuaribia vibaya zaidi.
 
Back
Top Bottom