GE2025 ‘Kapteni Tesha’ kawapa matumaini hewa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kufurahia allies wala si tatizo.

Tatizo ni kukosa nuance. Watu wana mentality ya all or nothing at all. Hero worship. Kutafuta mkombozi. Kutafuta silver bullet.

Ndiyo maana watu kama mimi au Nyani Ngabu tukija hapa na ku point out contradictions zinazooneshwa na habari ya kuwa euphoroc kwa video ya Kapteni Tesha, badala ya watu kukubali kuwa "Lakini kweli jamani, hapa tunamkubali Kapteni Tesha kwa hili na hili, lakini hili la kumsifia Magufuli na kumlilia is a red flag", hatuoni watu wengi kusema hilo.

Hatuoni watu wengi wakiwa na tatizo na dhana nzima ya utawala wa kijeshi.

Watu ndiyo kwanza wanataka wanajeshi wachukue nchi.

Utawala wa kijeshi si wa kidemokrasia.

Sasa watu wanadai demokrasia kwa kukumbatia utawala wa kijeshi?

That is a contradiction.
 
Ukishatoa hoja kuwa mimi ni mkimbizi tu niwaachie mambo yenu tayari ushanibagua kwamba sipaswi kuchangia kwenye mambo yenu.

Sasa hapo utasemaje hujanibagua?

Hoja ya "wewe uko mbali" haina mashiko. Kwa sababu mtu aliye mbali anaweza kuelewa na kuwa na hoja nzuri kuliko aliye karibu.

Natoa mfano mkali, si kwa kutaka kuwabagaza, bali kwa kutaka ku illustrate point. Mifano mikali inaweza kuchora picha vizuri zaidi.

Inawezekana nyie mlio karibu hapo mpo karibu na choo. Mmevita hewa ya mavi mpaka mmeizoea, hamjui hii ni hewa chafu.

Mnahitaji ntu anayetoka mbali anayevuta hewa safi aje hapo na kuwaambia hii hewa mnayovuta hapa si ya kawaida, inanuka mavi, ni uchafu, safisheni.

Wanasema kukaa karibu na msikiti si kuijua dini.

Jadili hoja, usimjadili mtoa hoja.

Kumjadili mtoa hoja negatively badala ya kujadili hoja ni kukosa hoja, ni logical fallacy.

Ad hominem logical fallacy.
 

Ww bakia na msimamo wako,
Huu ni muda wa kulipambania taifa haijalishi inatumika silaha Gani, lkn acha kabisa kuwaita watanzania desperate, waache wandelee kuipigania nchi yao kwa njia ambazo wanaimani zitawasaidia.
Unfortunately, hoja Yako Haina msaada wowote katika kulikomboa taifa hili.
 
hiii lugha hii lugha ya malkia imenyooka kushinda hata ya mwalimu wangu wa English wakati nasoma shule ya kwenda asubuhi na kidumu cha maji ,fagio,miiba+minyaa(kwa ajili ya kuweka uzio fensi),mbolea,majembe,mafyekeo (UTAFIKIRI UNAENDA VITANI)kumbe unaenda shuleni
,na unatembea kwa mguu,viatu unavaa,kaptula ,shati vyote ni ova size mzazi akinunua utakuwa navyo madarasa yote mpaka unamaliza shule navyo.

..ndio hii NGELI huku uswahili tunaita jamaa anatema YAI anabong'a UN'GEN'GE..
 
Usikariri, Tanzania siyo Rwanda, Syria, DRC. Ni muhimu kuisafisha hii nchi na kuondoa uchafu wote unaotuongoza sasa hivi. Tunapoendelea na huu utawala wa "kidemokrasia" machafuko hayazuiliki hivi karibuni.

Demokrasia ya genge la wahuni kufanya ufisadi bila kusumbuliwa na kulindwa na bunge, mahakama, polisi, tume haina tija.

Majority hawapendezwi na yanayoendelea. Hawana mbadala, njia rafiki kueleza kutopendezwa kwao.

Demokrasia ni nini, kama wengi wanaotaka haki, uwajibikaji wanapuuzwa, kutekwa na kuuwawa, kutupwa magereza.
 
Unamjibu wa nini huyo amejaa ujuaji sana.

Ukimjibu unampa bichwa anadhani points zake zina uzito.

Mwache ajifie kwa upweke huko Ulaya.
 
Huyo atabakia kuwa mkimbizi tu na Hana moral authority ya kuwapangia watanzania namna ya kupigania ukombozi wa TAIFA letu.
 
Maana yake kwako hata utawala wa kijeshi ni sawa tu.

Basi tuishi Mkuu. Hiyo siku nayo itafika. Hatuna sababu ya kubishana mtandaoni.
 
Sasa unaniambia nibaki na msimamo wangu.

Msimamo wangu ni kwamba Watanzania wengi, kwa kuangalia habari hii ya Kapteni Tesha angalau, wako desperate. Hawana logical consistency. Hawana high standard. Wana compromise mambo ya msingi kirahisi. Wana sacrifice core principles kwa sababu ya a little temporary security and convenience.

Halafu unaniambia nisiwaite Watanzania desperate.

Huoni kwamba unaji contradict hapo kwa kuniambia nibaki na msimamo wangu, halafu hutaki nibaki na msimamo wangu unanilazimisha nifuate msimamo wako?
 
Naunga mkono hoja
 
Umeelewa lakini? 😂😂😂
 
Maana yake kwako hata utawala wa kijeshi ni sawa tu.

Basi tuishi Mkuu. Hiyo siku nayo itafika. Hatuna sababu ya kubishana mtandaoni.
Nimeeleza hapo juu kwa kirefu. Ni utawala wa mpito wa kiraia wa Technocrats, wataalamu, wabobevu, wazalendo wakiongozwa na mtu kama Warioba kwa muda mfupi kuweka mambo sawa.

Nyuma yake jeshi jeshi lipo kuhakikisha wahuni, mafisadi, majambazi hawajuhumu mchakato wa kujenga nchi mpya yenye usawa, haki, uwajibikaji.

Unafikiri Samia angekuwa Rais kama sio kukingiwa kifua na Mabeyo, jeshi kuwa nyuma yake.

Nazungumzia kwa sasa jeshi lisimame nyuma kuwalinda wazalendo, haki, rasilimali za taifa, mchakato wa kujenga nchi inayojali kila Mtanzania badala ya kumlinda Samia na genge lake.
 
Tusubiri arudi tena ndio tupate hitimisho, kwasasa kusema haya ni mapema mno, ukiona mpya juu ya mti, lazima kuna mtu au watu nyuma yake. Tusipuuze
 
Nimekuuliza, kwa namna hali ilivyo sasa hivi, unaweza kwenda kupanga mstari kupiga kura?
 
nielewe wapi naokotoza
Umeelewa lakini? 😂😂😂
nielewe wapi baba, naokoteza okoteza neno moja moja najizoa zoa..aisee shule za ENGLISH MEDIUM za mabasi ya njano..zinasaidia naona wanangu akina junior nao wanagusa gusa wanadonoa donoa wanatema yai....japo tatizo naloliona HATA WALIMU WAO wanaowafindisha akina mwajuma nao ni kama mimi tu,ila wanajitahidi sio sawa na kumpeleka zile shule zetu za kata za kwenda na mapanga shuleni,mafyekeo,shoka ,madumu ya maji,mafagio..
kuna utofauti shule za english medium kama mzazi una uwezo mpeleke mtoto HUTOJUTA kumpeleka shule ya english medium mwanao kama unauwezo.
 
Huyo atabakia kuwa mkimbizi tu na Hana moral authority ya kuwapangia watanzania namna ya kupigania ukombozi wa TAIFA letu.

Jadili hoja, usijadili mtoa hoja.

Kijadili mtoa hoja kwa kashfa ya "huyu ni mkimbizi tu" ni logical fallacy, ad hominem logical fallacy.

Kuna logical consistency fulani inakosekana hivi. It irks me when logical consistency is violated willy nilly.

Kuna makosa fulani alifanya Magufuli akapewa pass, hata akatetewa ananyoosha nchi. Hayohayo anafanya Samia anashambuliwa vibaya sana.

Sasa nyie mnapinga haya makosa au hamumpendi Samia tu?

Nilitegemea wanaharakati wa demokrasia waoneshe contradictions kwenye suala zima la kumsifia Kapteni Tesha si tu kwa sababu ni mwanajeshi anayechochea mapinduzi ya kijeshi, jambo linalopingana nandemokrasia, bali pia kwa sababu kamsifia sana Magufuli.

Ila watu wanamsifia Kapteni Tesha bila kuona tatizo.

People see what they want to see, not what is there to be seen.
 
Hili linaweza kuwa kweli , usishangae watu wakijitokeza kupiga kura kwa wingi , vilaza ni vilaza tu.
Hata mimi naliona, sisi watanzania kwa ujumla wetu kwa bahati mbaya sana tupo tu tunaenda na namna upepo unavyoenda. Usishangae hata kidogo kuona mistari iliyoshiba watu wakisubiri kupiga kura.
 
Mkuu,

Wawekee watoto msingi mzuri. Halafu wajengee utamaduni wa kusoma vitabu vya Kiingereza vitawajenga sana.

Hapa tunapiga longolongo nyingi za siasa lakini hata kwenye siasa nimegundua Kiswahili kinatuangusha sana.

Tanzania imekuwa kama kisiwa kwa sababu watu wengi hawajui Kiingereza.

Na watawala wanatumia ujinga huu kama mtaji wa kuendelea kutawala.

Kiingereza hatuwezi kukwepa umuhinu wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…