Kapteni Komba: Tundu Lissu aende Jeshini

Kapteni Komba: Tundu Lissu aende Jeshini

yani komba nae anazungumzia uzalendo? kwani haoni matendo wanayo yafanya ccm? wanauwa watu wanateka watu wanatoboa macho wanawanyang'anya watu viwanja vyao, watu wakiona ufisadi unatendeka mbele ya macho yao wasiseme wanaweka roho zao rehani na huo ndio uzalendo? kabeba tumbo tu na mwili ila kichwani nothing.
 
hivi vi vihoja na vituko vingine vya viongoz wa ccm.....
 
Hii thread na post zake inaweza kuwa kati ya thread za kupasua mbavu zilizowahi kuwekwa humu kwa kipindi kirefu sana.
I just wish huyo mburula Komba angekuwa literate enough aingie humu asome habari zake za leo.

Kila post ni ukweli na inachekesha mno!
 
Anavituhumu vyombo vya habari kuwa vinaandika udaku lakini amesahau kuwa na yeye ni mmoja kati ya wanaoongoza kwa mipasho ndani ya ccm na kulala ndani bungeni wakati wa vikao
 
Komba ameshauri wabunge wanaochochea vurugu hapa nchini waende jeshini wakajifunze uzalendo waache kuhubiri siasa za ubaguzi. akatolea mfano wa mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni tundu lissu ambaye mara kadhaa amekuwa akiingia katika mgogoro na bunge kwa kusababisha vurugu na kutoweka kwa amani katika chombo hicho cha kutungia sheria za nchi.

Akaenda mbali na kusema kuna wabunge wanapenda kuuza sura na ndio wanahabari wanawapenda sana kuuzia habari zao.

Amevikemea vyombo vya habari kwa kuwa chanzo cha kukosekana kwa amani ya nchi kwa kuandika habari za udaku na vurugu na badala ya kuandika habari za maendeleo.

Kapteni Komba must be crazy.

Uzalendo ni swala la mtu binafsi kutoka moyoni mwake siyo mambo ya kujifunza Jeshini(JWTZ au JKT). Kwanza huko CCM kwenyewe kumejaa MAFISADI na WALA ARUSHWA wakubwa na walipita huko huko Jeshini......!!!

Jeshini siyo mahali pa kwenda kufundishwa umbumbumbu. Sijui Komba anazungumzia Uzalendo gani hapa? Maana nina uhakika zamani watu walikuwa wakienda JKT 12 months na leo wanapelekwa wiki 3 tu inasaidia kitu gani kama siyo mambo ya kisiasa na longolongo tu?.

Komba asitake kupotosha watu. Hana hoja hapa yeye aende zake kuimbisha kwaya ya TOT!!!!
 
Ila kwa taarifa tu wote na Mh. KAPTEN KOMBA pia..kutokana na historia ya Mh. LISU inaonekana ameenda jeshini kwa kipindi cha mwaka mmoja labda tu Mh. KOMBA angepitia CV ya Mh. LISU kabla hajamuhukumu. LAkini pia kupitia jeshini na uzalendo viko mbali mbali saana. Maana tunao viongozi ni wanajeshi kabisaa na ama walikuwa wanajeshi au pia wamepitia jeshini lakini ofisi zilizo na mamlaka zao zina ubadhilifu mkubwa, rushwa kubwa kubwa zinafahamika kuanzia EPA mbaka MEREMETA..au kukemea na kuisimamia serikali ni uchochezii!!! Kuiba na kula rushwa, kuhujumu mali asili ya nchi yetu ndio uzalendoo!!! Inatubidi tuwe makni sana tunapoongelea masuala ya uzalendo na Jeshini.."somtimes they are antonymous" Jeshini kunafundishwa utii na ujasiri sio uwoga na kupokea amri hata kama sio sahihi na endelevu.
 
He!Hadi Komba kapata cha kusema leo?Maana huyu namjua ni bingwa wa kulala bungeni na mwenzake Wassira,anafikiri jeshini ndio uzalendo unapatikana?Kweli wabunge wengi wa CCM fikra zao ni mbovu na hawana jipya.
 
when you go to equity you must go with clean hands,ndugu yangu Komba you have dirty hands,waache wenye clean hands waende kwenye haki,wewe utaangamia !
 
Ko.......mb......aaaaaa, kwanini usiende wewe ukapunguze hilo pakacha
 
Kwa nini asimshauri LULU aende shule kwanza kuliko kumuharibu?

images

Komba, huu ndi uzalendo wa jeshini??

Duuu nimecheka kweli Kama ndo hivi sitaki kwenda jeshini
 
Komba unastahili sifa kwa kuwa mkweli
Mafilili mtu mwingine anaweza kuitamka MAVIlili!
Komba ni mnafiki..Ashasema CCM bye bye kwenye bajeti ya Mwakyembe....
Hajui kwamba wanaoua tembo wetu na kutuingiza mikataba feki walipata ujasiri huo kutokana na mafunzo ya jeshi?!
 

Haya, Mheshimiwa umeanzisha vita kwa kutumia mawe, ilhali unaishi kwenye nyumba ya vioo. Ngoja sasa umiminiwe mawe, ndio uzalendo huo wa kutumia kodi ya Watz, halafu unabadilisha kiti za mjengoni kuwa kitanda ? Kwanda wewe unatakiwa kulipia hapo uko Lodge.
 
Naye alienda jeshini kuimba taarabu? Hivi huyu ana ukakamavu kweli? My hair
 
Hivi hajui kuwa lissu alishapiga kwata kitambo? Ngoja apate nafasi amchane. Kwaya mbali na hoja mbali.
 
Back
Top Bottom