Kachanchabuseta
JF-Expert Member
- Mar 8, 2010
- 7,263
- 685
Wana Jamvi
Niko jimboni Karagwe kama mwangalizi wa Uchaguzi (TEMCO).
Hivi sasa kikosi cha FFU kutoka Bukoba kimeingia na kuanza kurusha mabomu ya machozi mengi.
Kuna watu wapatao kama elfu kumi wamezingira ofisi ya tume wakidai itangaze matokeo ya ubunge.
Mabomu yameisha na sasa polisi wanatumia risasi za moto hewani. Watu wameumizwa na wengine wanakimbizwa hopsitalini.
Kuna tetesi kuwa Mgombea wa Chadema DEUSDEDITH JOVIN KAHANGWA amemshinda BLANDES GOSBERT wa CCM, lakini wakubwa wanakataa asitangazwe, bali Blandes ndiye atangazwe. Msimamizi wa Uchaguzi amejitahidi kukataa pressure kutoka kwa wakubwa lakini yaelekea sasa ananyonya mikono ili atangaze ushindi bandia kwa CCM. Hapahitajiki mabomu kumtangaza mgombea Chadema hapa maana maelefu ya watu wamekodi mafuso kuja kumlaki mbunge wao waliyemchagua.
Hii si dalili njema kwa Kikwete. Inabidi Kikwete na NEC wawajibike kwa lolote litakalotokea.
Viongozi wa Chadema waongeze makada kusaidia jitihada za kulinda zoezi la kujumlisha kura.Habari kutoka Karagwe zinadokeza kuwa kuna ugumu wa kutangaza matokeo na sasa polisi wanataka kuongezwa katika jitihada za kuwatawanya mashabiki wa Deusdedit ambaye ametarajiwa kwa kiasi kikubwa kushinda. Ikumbukwe kama ilivyotokea Nyamagana huyu kijana alienguliwa na msimamizi wa uchaguzi mwanzoni, alichelewa kuanza kampeni lakini akarudishwa na Tume ya Uchaguzi.
Habari kutoka Karagwe zinadokeza kuwa kuna ugumu wa kutangaza matokeo na sasa polisi wanataka kuongezwa katika jitihada za kuwatawanya mashabiki wa Deusdedit ambaye ametarajiwa kwa kiasi kikubwa kushinda. Ikumbukwe kama ilivyotokea Nyamagana huyu kijana alienguliwa na msimamizi wa uchaguzi mwanzoni, alichelewa kuanza kampeni lakini akarudishwa na Tume ya Uchaguzi.
Hao wanaokimbizwa si ndio wapiga kura wenyewe? Hii inji imeisha sasa.Mabomu yameletwa mengine na wanaendelea kuyamwaga kama njugu. Kibaya zaidi, sasa polisi wanawakimbiza watu hadi mitaani mbali na ofisi ya Mkurugenzi na hata wakikuta wamesimama zaidi ya mmoja wanawarushia bomu.
Nasikia Blandes alikuwa ameishakubali kushindwa na kuamua kuondoka tangu jana, lakini wenye mamlaka wamemuita arudi ili wamsaidie.
Habari ni kwamba watu wamepigwa vibaya na wengine wamekimbizwa hospitali.... Mtu waliyemchagua asiwe mbuge!!! Hiyo ndiyo demokrasia ya Demokrasia. Sitashangaa JK akitangazwa ushindi wa kishindo wa 100%+
Afu hawa polisi ni wapuuzi kweli,hawana akili hata kidogo...badala wamuache mpiganaji apite ili aje awasaidie coz wana shida kibao!
Look at their houses...
ccm kuanchia majimbo kwao ni issue
Watabana lakini wataachia tu pengine wana-test Dhali